Shakiro, 23, na Patricia, 27, walikamatwa mnamo Februari 8 katika mgahawa huko Douala, mji mkuu wa kiuchumi Kamerun.
Popular Cameroonian crossdresser, Shakiro, one other sentenced to 5 years in prison for ‘attempted homosexuality’ https://t.co/JLLmvpt34z pic.twitter.com/ZG2DOEUEVx
— Linda Ikeji (@lindaikeji) May 12, 2021
“Mtambaji maarufu wa Kameruni, Shakiro, amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa ‘kujaribu kuwa shoga'”
Kushindwa kulipa faini hiyo kunaleta adhabu ya nyongeza ya mwaka mmoja gerezani.
Alice Nkom, wakili wa haki za binadamu na wakili kiongozi wa utetezi wa Shakiro na Patricia, aliandika andiko lililoonesha kukasirishwa kwake kwenye Facebook, mnamo Mei 12: “Ni sheria ipi inayowaadhibu waliobadili jinsia [wanawake] kwa kuvaa sketi kwa miaka mitano? Hakuna mtu anayepaswa kufungwa kwa tuhuma rahisi; hii inafungua mlango wa kufungwa bila uthibitisho?”
Nkom alisisitiza kuwa wateja wake hawana hatia kulingana na kanuni ya adhabu ya Kameruni, ambayo inakataza “uhusiano wa kimapenzi kati ya watu wa jinsia moja, na ikiwa tu watashikwa katika kosa [katika kitendo cha kufanya makosa]”, kulingana na Kifungu cha Kanuni ya Adhabu ya 37.
Mnamo mwaka wa 2016, Kamerun iliimarisha sheria kwa kuhalalisha ushoga katika kanuni ya adhabu. Moja ya mabadiliko ni pamoja na, kutunga sheria katika suala la upande wowote wa kijinsia. Kwa hivyo, inaweza kutumika kwa “mahusiano ya kimapenzi kati ya wanaume na kati ya wanawake”, kulingana na asasi ya kiraia yenye makao yake Uingereza, Human Dignity Trust.
Jambo lingine la sheria ya 2016 ni kwamba polisi wanaweza kudhalilisha kihalali hadhi ya watu wa LGBTQ+ walioko chini ya ulinzi na “uchunguzi wa kulazimishwa wa mkundu” kwa “lengo la kupata ‘uthibitisho’ wa mwenendo wa ushoga”, inasisitiza Human Rights Watch.
Adhabu iliyowekwa ni adhabu ya kifungo kuanzia miezi sita hadi miaka mitano pamoja na faini ya faranga 20 hadi 200,000 za CFA (40-400 Dola za kimarekani).
Nchini Kamerun, Korti za mwanzo zina mamlaka ya kiraia katika kesi ambapo mashtaka hayazidi faini ya faranga 500,000 za CFA (kama dola 1,000).
Richard Tamfu, wakili wa haki za binadamu na mshiriki wa timu ya utetezi ya Shakiro na Patricia, aliiambia Global Voices mnamo Mei 17 kwamba Shakiro na Patricia watakata rufaa kuhusu hukumu hiyo. Walakini, usikilizwaji unaweza kuchukua kati ya mwezi au mwaka, kulingana na jinsi taratibu za kukata rufaa zinavyopitia korti, kulingana na Tamfu.
Mshikamano wa kimataifa
Uamuzi huo umevutia lawama ya kimataifa kutoka kwa vikundi vya haki, huku mazungumzo yakifurika kwenye mitandao ya kijamii.
Minority Rights Africa ilifafanua uamuzi huo kama “ongezeko la kukomesha mashoga na wa watu waliobadili jinsia”:
Transgender women sentenced to prison for “attempted homosexuality.” 23-year-old Shakiro and 27-year-old Patricia have received a five year jail term in Doula, Cameroon, where there has been an increasing clampdown on gay and transgender people. pic.twitter.com/iqPfSnFO7L
— Minority Africa (@MinorityAfrica) May 20, 2021
“Wanawake waliobadili jinsia wamehukumiwa kifungo kwa “kujaribu ushoga.” Shakiro mwenye umri wa miaka 23 na Patricia mwenye umri wa miaka 27 wamepewa kifungo cha miaka mitano jela huko Doula, Kamerun, ambako kumekuwa na ongezeko la kukomesha mashoga na wa watu waliobadili jinsia.”
