Habari kutoka Machi, 2012
Zambia: Ban Ki-Moon atoa wito kwa taifa kuheshimu haki za mashoga
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliitembelea Zambia mnamo Februari 21; ambapo alilihutubia bunge, alikutana wanasiasa maarufu na kutembelea Maporoko ya Viktoria, hakuna katika haya yaliyogonga vichwa vya habari kama mwito wake wa taifa hili kuheshimu haki za mashoga.
Iran: Wanawake wapinga ‘Jinamizi la Vita’
Utawala wa Kiislamu wa Iran umepuuza Siku ya Wanawake Duniani kwa zaidi ya miongo mitatu. Utawala huo hauitambui siku ya Machi 8, na umepiga marufuku mashirika ya wanawake kusherehekea siku hiyo. Lakini kila mwaka wanawake wa ki-Iran iwe kwa uwazi ama kificho bado wanasherehekea siku yao hiyo.
Palestina: Gaza yashambuliwa, watu 12 wauwawa na wengine wengi kujeruhiwa
Usiku kucha wa tarehe 9 Machi na asubuhi ya Machi 10, ndege za kivita za Israel zilishambulia maeneo maalumu katika Ukanda wa Gaza, na kuua takribani watu 12 na kujeruhi wengine 20.
Iran: Wachora katuni ‘wamkalia kooni’ Khatami kwa kupiga kura
Mohammad Khatami, aliyekuwa Rais mwanamageuzi wa Irani, Ijumaa ya tarehe 2 Machi, 2012 alipiga kura katika uchaguzi wa wabunge. Kitendo hicho kilikinzana na kauli aliyopata kutoa siku za nyuma kwamba angegomea kupiga kura hadi wafungwa wote wa kisiasa waachiwe huru na katiba kuheshimiwa. Kitendo chake hicho kimezua shutuma nyingi kutoka kwa wanamageuzi walio makini katika kugomea uchaguzi huo.
Amerika Kusini: Waathirika wa ‘biashara’ ya kukuza matiti waingia mtandaoni
Wanawake wengi wameungana kwenye tovuti za kijamii kusema wanachofikiri na kubadilishana taarifa kuhusu matatizo yanayosababishwa na viini vya kukuzia matiti. Wakati huohuo wanapanga hatua gani za kisheria wachukue. Kumekuwa na ongezeko kubwa la ugonjwa wa saratani huko Amerika ya Kusini. Je, ni kina nani hawa wanaopaaza sauti zao barani humo? Fuatilia ...
Baada ya Kony 2012, “What I Love About Africa” Yanyakua Mazungumzo
Kampeni katika mtandao kuhusu mhalifu wa kivita Joseph Kony umesababisha utata mkubwa barani Afrika. Kampeni nyingine ya kupinga utata huo na kuonyesha upande bora wa bara la Afrika, unaojulikana kama #WhatILoveAboutAfrica (Nini Ninachopenda Kuhusu Afrika) sasa unaenea katika tovuti la Twitter.