Januari, 2013

Habari kutoka Januari, 2013

Mwaka Mpya na Mienendo ya Zamani Nchini Bahrain

Wakati nchi mbalimbali ulimwenguni kote zikiukaribisha mwaka mpya kwa fataki na shamrashamra, serikali ya Bahraini iliandaa utaratibu wa aina yake kwa waandamanaji nchini humo. kwa bahati, watumiaji wa mtandao wa intaneti walikuwa tayari, kuonesha na kuweka kumbukumbu ya baadhi ya matukio kwa ajili ya kushuhudiwa na sehemu nyingine yote ya ulimwengu.

Bangladeshi: Msichana Mwingine Mzawa Abakwa na Kisha Kuuliwa.

  2 Januari 2013

Kwa mara nyingine msichana mzawa ameuawa nchini Bangladesh baada ya kubakwa kikatili. Mhanga huyo, Khomaching Marma (14) alikuwa mwanafunzi wa darasa la nane. Ubakaji huu wa kikatili uliosababisha mauaji kwa mara nyingine tena umeamsha hasira na ghadhabu nchini kote. Watumiaji wa mtandao pia wanapinga vikali vitendo hivyo.