Wanawake wa Kiafrika katika Mazungumzo walishiriki ombi mkondoni ili Shakiro na Patricia waachiliwe:
Arrested for being Trans in Cameroon and facing a 5 year sentence.
Please sign the petition to get Shakiro and Patricia released! @AllOut https://t.co/rkU3E97oiE
— African Women in Dialogue (@AfWIDafrica) May 17, 2021
“Walikamatwa kwa kubadili jinsia nchini Kamerun na anakabiliwa na kifungo cha miaka 5.
Tafadhali saini ombi ili Shakiro na Patricia waachiliwe!”
Mtumiaji huyu wa Twita anasisitiza kwamba “haki za LGBT = haki za binadamu”:
#Cameroon#LGBT ??
“She was a transgender social media star. Now she faces 5 years in prison”, via @washingtonpost https://t.co/LI3Uoilqrv
Shakiro and her friend Patricia, 2 transgender women arrested in Feb in Douala, should be urgently released.
LGBT rights =human rights. pic.twitter.com/4Nhr0VtteZ— ilaria allegrozzi (@ilariallegro) May 17, 2021
“”Alikuwa nyota wa mitandao ya kijamii ya jinsia. Sasa anakabiliwa na miaka 5 jela”, kupitia @washingtonpost
Shakiro na rafiki yake Patricia, wanawake 2 waliobadilisha jinsia walikamatwa mnamo Feb huko Douala, wanapaswa kuachiliwa haraka.
Haki za LGBT = haki za binadamu”
Ubalozi wa Merika nchini Kamerun ulitoa wito kwa serikali kuhakikisha kuwa watu binafsi wanafurahia haki zao za binadamu na uhuru wa kimsingi:
We are concerned about the 5 year sentence for 2 transgender women and the increase in arrests of LGBTQI+ persons in Cameroon. It is essential that governments work to ensure all individuals can freely enjoy the human rights and fundamental freedoms to which they are entitled.
— U.S. Embassy Yaounde (@USEmbYaounde) May 14, 2021
“Tuna wasiwasi juu ya hukumu ya miaka 5 kwa wanawake 2 waliobadili jinsia na kuongezeka kwa kukamatwa kwa watu wa LGBTQI + nchini Kamerun. Ni muhimu kwamba serikali zifanye kazi ili kuhakikisha watu wote wanaweza kufurahia uhuru wa haki za binadamu na uhuru wa kimsingi ambao wanastahili.”
‘Najisikia vizuri kama mwanamke’
Kwenye video maarufu ya YouTube ya mwaka jana – ambayo ilivutia maoni kama 26,000 – Shakiro anasema kwamba anajisikia “mzuri kama mwanamke.” Kama mtu mashuhuri wa mitandao ya kijamii, na mashabiki wapatao 5,000 wa Facebook, haishangazi kwamba kukamatwa kwake, miezi tisa baadaye, kumetengeneza vichwa vya habari.
Lakini umakini huu wa vyombo vya habari kwa kesi yake pia umeongeza vitisho kwa jamii ya LGBTQ + ya Kamerun
Kwenye mahojiano ya simu na Global Voices yaliyofanyika Mei 16, O.S. (jina halisi limeachwa kwa sababu za usalama), 25, alielezea wasiwasi wake juu ya usalama wake: “Tunakabiliwa na matusi, vurugu, na kunyimwa kutembea huru, na kufanya maisha kuwa magumu kwetu. Hatuna furaha kama hapo awali, tunajificha ”alisema.
“Mazingira ya chuki ni tishio kwa maisha yetu yanayotokana na athari baada ya kulaaniwa kwa Shakiro na Patricia. Hatujisikii kama watu wa kawaida, tunahitaji msaada kutoka nje ya nchi hii “, O.S. aliongeza.
Haikuwa mpaka alipoondoka Kameruni ndipo mtetezi maarufu wa haki za LGBTQ+ Bandi Kiki angeweza kuelezea waziwazi ujinsia wake.
Mnamo Februari 2021, BBC iliripoti kuuawa kwa watu watatu wa LGBTQ+ na 27 kukamatwa huko Kamerun.
Ingawa kumekuwa swala la aibu kuzunguka familia za watu wa LGBTQ+, baba yake Shakiro, Nguekam, mtumishi wa serikali aliyestaafu, amekubali ujinsia wa mtoto wake na amekuwa akimuunga mkono.
“Mtoto wangu hastahili adhabu ya aina hii na hajafanya chochote kibaya kufungwa jela”, baba alisema katika mahojiano ya simu na Global Voices.