Habari kutoka Mei, 2012
Afrika: Kusherehekea Siku ya Ukombozi wa Afrika kwenye Mtandao wa Twita
Siku ya Ukombozi wa Afrika ni maadhimisho ya kila mwaka kukumbuka tarehe 25 Mei 1963 siku ambayo Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) ulianzishwa. Mwaka 2002 OAU ilianzisha mrithi wake aitwaye AU. Waafrika na marafiki wa Afrika wanasherehekea siku hiyo kupitia mtandao wa twita.
Zambia: Maoni na Hisia Tofauti baada ya Mwakilishi Kutolewa kwenye Mashindano ya Big Brother
Kuondolewa kwa mwakilishi wa Zambia, mwanamuziki anayefahamika zaidi kwa jina la Mampi, kutoka katika mashindano yanayoendelea ya Big Brother Africa, kumepokelewa kwa hisia na maoni tofauti miongoni mwa watumiaji wa mtandao. Big Brother Africa: StarGame ni toleo la saba la mfululizo wa mashindano hayo maarufu zaidi barani Afrika yanayoonyesha moja kwa moja kupitia televisheni maisha ya washiriki.
Wanablogu wa Kenya: Je, ungependa kushiriki kwenye Mkutano wa Global Voices kuhusu Vyombo vya Habari vya Kiraia pasipo kulipia?
Mtandao wa Global Voices unawapa wanablogu sita (6) fursa ya kushiriki pasipo kulipia kwenye Mkutano wake unaohusu Vyombo vya Habari vya Kiraia utakaofanyika jijini Nairobi. Ili uweze kushinda moja ya nafasi hizo, andika makala ya walau maneno 500 au pungufu kidogo kuhusu mada hii: "Jinsi gani vyombo vya habari vya kiraia vinaweza kusaidia kufanya uchaguzi mkuu wa Kenya wa mwaka 2013 uwe wa amani".