makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mghosya kutoka Februari, 2015
Filamu: ‘Sanaa ya Ama Ata Aidoo’
The Art of Ama Ata Aidoo ni filamu iliyotayarishwa na mtayarishaji wa filamu Yaba Badoe: The Art of Ama Ata Aidoo, inasaili mchango wa kisanii wa mmoja wa waandishi wanawake mashuhuri barani Afrika, anayeongoza kizazi hiki kwa kipaji kipya cha pekee. Dokumentari hii inasaili safari ya ubunifu ya Ama Ata...
Hofu ya Yaliyotokea? Likizo ya Rais Mpya wa Zambia Yaibua Mjadala wa Afya Yake
Raia wa Zambia wanajiuliza maswali kuhusu afya ya Rais Lungu, pamoja na cheti cha afya kuonesha yu mzima, kufuatia likizo yake majuma mawili tu tangu ashike madaraka kumrithi Michael Sata, aliyefariki akiwa madarakani.
GV Face: Maandamano Yazuiliwa na Waasi wa Houthi Nchini Yemen
Yemen iko kwenye mzozo wa kisiasa, bila kuwa na rais na serikali, tangu wanamgambo wa Houthi kuangusha taasisi za kiserikali na kuiteka ikulu kwenye mji mkuu wa Sanaa
Msichana Achora Ramani ya Palestina kwa Kutumia Risasi za Israeli Alizokusanya Karibu na Nyumbani Kwao
Picha hii ya msichana wa ki-Palestina inazunguka kwenye mitandao ya kijamii. Taarifa zinasema msichana huyu alikusanya maganda ya risasi karibu na nyumbani kwao, akayatumia kuchorea ramani ya Palestina.
Vijana wa Naija Wacharuka Kufuatia Shambulizi la Boko Haram huko Bosso na Diffa
Kwa mara ya kwanza, Boko Haram kimetekeleza shambulio kwenye mpaka na Naija na vijana wa ki-Naija hakuweza kuvumilia. Boko Haram walishambulia Bosso na Diffa, miji miwili iliyo kusini mashariki mwa Naija kwenye mpaka wa nchi hiyo na Naijeria lakini walirudishwa nyuma na majeshi ya Chad na Naija. Boko Haram imepoteza...
Boko Haram Yaua Watu Wasiopungua 81 Huko Fotokol, Cameroon Kaskazini
Mnamo Februari 4, Boko Haram walifanya shambulio baya kwenye mji wa Fotokol Kaskazini mwa Cameroon, baada tu ya kuvuka mpaka wa Naijeria. Mamia wa raia wanahofiwa kupoteza maisha 81 wamethibitika kufa na Wizara ya Ulinzi. Shirika la Haki za Binadamu nchini humo linaamini kwamba karibu watu 370 wameuawa. Mashuhuda wa...
Wafilipino Wauliza ‘Rais Yuko Wapi?’ Baada ya Kutokuonekana Kwenye Mapokezi ya Polisi Waliouawa
Polisi arobaini na wanne walipoteza maisha yao kwenye operesheni maalum ya kumkamata mtu anayedaiwa kuwa mhusika mkuu wa mabomu ya Bali ya mwaka 2002. Rais Aquino alihudhuria uzinduzi wa kiwanda cha magari badala ya kupokea miili ya polisi hao
Baada ya Miaka 29 Madarakani, Rais wa Uganda Museveni Hana Mpango wa Kung'atuka
"Kwa hiyo ni rasmi. Hakuna demokrasia nchini Uganda. Museveni na Jeshi lake ndio kila kitu."
Serikali ya Masedonia Yazuia Kupiga Picha za Maandamano kwa Kutumia Kamera za Anga
Video na picha zilizotengenezwa kwa kutumia kamera inayopaa angani zilikuwa nyenzo muhimu ya kuonesha ukubwa wa maandamano ya wanafunzi, ambayo yameitwa maandamano makubwa ya wanafunzi kuwahi kutokea nchini Masedonia tangu uhuru.