Habari kutoka Agosti, 2010
Cape Verde: Midahalo Kuhusu Vijana na Siasa Inayoendelea Huko Ureno
Kuna kundi la raia wa Cape Verde ambalo huandaa mikutano mjini Lisbon ili kujadili uhusiano kati ya vijana na siasa, kama anavyoeleza Suzano Costa katika video [pt] kama ilivyowekwa tena na...
Malaysia: Je, Uhuru wa Habari Unaelekea Wapi Sasa?
Picha uliyonayo ni kwamba Malaysia inaweza kuwa ni moja ya nchi zinazokua haraka kiuchumi katika bara la Asia, lakini je unafahamu kuwa ilikuwa katika nchi tatu za mwisho (nchi ya 131) kwenye masuala ya uhuru wa vyombo vya habari? Je wananchi na vyama vya upinzani vinavyopigana dhidi ya uchujwaji wa habari wanapata ahueni? Tutajua ukweli kwa kuangalia hali ya sasa ya uhuru wa vyombo vya habari nchini Malaysia.
Jamaica: Dansi!
Tallawah ametuma picha kutoka katika muhula wa 2010 wa Kikundi cha Taifa cha Dansi cha Jamaica.
China: Pato la Taifa Linaongezeka, Matumizi Katika Huduma za Jamii je?
Tunaendelea kusikia kuwa uchumi wa China unaendelea kukua; je matumizi ya huduma za jamii yameongezeka? Akiba binafsi zinabaki kwenye benki, anaandika mwanablogu mmoja: kutokea hospitali mpaka shuleni mpaka malipo ya uzeeni, China haiwezi kujilinganisha.
Moroko: Mtoto Mwanablogu Asalimia Ulimwengu
Salma alianza kublogu akiwa na umri wa miaka sita ili kuwasiliana na ndugu na marafiki. Chii ya usimamizi wa wazazi wake, mwanablogu huyu mdogo wa Moroko anapendelea kuandika hadithi fupi fupi na kuielezea dunia matukio anayokumbana nayo kila siku shuleni.
Afrika Kusini: Wanablogu Wajadili Hukumu ya Mkuu wa Zamani wa Jeshi la Polisi
Siku ya ijumaa tarehe 2 Julai 2010, aliyekuwa mkuu wa polisi na rais wa zamani wa Shirika la Kimataifa la Polisi (Interpol) Jack Selebi alihukumiwa kwa kosa la rushwa. Hukumu hiyo imezua mdahalo nchini na kadhalika imeacha maswali mengi yasiyo na majibu.
Korea Kusini: Maombolezo ya Kitaifa ya Mwanamwali wa Kivietnam
Mwanamwali mdogo wa Kivietnam aliuwawa na mumewe wa Kikorea nchini Korea. Wanablogu wa Korea wanatoa rambirambi zao kwa kifo kibaya cha mke huyo mwenye umri mdogo huku wakiitaka serikali kutokomeza eneo hili lisiloonekana kwa urahisi la haki za binaadamu, linalohusiana na wachumba kutoka nchi za kigeni.
Italia: HAPANA kwa Vikwazo Dhidi ya Uhuru wa Kujieleza wa Mtandaoni
Muswada mpya wa habari na Unasaji wa siri wa Mawasiliano ambao umewasilishwa kwenye bunge la Italia unaweza kuanzisha "hatari ya malipo ya fidia" kwa wanablogu wote na vyombo vya habari vya mtandaoni.
Udhibiti Nchini Singapore
Singapore imesababisha kelele kubwa baada ya kupiga marufuku filamu ya aliyewahi kuwa mfungwa wa kisiasa na kumkamata mtunzi Mwingereza wa kitabu kilichoandiaka kuhusu adhabu ya kifo nchini humo. Wanablogu wanajadili.