Mei, 2011

Habari kutoka Mei, 2011

Singapore: Wanablogu Waikosoa Ilani ya PAP

  12 Mei 2011

Chama kinachotawala Singapore, People’s Action Party (PAP), kilitoa ilani yake ya uchaguzi tarehe 17 aprili, 2011, ambayo mara moja ilikosolewa na wanablogu wengi kwa “kutokuwa wazi”. PAP tayari kimekuwa madarakani kwa miongo mitano. Uchaguzi mkuu nchini humo umefanyika tarehe 7 Mei.

Nepal: Mwanzo wa Mapinduzi ya Facebook?

  10 Mei 2011

Pradeep Kumar Singh anaweka picha na habari za kampeni ya hivi karibu ni ya Facebook iliyopewa jina la “Jitokeze. Simama. Ongea. Vinginevyo, kaa kimya. Takriban vijana 400 wa Nepali walijitokeza...

Msumbiji: Polisi Washambulia Waandamanaji

Siku ya tarehe 6 Aprili, maofisa wa tawi la Polisi wa jamhuri ya msumbiji (PRM) – Kikosi cha Askari Maalum wa Dharura (FIR) – walitumia nguvukusitisha maandamano ya wafanyakazi wa shirika binafsi la ulinzi Group Four Security (G4S). Kwenye Facebook, wanamtandao walionesha kuchukizwa kwao kutokana na vitendo hivyo vya kikatili na kuhoji wajibu wa polisi, sheria na haki za binadamu.