makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mghosya kutoka Februari, 2014
Pongezi kwa Waziri Mkuu Mpya wa Nepal
Bunge la Nepal limemchagua Bw. Sushil Koirala (75), rais wa chama cha Nepali Congress, kuwa Waziri Mkuu wa Nepal. Mwanablogu wa NNepali aishiye ughaibuni Indra anampongeza Waziri Mkuu mpya na anafikiri kwamba “zawadi aliyonayo Bw. Koirala kwa kuwawezesha wengine kwa unyenyekevu na ukweli haitaondoka wa haraka”.
Mwandishi Mwandamizi wa Kichina Akosolewa kwa Kujifungulia Marekani
"...anachotaka tu ni mwanae awe na mtindo wa kawaida wa maisha, kitu ambacho hakina uhusiano na uzalendo. Labda, hili ndilo tatizo ambalo serikali yapaswa kulitafakari..."
Waandishi wa Habari za Kiraia, Jiandikishe Kupata Video Bure
Jukwaa linalokusanya video kadri zinavyowekwa mtandaoni linaloitwa Ustream linalota fursa ya kujiandikisha kufungua anuania mpya na pia kuzitangaza kwa ajili ya kuzitumia video hizo kwa ajili ya habari zinazotokea, uanaharakati na hata kwa matumizi ya mengine ya faida kwa jamii. Hivi karibuni Ustream imesaidia chaneli tatu za moja kwa moja...
Majadiliano ya GV: Maandamano ya Venezuela
Maandamano ya Venezuela yanahusu nini? Vyombo vya habari za kiraia vina wajibu upi? Tunazungumza na mwandishi wa Global Voices Marianne Díaz kuhusu hali ya mambo inavyoendelea nchini humo hivi sasa.
Maandamano ya Venezuela: ‘Vyombo vya Habari vya Kimataifa: Ingilieni Kati!’
Mpendwa Mhariri wa Kimataifa: Sikiliza na uelewe. Hali ya mambo imebadilika nchini Venezuela usiku wa kuamkia leo. Kile kilichokuwa kinaonekana kuwa hali ya kutokuelewana iliyokuwepo kwa miaka sasa imebadilika ghafla. Kile tulichokishuhudia asubuhi hii si habari ya Venezuela uliyodhani unaielewa. Kwenye blogu ya Caracas Chronicles Francisco Toro anashutumu kutokuwepo kwa vyombo...
Kiongozi wa Upinzani Nchini Venezuela Leopoldo López Ajisalimisha Serikalini
Kiongozi wa Upinzani nchini Venezuela Leopoldo López amejisalimisha mwenyewe kwa Vikosi vya Polisi, kama alivyokuwa ametangaza angefanya kwenye video [es] hiyo hapo juu. López, kiongozi wa chama cha Voluntad Popular, alitakiwa kujisalimisha kwa agizo la mahakama jijini Caracas kwa kutuhumiwa kuhusika na makosa ya jinai yanayohusiana na maandamano yanayoendelea nchini...
PICHA: Wavenezuela Waishio Ng'ambo Waungana na Waandamanaji
Wavenezuela wnaoishi nje ya nchi hiyo wameandaa maandamano kuunga mkono maandamano yanayoendelea nchini mwao. Picha zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwa alama za #iamyourvoicevenezuela #SOSVenezuela na #PrayForVenezuela, chache kwa kuzitaja.
Ghasia za Ukraine: “Kijana Alifia Mikononi Mwangu”
Mwanafunzi wa Kyiv, Ukraine alitwiti kuanzia alfajiri mpaka usiku wa manane wakati ghasia kati ya waandamanaji na polisi ziliposababisha vifo zaidi ya 25 na kujeruhi mamia
Mrembo wa Venezuela Auawa kwa Risasi Wakati Akiandamana
Genesis Carmona ameuawa kwa risasi iliyomjeruhi kichwani. Amekuwa mwathirika wa maandamano yanayoendelea nchini Venezuela.
Fuatilia Kuenea kwa Maandamano ya Ukraine
Maandamano yamechukua sura mpya tarehe 18 Februari, na Ukraine sasa imekuwa uwanja wa mapambano baina ya mamia ya maelfu ya raia na vikosi vya ulinzi.