Habari kutoka Oktoba, 2014
Walidanganya Mpaka Amefariki: Serikali ya Zambia Yakiri Ugonjwa wa Rais Mauti Yalipomkaribia
Rais wa tano wa Zambia, Michael sata, alifariki Oktoba 28, 2014. Wa-Zambia wanahoji uamuzi wa serikali hiyo kushindwa kuliambia taifa ukweli wa afya yake.
Wakati Taiwani Ikifikiria Usawa wa Haki ya Ndoa, Maelfu Wahudhuria Matembezi ya Mashoga
Matembezi ya watu wenye mapenzi ya jinsia moja yamefanikiwa mwaka huu huko Taiwani. Wapenzi wawili mashoga katika hali ya kujawa matumaini walivaa fulana zenye ujumbe kuwa wanajiandaa kuoana
Jiandikishe Sasa kwa Mkutano wa Global Voices 2015: Januari 24-25 jijini Cebu, Ufilipino
Jiandikishe sasa kwa ajili ya Mkutano wa Global Voices 2015 jijini Cebu, Ufilipino, utakaokusanya wanaharakati na waandishi wa kiraia kutoka duniani kote.
Miaka 50 Baadae, wa-Zambia Wanajiuliza Nini Maana ya Uhuru
Wakati wa-Zambia duniani kote wakisherehekea siku kuu hiyo kwa vyakula, rangi rasmi za nchi hiyo na chochote walichoweza kukifanya, baadhi ya wachunguzi wa mambo waliibua maswali mazito kuhusu historia na mustakabali wa nchi hiyo.
Salamu ya ‘vidole vitatu’ Yaleta Matumaini kwa Wanaharakati wa Demokrasia Nchini Thailand
Wahudhuriaji wa mazishi ya afisa wa zamani wa serikali walionesha ishara ya vidole vitatu ambayo inatumiwa na wanaharakati wanaopigania demokrasia nchini Thailand.
‘Uandishi na Vyombo vya Habari Katika Kuleta Dunia Bora Zaidi': Mkutano wa Taasisi ya Transformational Media 2014 Jijini DC
Washiriki wa Mkutano wa TM watajadili uandishi, ubunifu, teknolojia mpya, bishara na maisha enedelevu, ustawi na afya, upigaji picha, filamu na muziki,uandishi wa habari, pamoja na mambo mengine
GV Face: ‘Tupige Kura au Tusipige'? Sauti za Raia wa Tunisia Katika Uchaguzi Unaokaribia
Zaidi ya wagombea 9,000 wa vyama zaidi ya 100 wanagombea kwenye uchaguzi wa mwaka huu
Kutangaza Mkutano wa Global Voices, Dar es Salaam, Novemba 2, 2014
Mkutano wa kwanza unaowakutanisha waandishi na watafsiri wa Global Voices na wadau wa Uandishi wa Kiraia hapa nchini unafanyika Dar es Salaam, Tanzania
Wenyeji wa Visiwa vya Pasifiki Waizuia Meli za Makaa ya Mawe Kupinga Mabadiliko ya TabiaNchi
Kwa kutumia ngalawa zilizotengenezwa kwa mkono, washujaa wa mabadiliko ya tabianchi, wakishirikiana na raia wa Australia, waliweza kuzuia meli 10 zilizokuwa zitumie bandari ya Makaa ya mawe ya Newcastle.
Hukumu ya Haki? Ina uzito wa Kutosha? Oscar Pistorius Amehukumiwa Kifungo cha Miaka Mitano Jela
Mkimbiaji wa Afrika Kusini aliyepatwa na hatia kwa kumwuua pasipo kukusudia rafiki yake wa kike Reeva Steenkamp imelinganishwa na hukumu ya jangili aliyefungwa miaka 77 jela kwa kumwuua faru mwezi Julai