Habari kutoka Februari, 2013
Bulgaria: Gharama Kubwa za Nishati Zasababisha Maandamano
Ruslan Trad anataarifu kuwa, siku ya Jumapili tarehe 17 Februari, makumi ya maelfu ya watu katika mji mkuu wa Bulgaria, Sofia pamoja na majiji mengine waliendelea na maandamano kupinga bei kubwa za nishati ya umeme pamoja na gharama za kupasha joto.
Bulgaria: Pamoja na Serikali Kujiuzulu Maandamano Yapamba Moto
Maandamano nchini Bulgaria yanaendelea: Ruslan Trad anataarifu kutoka mji mkuu wa Bulgaria kuwa, siku ya Jumapili, huko Sofia na katika majiji mengine, makumi ya maelfu ya watu waliandamana kupinga rushwa, gharama kubwa za huduma za jamii pamoja na umasikini.
Vurugu Zinazofadhiliwa na Serikali Nchini Angola
Mwanablogu Claudio Silva anaandika kwenye makala yake Africa Ni Nchi kwamba mtazamo wa kina juu ya vurugu zinazofadhiliwa na serikali (kufukuzwa watu mijini na kupigwa kwa waandamanaji) unahitajika ili kuelewa...
Udhaifu wa Watawala wa Afrika unajionesha Mali?
Ousmane Gueye katika tovuti ya Mondoblog anaandika [fr] kuhusu kuchelewa kupeleka vikosi vya kijeshi kasikazini mwa Mali: Kama tungekuwa tunasaiili matokeo ya watu wenye amani na huru kuingilia kati hali ya...
Wakati Papa Anajiuzulu, Warusi Wajiuzulu kwa Putin
Pasipokutaka kujua matokeo ya kujiuzulu kwa Papa Benedict na athari yake kwa imani ya Kikatoliki au tafsiri ya hatua hiyo kufuatia kashfa ya udhalilishaji iliyowakabili kwa watawa, RuNet walioweka habari hiyo kwenye safu za vichekesho.
Hali ya Hatari kwa Watoto nchini Syria: Namna Utakavyo Saidia.
Hadi sasa,inakadiriwa watoto 4,355 wameshauawa katika mgogoro unaoendelea hivi sasa nchini Syria. Mapema wiki hii, tulitoa taarifa juu ya madhila wanayokabiliana nayo watoto wa Syria kufuatia vita hii inayoisambaratisha nchi yao vipande vipande. Leo tunaangalia namna ambavyo watu wanaweza kusaidia kukabiliana na baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo.
PICHA: Maandamano ya Pamoja ya Watu wa Shia Nchini kote Pakistan Yamalizika Kwa Amani.
Baada ya milipuko ya mabomu huko Quetta kuua zaidi ya watu 100, maanadamano ya watu wa jamii ya Hazara ya Shia yalisambaa kama moto katika maeneo mbalimbali ya Pakistani. Watu kutoka katika makundi makuu ya dini na makabila mbalimbali waliungana kwa pamoja na watu wa Hazara wakiimba kwa kurudiarudia#Sisi sote ni watu wa Hazara. Maandamano ya kuishinikiza serikali kusikiliza madai yao yalianzishwa katika zaidi ya majiji 100 na miji.
Blogu 10 Bora za Mapishi ya ki-Afrika
MyWeku anatengeneza orodha ya Blogu 10 bora za Mapishiya ki- Afrika kwa mwaka 2013: “Inaonekana kuna blogu milioni moja zinazozungumzia mapishi, lakini ni chache sana zinazoonyesha vyakula vya Kiafrika. Pamoja...