- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Wanawake wawili waliobadilisha jinsia nchini Kamerun wahukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa ‘kujaribu ushoga’

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Kameruni, Haki za Binadamu, Haki za Mashoga, Uandishi wa Habari za Kiraia

Kutoka kushoto: Njeukam Loic Midrel (Shakiro) na Mouthe Roland (Patricia). Picha https://www.facebook.com/permalink.php?story_fbid=201199005125091&id=106522774592715&__cft__[0]=AZXkLJww4FYhI_d8l4UZ6k8MEGHeo2BeAHlRJZpvraUyiGnR6Me9tFUWYDrFKBYRCDdXeVLwrqN7lPqn9r7nmeu9tvmPIlzfglRSxHa9Wmgq0pf_zVGcIS9STcmzhNqlkge_zRRUFaF8LucI6jr_0cfS&__tn__=%2CO%2CP-R

From left to right: Njeukam Loic Midrel (Shakiro) and Mouthe Roland (Patricia). Image credit: Shakiro/Facebook [1]

Mnamo Mei 11, watu wawili wa Kameruni waliobadili jinsia, Njeukam Loic Midrel (Shakiro) na mwenzake, Mouthe Roland (Patricia), walihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na faranga  200,000 za CFA (sawa na dola za kimarekani 370) kwa “kujaribu kuwa mashoga, kuvaa mavazi yasiyo na heshima na kukosa karatasi za utambulisho” inaripoti [2] BBC.

Shakiro, 23, na Patricia, 27, walikamatwa mnamo Februari 8 katika mgahawa huko Douala, mji mkuu wa kiuchumi Kamerun.

Kushindwa kulipa faini hiyo kunaleta adhabu ya nyongeza ya mwaka mmoja gerezani.

Shakiro na Alice Nkom wakiwa mahakamani. Picha imetumika bila idhini

Shakiro and Alice Nkom in court. Image used with permission.

Alice Nkom, wakili wa haki za binadamu na wakili kiongozi wa utetezi wa Shakiro na Patricia, aliandika andiko lililoonesha kukasirishwa kwake kwenye Facebook [6], mnamo Mei 12: “Ni sheria ipi inayowaadhibu waliobadili jinsia [wanawake] kwa kuvaa sketi kwa miaka mitano? Hakuna mtu anayepaswa kufungwa kwa tuhuma rahisi; hii inafungua mlango wa kufungwa bila uthibitisho?”

Nkom alisisitiza kuwa wateja wake hawana hatia kulingana na kanuni ya adhabu ya Kameruni, ambayo inakataza [6] “uhusiano wa kimapenzi kati ya watu wa jinsia moja, na ikiwa tu watashikwa katika kosa [katika kitendo cha kufanya makosa]”, kulingana na Kifungu cha Kanuni ya Adhabu ya 37 [7].

Mnamo mwaka wa 2016, Kamerun iliimarisha sheria kwa kuhalalisha ushoga katika kanuni ya adhabu. Moja ya mabadiliko ni pamoja na, kutunga sheria katika suala la upande wowote wa kijinsia. Kwa hivyo, inaweza kutumika kwa “mahusiano ya kimapenzi kati ya wanaume na kati ya wanawake”, kulingana na [8] asasi ya kiraia yenye makao yake Uingereza, Human Dignity Trust.

Jambo lingine la sheria ya 2016 ni kwamba polisi wanaweza kudhalilisha kihalali hadhi ya watu wa LGBTQ+ walioko chini ya ulinzi na “uchunguzi wa kulazimishwa wa mkundu” kwa “lengo la kupata ‘uthibitisho’ wa mwenendo wa ushoga”, inasisitiza [9] Human Rights Watch.

Adhabu iliyowekwa ni adhabu ya kifungo kuanzia miezi sita hadi miaka mitano pamoja na faini ya faranga 20 hadi 200,000 za CFA (40-400 Dola za kimarekani).

Nchini Kamerun, Korti za mwanzo zina mamlaka ya kiraia katika kesi ambapo mashtaka hayazidi faini ya faranga 500,000 za CFA (kama dola 1,000).

Richard Tamfu, wakili wa haki za binadamu na mshiriki wa timu ya utetezi ya Shakiro na Patricia, aliiambia Global Voices mnamo Mei 17 kwamba Shakiro na Patricia watakata rufaa kuhusu hukumu hiyo. Walakini, usikilizwaji unaweza kuchukua kati ya mwezi au mwaka, kulingana na jinsi taratibu za kukata rufaa zinavyopitia korti, kulingana na Tamfu.

Mshikamano wa kimataifa

Uamuzi huo umevutia lawama ya kimataifa kutoka kwa vikundi vya haki, huku mazungumzo yakifurika kwenye mitandao ya kijamii.

Minority Rights Africa ilifafanua uamuzi huo kama “ongezeko la kukomesha mashoga na wa watu waliobadili jinsia”:

Wanawake wa Kiafrika katika Mazungumzo walishiriki ombi mkondoni ili Shakiro na Patricia waachiliwe:

Mtumiaji huyu wa Twita anasisitiza kwamba “haki za LGBT = haki za binadamu”:

Ubalozi wa Merika nchini Kamerun ulitoa wito kwa serikali kuhakikisha kuwa watu binafsi wanafurahia haki zao za binadamu na uhuru wa kimsingi:

‘Najisikia vizuri kama mwanamke’ 

Njeukam Loic Midrel (Shakiro). Image credit: Shakiro/Facebook [22]

Kwenye video maarufu ya YouTube [23] ya mwaka jana – ambayo ilivutia maoni kama 26,000 – Shakiro anasema kwamba anajisikia “mzuri kama mwanamke.” Kama mtu mashuhuri wa mitandao ya kijamii, na mashabiki wapatao 5,000 wa Facebook [22], haishangazi kwamba kukamatwa kwake, miezi tisa baadaye, kumetengeneza vichwa vya habari.

Lakini umakini huu wa vyombo vya habari kwa kesi yake pia umeongeza vitisho kwa jamii ya LGBTQ + ya Kamerun

Kwenye mahojiano ya simu na Global Voices yaliyofanyika Mei 16, O.S. (jina halisi limeachwa kwa sababu za usalama), 25, alielezea wasiwasi wake juu ya usalama wake: “Tunakabiliwa na matusi, vurugu, na kunyimwa kutembea huru, na kufanya maisha kuwa magumu kwetu. Hatuna furaha kama hapo awali, tunajificha ”alisema.

“Mazingira ya chuki ni tishio kwa maisha yetu yanayotokana na athari baada ya kulaaniwa kwa Shakiro na Patricia. Hatujisikii kama watu wa kawaida, tunahitaji msaada kutoka nje ya nchi hii “, O.S. aliongeza.

Haikuwa mpaka alipoondoka Kameruni ndipo mtetezi maarufu wa haki za LGBTQ+ Bandi Kiki angeweza kuelezea waziwazi ujinsia wake [24].

Mnamo Februari 2021, BBC iliripoti [2] kuuawa kwa watu watatu wa LGBTQ+ na 27 kukamatwa huko Kamerun.

Ingawa kumekuwa swala la aibu kuzunguka familia za watu wa LGBTQ+, baba yake Shakiro, Nguekam, mtumishi wa serikali aliyestaafu, amekubali ujinsia wa mtoto wake na amekuwa akimuunga mkono.

“Mtoto wangu hastahili adhabu ya aina hii na hajafanya chochote kibaya kufungwa jela”, baba alisema katika mahojiano ya simu na Global Voices.