makala mpya zaidi zilizoandikwa na Egidio Ndabagoye
Gumzo la moja kwa moja kuhusu Virusi vya ukimwi na Ukimwi mtandaoni Tarehe 6 machi
Mradi wa Rising Voices na Global Voices wanaandaa gumzo la moja kwa moja mtandaoni kwa wanablogu na wanaharakati siku ya Ijumaa mwezi wa tatu mwaka huu(saa 11 jioni kwa saa za Nairobi) mada kuu ikiwa jinsi ya kublogu na kuongeza uelewa na habari kuhusu virusi vya ukimwi na Ukimwi.
Iraki:OBAMAAAAA!!! Huraaah Oyee!!
Hivyo ndivyo asemavyo Neurotic Iraqi Wife. Kwa ujumla blogu nyingi za Iraki zimemchukulia vyema rais mteule Obama, lakini sio wanablogu wote waliofurahia. Salam Adil anaorodhesha maoni baada ya Uchaguzi wa rais huko Marekani.
Marekani ya Kusini:Taarifa,Twita kwa Waandishi wa Habari Yapata Umaarufu
"Reporting On" ni zana mpya ya kublogu kwa kifupi na inachukua umaarufu mkubwa katika kundi la wanahabari wa Marekani ya Kusini (Walatino) ambao wanatumia zana hii ili kupashana habari na wengine kuhusu yale wanayoyaandika.