makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mghosya kutoka Mei, 2014
Uchaguzi wa Malawi 2014
Malawi inapiga kura kumchagua rais siku ya Jumanne Mei 20, 2014. Fuatilia taarifa za moja kwa moja kwenye mtandao wa Twita @Malawi2014 na @MEIC_2014.
PICHA: Watu 20,000 Waandaman huko Macau China Kupinga “Muswada wa Ulafi”
Muswada utampa mkuu wa serikali jimboni Macau, nchini China, kinga ya kushitakiwa kwa makosa ya kijinai wakati akiwa madarakani na ataaendelea kupata mshahara wake hata baada ya kuondoka madarakani.
“Hatujaweka Mkazo vya Kutosha Kwenye Afya ya Vijana”
Ripoti ya hivi karibuni kutoka kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu afya ya vijana duniani inabainisha kwamba: Sababu kubwa za vifo vya vijana duniani ni ajali za barabarani, VVU?UKIMWI, na kujiua. Duniani kote, wastani wa vijana milioni 1.3 walipoteza maisha yao mwaka 2012. Ripoti inaongeza vile vile kuwa :...
Mazungumzo ya GV: Kupigania Kuachiliwa Huru kwa Wanablogu wa Ethiopia wa Zone 9
Wanablogu tisa ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari ---wanne wao wakiwa ni wanachama wa Global Voices ---wanashikiliwa nchini Ethiopia kwa sababu ya kutekeleza majukumu yao. Fahamu namna ya kuunga mkono kampeni ya #FreeZone9Bloggers!
Mzee wa Kimasedonia Apambana Kurejeshewa Mali Yake
Mwanablogu wa Kimasedonia anayeitwa Dushko Brankovikj, ambaye mali zake zimetaifishwa mara mbili, ameshinda kesi, lakini serikali haijaweza kumrudishia mali zake.
Global Voices na Connectas Watangaza Kushirikiana Maudhui
Global Voices itachapisha maudhui yanayoandikwa na CONNECTAS, mradi wa kiuandishi kwa Bara la Amerika Kusini uliopo nchini Columbia.
Ungana na Kampeni ya #FreeZone9Bloggers Twita Mei 14
Ungana na wanablogu wa Global Voices kwa ajili ya kampeni ya kutwiti barani Afrika kwa ajili ya kuunga mkono wanablogu na waandishi wa habari tisa waliokamatwa mwishoni mwa mwezi Aprili na kwa sasa wako rumande nchini Ethiopia.
China Yamweka Kizuizini Mwanasheria wa Haki za Binadamu Pu Zhiqiang
Hii si mara ya kwanza kwa Pu Zhiqiang kuwekwa kizuizini. Akiwa mkosoaji maarufu wa sera za serikali ya China, amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na vyombo vya usalama wa nchi hiyo.
Wazimbabwe Wamkejeli Tsvangirai Kwenye Mtandao wa Twita
Lipi ndilo jina sahihi la kitabu cha kufikirika kumhusu Morgan Tsvangirai aliyetimuliwa na chama chake? Watumiaji wa mtandao wa Twita wana mapendekezo kadhaa
PICHA: Waandamanaji Nchini Taiwani Wageuza Uzio wa Polisi kuwa Mapambo
Polisi waliweka uzio wa kuwapa tahadhari waandamanaji kuzunguka majengo ya serikali katika jitihada za kuwazuia waandamanaji kukusanyika. Wataiwani wakawajibu kwa kile kinachoonekana kuyageuza mabango hayo ya tahadhari kuwa mapambo.