Septemba, 2012

Habari kutoka Septemba, 2012

Kenya: Wito wa Mshikamano Baada ya Mashambulizi ya Kigaidi

Siku chache kabla ya ufunguzi  wa GV2012 mjini nairobi, Kenya ilikumbwa na milipuko na utekaji nyara huko Mombasa na mjini Garissa. Mlipuko ulitokea katika sehemu ya burudani mnano Juni 24 na kuwauwa watu watatu siku moja baada ya ubalozi wa marekani kuonya mamlaka ya Kenya kuhusu mashambulizi hayo jijini. Umati huo ulikuwa umekusanyika katika kilabu kutazama robo fainali  kati ya Uingereza na Italia.

30 Septemba 2012

India: Waume Kuwalipa Wake Zao kwa Kufanya Kazi za Nyumbani

Wizara ya Maendeleo ya Watoto na Wanawake nchini India inaandaa mswada ambao, kama utapitishwa na bunge, utawalazimisha waume kisheria kuwalipa wake zao wanaoshinda nyumbani mshahara wa mwezi, kwa kufanya shughuli za nyumbani. Wizara ya Maendeleo ya Watoto na Wanawake nchini India inaandaa mswada ambao, kama utapitishwa na bunge, utawalazimisha waume kisheria kuwalipa wake zao wanaoshinda nyumbani mshahara wa mwezi, kwa kufanya shughuli za nyumbani.

30 Septemba 2012

Je, Sifa ya ‘Kisiwa cha Amani’ Tanzania Imeanza Kutoweka?

Tanzania imeshuhudia matukio kadhaa mabaya tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa 2010. Tukio la hivi karibuni ni kifo cha kikatili cha mwandishi wa habari wa Tanzania Daudi Mwangosi, aliyeuawa kwa bomu la machozi huko Iringa, Kusini mwa Tanzania, wakati polisi walipojaribu kukitawanya kikundi cha wafuasi wa chama cha upinzani.

19 Septemba 2012

Afrika: Tuzo la Mbuyu wa Dhahabu

Wasilisha kisa chako upate fursa kushinda Tuzo ya Mbuyu wa Dhahabu: “Tuzo ya Mbuyu wa Dhahabu ilianzishwa mwaka 2008 kuwahamasisha waandishi wa ki-Afarika waliojikita katika vitabu vya watoto na vijana.”...

18 Septemba 2012