Habari kutoka Juni, 2012
Umuhimu wa Kongamano La Sauti za Dunia (Global Voices Summit) hapa Nairobi
Kuanzia tarehe mbili mwezi wa Julai hadi tarehe nne mwezi huo huo, familia ya Sauti za Dunia (Global Voices, GV) pamoja na washiriki wao wa kimataifa, raia wapendao vyombo vya habari na watazamaji watakusanyika pamoja katika hoteli ya Pride-Inn mjini Nairobi kwa kongamano la GV. Bila shaka tukio hili ni la kusisimua na ambalo limekuwa likitarajiwa na wengi kwa shauku kuu.
Sudani: Kuondoa kizuizi cha Mapinduzi ya Sudani
Tofauti na nchi nyingine katika eneo lake, Sudani mara nyingi huwa haipati nafasi katika vyombo vikuu vya habari, na hili lilikuwa wazi zaidi wakati wa maandamano yalifanyika Ijumaa na Jumamosi. Sababu ni kwamba serikali ya Sudani imevibana mno vyombo vya ndani vya habari na kuwazuia waandishi kuripoti habari zinazohusu masuala ya haki za binadamu na ufisadi.
Sudani: “Polisi Yakanusha Kutumia Risasi; Majeruhi wote ni Wakufikirika
Maafisa wa serikali ya sudani wanarudia ‘uongo’ uliozoeleka ambao watawala wa ki-Arabu wamekuwa wakitumia tangu kuanza kwa yale yanayoitwa Mapinduzi ya Uarabuni yaliyoanza mwezi Desemba 2010. Imekuwa kawaida kusikia kauli kama, ‘waandamanaji wamedhibitiwa wakati wakiwashambulia polisi, ambao nao walijihami kwa kushambulia' Watumiaji wa mtandao wanaonyesha picha tofauti wakati tetesi zinadai mtandao wa intaneti utakatwa kufuatia kuongezeka kwa maandamano.
Sudani: Watumia Mtandao Wathibitisha Tetesi za Kukatwa kwa Intaneti
Raia wa kwenye mtandao wanaifuatilia kwa karibu Sudani, kufuatia tetesi kuwa serikali ya Sudani inadhamiria kuukata mtandao wa intaneti - hatua inayokumbushia jaribio la Misri kuwanyamazisha wanaharakati na kuthibiti mapinduzi ya Januari 25 pale ilipoondoa uwezekano wa watu kuwasiliana kwa mtandao wa intanenti mnamo Januari 27.
Kenya: Kilimo cha Bustani Mijini Chashika Kasi
Nchini Kenya, wakazi wa mjijini wanajifunza mbinu mbalimbali za kulima mazao ya chakula kwa ajili ya matumizi binafzi na kwa ajili ya kuuza katika maeneo madogo. kwa watu wenye kipato kidogo au wasio na kipato, ukulima wa mijini unaweza kuwa ndiyo ufumbuzi wa kujihakikishia uwepo wa chakula. Video hizi zinaonyesha jinsi ambavyo chakula kinaweza kuzalishwa katika makasha na vifaa vingine vya kubebea kwa kutumia maeneo na rasilimali kidogo.
Pakistani: Buriani Mehdi Hassan; Mfano wa kuigwa wa Ghazal.
Mehdi Hassan Khan ambaye maarufu alijulikana kama ‘Mfalme wa Ghazal’alifariki dunia Jumatano tarehe 13, Juni, 2012 baada ya kuugua kwa muda mrefu, katika hospitali jijini Karachi nchini Pakistan. wananchi wa Mtandaoni wanattoa salamu zao za mwisho.
India: Kipindi cha Runinga cha Aamir Khan Chaweka Wazi Masuala ya Kijamii
Kipindi kipya cha maongezi kwenye televisheni nchi India kinachoitwa Satyamev Jayate (Ni Ukweli tu Utakaoshinda) kinachoendeshwa na muigizaji na mtengeneza filamu wa Bollywood, Aamir Khan kinaleta na kujadili miiko na masuala moto moto ya kijamii ambayo yanawanasa na kuwavutia WaHaindi wengi zaidi na zaidi. Wananchi wa kwenye mtandao wanatoa maoni yao.
Ethiopia: Ardhi, Historia na Haki katika Eneo la Gambella
Wanaharakati wa masuala ya ardhi wanatumia hati ya malalamiko ya mtandao, mtandao wa facebook na twita kufanya kampeni dhidi ya unyang’anyi wa ardhi nchini Ethiopia. Inaarifiwa kwamba wanakijiji kwenye jimbo msikini zaidi nchini humo, Gambella, wanalazimishwa kuhamia kwenye vijiji vilivyobuniwa na serikali ili kuwapisha wanaoitwa 'wawekezaji' wakubwa.
Misri: Maandamano ya Kukomesha Udhalilishaji wa Kijinsia Yavamiwa
Maandamano kudai kukomeshwa kwa udhalilishaji wa kijinsia yaligeuka kuwa shubiri baada ya wanawake waliokuwa wanahusika nayo kuvamiwa na kundi la wanaume wenye hasira kwenye viwanja vya Tahrir leo(June 8, 2012). Watu walioshuhudia tukio hilo walielezea maoni yao kupitia twita.
Kenya: Intani walipwe au wasilipwe?
Mada hapa ni kuhusu kama inafaaa au haifai kwa intani kulipwa,mjadala ulioanzishwa na @RobertAlai.