Habari kutoka Agosti, 2012
Nigeria: Rais wa Seneti Atakiwa Kuwataja Wafadhili wa Boko Haram
Makundi mawili ya vijana Kaskazini mwa Nigeria Jumatano yalimkosoa Rais wa Seneti, David Mark, kutokana na matamshi aliyotoa siku za karibuni akiwataka viongozi wa mikoa ya kaskazini kudhibiti shughuli za...
Brazil: Mtoto wa Miaka 13 Aonyesha Matatizo ya Shule Kupitia Facebook
Diário de Classe [pt], ukurasa wa Facebook uliofunguliwa na Isadora Faber, aliye na miaka 13 na anayetokea Santa Catarina, Brazil, tayari umeonyesha kupendwa zaidi ya mara 176,000. Huku lengo lake likiwa...
Tanzania/Malawi: Utafutaji Mafuta kwenye Ziwa Nyasa WachocheaMgogoro wa Umiliki
Taarifa kwamba Malawi inatafiti mafuta katika Ziwa Nyasa (linalojulilkana pia kama Ziwa Malawi) zimeibua mjadala motomoto. Wakati ambapo serikali ya Malawi inadai umiliki kamili wa ziwa hilo, Tanzania inataka mpaka utambuliwe kuwa katikati ya ziwa.
Serikali ya Kolumbia Yapanga Kufanya Mazungumzo na Waasi wa FARC
Katika blogu ya Crónicas, Santos García Zapata anaeleza muktadha [es] kuhusu uamuzi wa Rais wa kuanzisha mazungumzo ya amani na makundi ya waasi. Kongresi ya ‘Kamisheni ya Amani’ imetangaza kwamba...
Iran: ‘Marufuku Isiyo Rasmi ya Kutembea’ ya Tehran Wakati wa Mkutano wa NAM
Mkutano wa 16 wa Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote ulianza mnamo tarehe 26 Agosti, 2012 jijini Tehran huku kukiwa na ulinzi mkali. Umoja huo madhubuti (NAM) unaoundwa na nchi ni mabaki ya mvutano uliokuwepo enzi za Vita Baridi kati ya Mashariki na Magharibi, na umoja huu unachukuliwa na Iran pamoja na mataifa mengine kama jukwaa mbadala kwa ajili ya kuendesha mijadala kuhusu masuala mbalimbali yanaoukabili ulimwengu hivi sasa. Iran inasema inapanga mazungumzo kuhusu mpango wa amani ili kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, lakini hakuna uwakilishi kutoka upande wa waasi ulioalikwa kwa sababu Tehran ni rafiki wa karibu wa utawala wa Rais Bashar Assad wa Syria.
Mgogoro wa Umoja wa Ulaya: Kitabu cha Kwanza cha Global Voices cha Kieletroni
"Umoja wa Ulaya katika Mgogoro" (EU in Crisis) ni chapisho letu la kwanza katika Mradi wa Vitabu wa Global Voices na ambao unahusisha makala bora zaidi kuhusu mazungumzo ya kijamii, ushiriki na uhamasishaji unaopewa nguvu na raia wanaopitia nyakati ngumu za kubana matumizi katika bara la kale zaidi na kwingineko.
Mfumo wa Kipekee wa Kuwapa watoto Majina wa Nchini Myanmar (Burma).
Raia wengi wa Myanmar hawana majina ya ukoo. Je, umewahi kujiuliza wanajaza vipi fomu zinazowadai kujaza majina yao ya mwanzo na ya ukoo, au hata kujiuliza kuwa 'Daw' ina maana gani katika jina la Daw Aung San Suu Kyi? Hapa tutatazama mtindo wa pekee kabisa wa Mynmar wa kutoa majina.
Ufilipino: Mafuriko Yaathiri Vitongoji vya Jiji la Manila na Mikoa ya Karibu
Mvua kubwa ilisababisha mafuriko katika vitongoji vingi ya jiji la Manila pamoja na majimbo ya jirani katika Kisiwa cha Luzon nchini Ufilipino. Mhariri wa Global Voices aliye huko Manila, Mong Palatino, anakusanya picha kutoka katika majukwaa mbalimbali ya habari za kiraia yanayoonyesha athari kubwa ya mafuriko hayo katika mji huo mkuu wa nchi.
Mauritania: Wafanyakazi wa Migodini Wapinga ‘Aina Mpya ya Utumwa’
Zaidi ya wafanyakazi 2,300 wako kwenye mgomo nchini Mauritania katika mji wa kaskazini wa Zouerat, jambo ambalo limesababisha kuzorota kwa maeneo mengine kumi ya Kampuni la Taifa la Madini na Viwanda, huku kazi zikiwa kwenye mvurugiko mkubwa. Madai yamejikita katika suala zima la maslahi bora ya wafanyakazi.
Syria: Mafunzo ya Silaha na Namna ya Kupigana Katika Mtandao wa Intaneti
Waasi nchini Syria wameanza kutumia YouTube ili kupeana mafunzo hasa kupitia 'Free Syrian Army Help' yaani 'Msaada wa Jeshi la Kuikomboa Syria'. Chaneli hiyo ina picha za video zipatazo 80 zikiliezea mbinu kama vile vita ya uso-kwa-uso, jinsi ya kutengeneza mabomu ya kutupwa kwa mkono, na jinsi ya kuwavizia maadui.