- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kundi La Wadukuaji Wasiojulikana Laweka Wazi Takwimu za Siri za Serikali Kuhusu Maambukizi ya COVID-19 Nchini Nicaragua

Mada za Habari: Nicaragua, Censorship, Harakati za Mtandaoni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala, COVID-19, GV Utetezi
Picha na: Max Pixel [1], chini ya CC0 Public Domain [2] leseni.

Hapo Agosti 17, kundi la wadukuaji wasiojulikana [3] lilishambulia maktaba ya wizara ya Afya ya Nicaragua. Mafaili  400 yaliyowekwa wazi [4]yalionesha kwamba kuna ongezeko la visa 6,245 vya wagonjwa wa COVID-19 nchini Nicaragua ambavyo hapo awali havikuwa vinafahamika kwa umma. Tangazo hili [5]lilitolewa huko Twitter na mtu aliyejulikana kama Lorian Syrano, mwanachama wa kundi la wasiojulikana.

Wanicaragua waliopo Twitter walijibu kwa shauku kubwa udukuaji kwa hashitagi ya #OpNicaragua [6]. Tangu mwanzo wa janga  hili mamlaka za Nicaragua ziliamua kuficha [7]taarifa za  COVID-19 na pia  walikataa [8] kufungia watu ndani.

Mtu asiyejulikana alidhihirisha [9] kwamba  mpaka mwezi Mei  idadi ya watu waliopimwa na kukutwa na COVID-19 ilikuwa ni kwa asilimia  98.80 zaidi ya idadi ile maofisa wa Wizara wanatangaza: visa 1332 badala ya 16. Namna hiyo imeendelea kwa miezi iliyofuata. Mpaka Julai 24, ilionekana  kwamba jumla ya visa 6,245 vya maambukizi havikuripotiwa  kwa umma.

Pia imeonekana kwamba kasi ya ongezeko la idadi  ya maambukizi kwa kila kipimo ni  kubwa [10] sana duniani, ambapo karibu asilimia 56 [9] ya vipimo inarudi ikionesha wana maambukizi ya COVID-19. Mkurugenzi wa zamani wa Kitengo cha magonjwa ya mlipuko katika wizara ya afya Álvaro Ramírez, alifafanua wakati akihojiwa [11] na  Usiri kwamba ni kwa sababu vipimo vinafanyika kwa watu waliolazwa mahospitalini au wale wenye dalili za maambukizi.

Tayari kabla ya udukuaji huo, mashaka juu ya uhakika wa taarifa rasmi ya  takwimu za maambukizi ya COVID-19  yalikuwa yameongezeka.  Kwa mfano uchunguzi wa kujitolea ulifanywa na wataalamu wa afya, watafiti, wahandisi, wataalamu wa sayansi ya kompyuta na mawasiliano iliripotiwa [12]  kwamba idadi ya vifo vinavyohusishwa na COVID-19  ni mara ishirini zaidi  ya taarifa zilizotolewa [13] na Wizara  ya Afya.

Kwa mujibu wa Álvaro Ramírez, taarifa zilizovujishwa zinathibitisha kwamba serikali ilikuwa ikificha taarifa kwa makusudi.  Alisema [9]:

…el hecho de que esta información estaba ahí, que llegaba todos los días a la presidencia, y que por cualquier razón, que no la vamos a entender fácilmente, ellos (Daniel Ortega y Rosario Murillo) decidieron mentir a la población, y cambiar los datos, y poner datos diferentes.

… ukweli ni kwamba taarifa hizi zilikuwepo pale na zilikuwa zikiifikia ofisi ya Rais kila siku na kwa sababu yoyote ile ambayo hatutaielewa kirahisi, wao  (Daniel Ortega na Rosario Murillo) wameamua kuudanganya umma na kubadilisha takwimu na kuweka takwimu za uongo.

Serikali inayoongozwa  na Rais Daniel Ortega na mkewe na Makamu wa Rais Rosario Murillo, ilithibitisha hapo Mei kwamba watu walikuwa wakiugua  nimonia [14]badala ya  COVID-19. Mwezi Mei na Juni taarifa ya kutahadharisha kuhusu maziko ya siri yaliyokuwa yanafanyika  ilisambaa [15]. Mwanahabari Lucydalia Baca Castellón alitumaini [16] kwamba masharti ya mikopo ya Kimataifa ingeilazimisha serikali ya Nicaragua “kuchukua hatua za haraka na za uwazi” kuhusu janga la COVID-19.

Mnamo Agosti 16, Mtu asiyejulikana alifanya mzaha kuhusu taarifa zilizovujishwa:

Asiyejulikana, kama mpinzani wa serikali, wachambuzi [24] na vyombo [25] vya habari vya Nicaragua, vimekuwa vikiita serikali ya Ortega kama “serikali ya kidikteta” kwa sababu ya tabia za mabavu, [26]ufinywaji [27] wa haki na  rushwa. [28] Kulingana na taarifa ya kikundi  cha wataalamu kutoka kada mbalimbali Ortega amefanya uhalifu mwingi dhidi ya utu, [29] dhidi ya mahasimu wake wa kisiasa hasa wakati wa vuguvugu la kuipinga serikali hapo 2018.

Hapo  Agosti 21, Lorian Synaro [30] alishirikisha wavuti ambayo ilisema kwamba taarifa zote za wizara ya Afya ya Nicaragua na mafaili mengine 400 yanaweza kupakuliwa hapo:

Hii sio  mara ya kwanza kwa asiyefahamika huyo kuishambulia serikali ya Ortega. Katika mwaka wa 2018 wote wakati wa maandamano ya kuipinga serikali na unyanyasaji wa serikali, Asiyejulika huyo aliiangusha tovuti ya vyombo vya habari vya serikali [34] na ile ya  polisi. [35]April [36] 2020, Lorian Syrano aliilenga benki kuu ya Nicaragua, kituo cha runinga cha serikali, polisi na tovuti nyingine za  kitaasisi akipinga namna serikali inavyolishughulikia suala la  COVID-19. Serikali ya  Nicaragua ilinunua [37] vitumizi kwa ajili ya kuzilinda kompyuta vyenye thamani ya 916,000 (sawa na dola za Marekani 26,295).
 Mwezi Mei, Syrano aliendelea  [38] na kuangusha tovuti za wizara za serikali.

Chombo kikuu cha habari El 19 Digital, ambacho kina mahusiano ya karibu na serikali  hakijaripoti [45]  chochote kuhusu matukio haya pamoja na kuwepo kwa habari zinazohusiana [46]  na Wizara ya afya. Pia Wizara ya afya  nayo haikusema chochote kuhusu mashambulizi hayo.