- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

TAZAMA/SIKILIZA: “Kwenda zaidi ya Maandamano,” mazungumzo na Tanya Lokot

Mada za Habari: Ulaya Mashariki na Kati, Ukraine, Urusi, Haki za Binadamu, Maandamano, Mawazo, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, GV Insights

Kwenye kitabu chake kipya, “Beyond the Protest Square: Digital Media and Augmented Dissent [1],” msomi wa masuala ya habari Tanya Lokot [2] anajenga hoja kwamba, “ukweli unaokuzwa kuhusu maandamano unaenda mbele ya watu, mahema na mawe kwenye viwanja vya maandamano, ikijumuisha habari mubashara, zinazokwenda duniani kote bila kujali saa za maeneo mbalimbali, mazungumzo yanayofichwa yasidukuliwe, na tafsiri za papo kwa hapo za habari za maandamano kwenda kwenye lugha mbalimbali duniani.”

Mnamo Juni 17 mkurugenzi mtendaji wa Global Voices Ivan Sigal alikaa kitako na Tanya kwa mazungumzo kuhusu kitabu chake, ambacho kinazungumzia mahojiano yake na washiriki wa maandamano sambamba na uchambuzi wa kiethnografia (utafiti unamdai mtafiti kujifunza utamaduni wa anaowatafiti kwa muda mrefu) kwa maudhui yanayowekwa mtandaoni kutoka Ukraine na Urusi.

Tanya ni Profesa Mshiriki katika masuala ya Uandishi wa Kidijitali na Jamii kwenye Shule Kuu ya Uandishi wa Habari ya Chuo Kikuu cha Dublin City, na ni Mhariri wa habari za Ulaya Mashariki wa Global Voices.

globalvoices [3] · A conversation w/ media scholar Tanya Lokot About Her Book “Beyond The Protest Square” [4]