Habari kutoka Februari, 2009
Dunia Nzima: Lugha 2,500 Zinapotea
Ramani shirikishi ya lugha zinazopotea, inayoonyesha lugha 2,500 kati ya 6,000 ambazo ziko hatarini, imezinduliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO). Shirika hilo la kimataifa linawaomba watumiaji wachangie kwa kutuma maoni kwenye mradi huo ambao unawatia mashaka wanablogu wengi wenye nia ya kuhifadhi tamaduni.
Sudani: Maombolezo ya Mwandishi Maarufu wa Riwaya na Mahakama ya Kimataifa
Baada ya kimya kirefu, wanablogu wa Kisudani, wamerejea kwenye ulimwengu wa blogu kuongea, na kubadilishana mawazo kuhusu matukio ya hivi karibuni. Mawazo hayo yanayojumuishwa katika muhtasari huu ni pamoja na yale ya wanablogu tuliowazoea. Baada ya malalamiko kuhusu hali mbaya ya usalama wa afya kwenye Uwanja wa Ndege wa Khartoum, Msudani mwenye matumaini anaomboleza kifo cha mwandishi wa riwaya mashuhuri, Al- Tayeb Saleh.
India: Filamu ya Slumdog Millionaire Yanyakua Tuzo za Oscar
Filamu ya Danny Boyle, Slumdog Millionaire, iliyotokana na kitabu chenye maudhui ya India imefanya vyema katika sherehe za 81 za tuzo ya Academy. Wahusika wake kutoka Uingereza na India walitia...
Clinton Azuru Indonesia
Pamoja na kukutana na viongozi wa Indonesia, Katibu wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton alipata muda wa kutembelea makazi ya watu masikini mjini Jakarta. Kadhalika alitokea kwenye kipindi cha televisheni cha vijana. Ni nini maoni ya wanablogu?
Martinique: Uhuru na “Ubeberu” wa Kifaransa
Wakati harakati za wafanyakazi zinaendelea huko Martinique na Guadeloupe, wanablogu wa Martinique wanapima uhuru wa Idara za Ng'ambo utamaanisha nini. Le blog de [moi] anaona dhana ya kuwa Martinique haiwezi kujitegemea ni dhana inayotusi na ya kibeberu. Wasomaji wake wanadhani kuwa ukweli wa kisiwa chochote kidogo ni kuwa kila siku kitakuwa katika kivuli cha wengine.
Indonesia: Talaka na Ndoa za Mitala
Najihisi nina hatia ninapoandika kuhusu talaka na ndoa za mitala wakati wa siku ya wapendanao ya Valentino. Lakini mada hizi zisizotamkika ni ukweli wa mapenzi na mahusiano. Katika Indonesia, wanawake wengi wanawataliki waume zao kwa sababu ya mitala.
Paraguai: Wahamiaji Wasimulia Visa Vyao
Ni jambo la kawaida katika Marekani ya Latini kwa wahamiaji kuondoka na kwenda kwenye malisho ya kijani zaidi kwenye nchi jirani au nchi za mbali. Hakuna tofauti kwa Waparaguai, ambao huwaacha nyuma marafiki zao na familia ili kufuata fursa nyingine. Simulizi kadhaa za namna hiyo zinasimuliwa kwenye blogu inayoitwa Paraguayos (sisi ni Waparaguai), ambayo inawaalika wahamiaji walioko duniani kote kuwasilisha simulizi zinazohusu uzoefu wao.
Haiti: Fanmi Lavalas na Uchaguzi Ujao
Mwishoni mwa juma lililopita, ulimwengu wa wanablogu wa Kihaiti ulijaa habari za kutengwa kwa vyama vya siasa na Tume ya Muda ya Uchaguzi kwenye uchaguzi wa maseneta utakaofanyika mwezi Aprili 2009 , na siku ya tarehe 6 Januari, tume hiyo CEP ilichapisha orodha ya wagombea ubunge watakaokwaana kwenye uchaguzi ujao wa bunge nchini Haiti. Wanablogu wanaandika mawazo yao kuhusu wagombea walioachwa.
Ukraine: Umaarufu wa Yushchenko Unafifia
Kwa mujibu wa kura ya maoni iliyofanyika mwezi uliopita, Rais wa Ukraine Victor Yushchenko “angeshinda chini ya asilimia 2.9 ya kura kama uchaguzi wa rais ungefanyika mwishoni mwa mwezi Desemba 2008 au mwanzoni mwa mwezi wa Januari 2009.” Yafuatayo ni maoni yanayomhusu rais na wanasiasa wengine katika ulimwengu wa blogu za Ukraine.
Malawi: Homa Ya Uchaguzi na Kuelea Teknolojia ya Kidijitali
Juma lililopita lilikuwa lenye moto wa kisiasa kwa Wamalawi wengi kwani wameshuhudia wagombea wa viti vya urais na ubunge wakiwasilisha maombi yao kwenye Tume ya Uchaguzi kuelekea Uchaguzi utakaofanyika terehe 19 Mei. Hadi kufikia mwisho wa zoezi hilo wagombea wapatao 10 waliwasilisha maombi yao ya kugombea urais na mamia wengine kwa ajili ya kugombea viti 193 vya bunge.