Albert Kissima · Julai, 2013

makala mpya zaidi zilizoandikwa na Albert Kissima kutoka Julai, 2013

Saudi Arabia: Familia za Wanaoshikiliwa Gerezani Zaandamana

Familia za watu wa Saudi Arabia wanaoshikiliwa gerezani yaingia siku ya tatu ya kupinga kushikiliwa kwa wapendwa wao bila sababu maalum. Saudi Arabia ni moja ya nchi chache duniani ambazo bado zipo chini ya mfumo wa utawala wa kifalme na ina rekodi isiyoridhisha kuhusu haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kushikilia gerezani zaidi ya watu 30,000 bila sababu maalum.

Global Voices Yazindua Ushirikiano na Shirika la NACLA

Global Voices na Shirika la Marekani Kaskazini Linaloshughulika na Amerika Kusini (NACLA) wameanzisha ushirikiano mpya ambao utaleta kwa pamoja dira ya Sauti za Dunia ya habari za kiraia na na ile ya NACLA ya uchunguzi na utoaji wa elimu, lengo likiwa ni kuwaletea wasomaji wetu habari halisi na za kina kutoka katika eneo hili la Latini Amerika.

Benin: Kampeni ya Kusaka Wahalifu Yawagawa Wananchi

  7 Julai 2013

Ikiwa imezinduliwa na wizara ya Mambo ya Ndani, Ulinzi wa Umma na Dini, kampeni ya Djakpata yenye lengo la kuwasaka wahalifu wote wanaojihusisha na shughuli zisizo halali ambazo zinaweza kuhatarisha hali ya utulivu ya wananchi wa Benin. Hata hivyo, kwa siku chache zilizopita, wananchi wamekuwa na maoni tofauti sana kuhusu jambo hili.

Mama na Watoto Wake Wauawa kwa Kucheza kwenye Mvua

  6 Julai 2013

Mama na watoto wake wawili wa kike waliuawa kwa kufyatuliwa risasi mara baada ya watu watano waliokuwa wamefunika nyuso zao kuvamia nyumba alimokuwa akiishi mama huyu na watoto wake katika mji mdogo wa Chilas nchini Pakistan, tukio linalosadikiwa kuwa ni la mauaji ya kulinda heshima. Video iliyorekodiwa kwa simu inayowaonesha wasichana hao wakicheza kwenye mvua imekuwa ikisambaa kiholela na ambayo imeonekana kama ni kashfa na hivyo kuharibu heshima ya familia.

China Yawaamrisha Vijana Kuwatembelea Wazazi Wao

  6 Julai 2013

Wiki hii, China imeanza kutumia sheria mpya inayowataka watoto waliokwisha fikia umri wa kujitegemea kuwa na mazoea ya kuwatembelea wazazi wao, hali iliyopelekea sheria hii kudhihakiwa na watumiaji wa tovuti ya jukwaa maarufu la wanablogu la China lijulikanalo kama Sina Weibo.

Raia wa Misri Wamng'oa Morsi Madarakani

Mohamed Morsi, ambaye ni kiongozi mkuu wa chama cha Muslim Brotherhood siyo tena Rais wa Misri. Morsi ameondoshwa madarakani baada ya kutumikia kwa mwaka mmoja kama Rais mara baada ya maandamano makubwa nchini kote Misri yaliyomtaka kujiuzulu, maandamano hayo yalianza mapema mwezi Juni 30. Mkuu wa majeshi ya Misri, Generali Abdel Fattah Al Sisi, katika matangazo ya mojakwa moja dakika chache zilizo pita, alisema kuwa, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Katiba ndiye atakayekuwa Rais mpya wa mpito na kwamba serikali ya kitaifa ya Kiteknokrasia itaundwa.

Misri: Wasalafi Washambulia Makazi ya Washia, Wanne Wauawa

Watu wanne nchini Misri ambao ni wafuasi wa imani ya Shia wameuawa leo nchini Misri mara baada ya nyumba waliyokuwa wanakutania kushambuliwa na Waislam wenye msimamo mkali, shambulio hili linafuatia wiki mbili za uchochezi dhidi ya waumini wa Shia. Kwa mujibu wa taarifa za awali, nyumba ambayo waumini hao wa Shia waliyoitumia kukutania, iliyopo huko Giza, Cairo, ilishambuliwa na kuchomwa moto. Kwa mujibu wa taarifa za habari za Al Badil, shuhuda mmoja alikaririwa akisema kuwa mmoja wa watu waliouawa alichinjwa na wengine watatu walijeruhiwa vibaya vichwani mwao. Tukio hili la kutisha lilizua ghadhabu kubwa mtandaoni.