makala mpya zaidi zilizoandikwa na Albert Kissima
Mwandishi wa Habari wa Thailand na Wakosoaji Dhidi ya Serikali ya Kijeshi Wakabiliwa na Makosa ya Uchochezi Kupitia Facebook

"Nitaendelea kuikosoa serikali batili ya kijeshi hadi watakaponinyang'anya simu janja yangu."
Salvador Adame ni Mwandishi wa Habari wa Saba Kuuawa Nchini Mexico Tangu Mwanzoni mwa 2017
"Ukweli haufi kwa kumuua mwandishi wa habari."
Kubaki au Kuondoka Hakutoi Mustakabali wa Wakazi wa Al-Waer Nchini Syria
Waasi pamoja na familia zao wanaihamisha ngome yao kutoka kwenye jiji hili lililobatizwa jina la "Kitovu cha Mapinduzi". Hizi hapa ni baadhi ya simulizi zao.
Makosa ya Uhalifu wa Mtandaoni dhidi ya Mwanzilishi wa Kampeni ya Jeshi la Manyanga Yafutwa
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Seriakali ya Jamaica amemfutia mashitaka yote matatu yaliyokuwa yakimkabili mwanaharakati La Toya Nugent, chini ya sheria ya nchi ya makosa ya uhalifu wa Mtandaoni.
Wito wa Kimataifa wa Kudai Haki Wawaunganisha Wachoraji Nchini Guatemala
Ni miezi miwili sasa tangu wasichana 41 kuuawa kwa kuchomwa moto kwenye nyumba ya kulelea watoto inayosimamiwa na serikali. Hata hivyo, serikali ya Guatemala imekuwa imekuwa ikisuasua kwenye kuchukua hatua.
Mwanablogu na Mwanaharakati wa Maldives Yameen Rasheed Auawa kwa Kuchomwa na Kitu chenye Ncha Kali
"Ile inayoitwa" Paradiso ya duniani haihakikishii raia wake usalama. Kesho inaweza kuwa ni mimi, wewe au yeyote miongoni mwetu," aliandika mtumiaji mmoja wa Facebook.
‘Kwa nini Siwezi Kumbusu Mpenzi wangu wa Kike Hadharani?’ Simulizi ya Mwanamke Basha wa Armenia
Mwanamke basha aweka bayana historia ya maisha yake na kueleza harakati zake zenye changamoto lukuki za kuwakomboa wasagaji kutoka kwenye jamii ya mfumo dume isiyoamini uhusiano wa kimapenzi wa watu wa jinsia moja.
Salamu ya Siku ya Wajinga Kutoka Ubalozi wa Urusi

Tarehe 1 Aprili ni siku ya wajinga Duniani. Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imekuja na mzaha wake.
Unamjua Muuaji Mkuu Nchini Georgia? Ni Barabara Zake
Mnamo Machi 22 huko Tbilisi, mama mmoja pamoja na mtoto wake wa kike waliokuwa wamesimama kando ya barabara waligongwa na gari. Msichana huyo wa miaka 11 alipoteza maisha papo hapo.
Kilicho cha Zamani ni Kipya: Unasikiliza? Matangazo ya Sauti
Katika matangazo haya ya sauti, tunakupeleka hadi Jamaica, Indonesia, Syria, Macedonia na Ethiopia kwa simulizi za kumbukumbu, ufufuaji na uzima mpya