Habari kutoka Novemba, 2010
Haiti: Kuokoa Maisha
“Idadi ya wagonjwa waliotibiwa katika siku 10 zilizopita ni 227″: matumaini ya kweli kwa haiti wanaeleza uzoefu wao wakati wanasaidia kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.
Myanmar: Hatimaye Suu Kyi Amekuwa Huru
Amekuwa kifungoni kwa miaka 15 katika miaka 21 iliyopita, lakini hivi sasa hatimaye yuko huru. Kiongozi wa upinzani na alama ya wapenda demokrasia nchini Burma, Aung San Suu Kyi aliachiwa huru kutoka kizuizini mchana siku ya Jumamosi na serikali inayoungwa mkono na jeshi la Myanmar
Ivory Coast: Wimbo Mpya Kwa Ajili Ya Uchaguzi wa Rais
Museke imeweka video ya wimbo mpya “Mpiga Kura” ulioandikwa maalum kwa ajili ya uchaguzi wa rais nchini Ivory coast. Wimbo huo unachezwa na Le Griot-Guére, Jackivoire, Soro Solo, na gitaa...
Mexico: Mwanamke wa Miaka 20 ni Mkuu Mpya wa Polisi katika Mji wa Kaskazini mwa Mexico
Valles García ni mwanamke aliyeolewa mwenye umri wa miaka 20 anayesoma masomo ya makosa ya jinai na uhalifu; vile vile ni mkuu mpya wa polisi wa Práxedis, Chihuahua, mji uliopo umbali wa kilometa 100 (maili 62) kutoka Ciudad Juárez, mji wenye uhalifu zaidi nchini Mexico.
Peru: Kampeni ya Kuzuia Kufungwa kwa Maktaba ya Amazon
Juan Arellano wa Globalizado [es] anaripoti juu ya kampeni ya kuzuia kufungwa kwa maktaba huko Iquitos, Peru , maktaba ambayo inatilia mkazo vitabu na masuala yanayohusu Amazon. Maktaba hiyo ni...
Watu wa Uruguay Waomboleza Kifo cha Mwanamuziki José Carbajal, ‘El Sabalero’
Mwimbaji na mtunzi José Carbajal, anayejulikana kwa jina la utani kama “el Sabalero,” amefariki kutokana na shambulio la moyo mnamo Oktoba 21 akiwa na umri wa miaka 66. Carbajal anachukuliwa kuwa gwiji na utambulisho wa utamaduni wa Uruguay. Mwaka huu alikuwa akifanya kazi na wasanii wengine katika mradi wa Kompyuta Moja ya Mapajani kwa Kila Mtoto nchini Uruguay Uruguay, Mpango wa Ceibal, ili kutumbuiza kwenye maonyesho kwa ajili ya watoto wa shule nchini kote.
Haiti: Video Inayookoa Maisha
Mganga nayeishi jijini Fransisco ambaye pia ni mwanablogu Dkt. Jan Gurley amezuru Haiti mara mbili tangu lilipotokea tememeko la ardhi la Januari 12 ili kuwahudumia watu kwa kujitolea. Ziara yake...