- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Netflix kuonyesha filamu ya kwanza ya Angola

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Afrika Kusini, Angola, Filamu, Habari Njema, Uandishi wa Habari za Kiraia

 

 

 

‘Tangazo la Netflix la sinema ya Santana, itakayoonyeshwa tarehe 28 Agosti. Screengrab. Nakala ya picha: “Nataka Dias Santana na kaka yake wakiwa wafe”’ [1]

Tangazo la Netflix [2] kwa ajili ya filamu ya Santana, itakayokwenda hewani mnamo Agosti 28. Picha imepigwa kwenye filamuManeno yanayoonekana yanasema: “Ninataka Dias Santana na kaka yake wauawe” 

Kuanzia Agosti 28, filamu iliyozalishwa Angola itaonekana kwa mara ya kwanza katika orodha ya Netflix. Ni filamu “Dias Santana”, iliyotengenezwa kwa ushirikiano na Afrika Kusini.

Filamu “Santana”, imetarishwa kwa pamoja kati ya Angola na Afrika Kusini, na Maradona Diad dos Santos na Chris Roland, ambayo ilionyeshwa katika sinema mnamo 2015 kwa jina la “Dias Santana”, itapatikana kwenye Netflix mnamo Agosti 28.

Filamu iliyoonyweshwa kwenye tamasha la filamu la Cannes mwaka 2015, inaelezea stori ya ndugu wawili, Jenerali na Afisa wa polisi, waliogundua utambulisho wa mtu aliyewaua wazazi wao, mauaji yaliyotokea miongo kadhaa iliyopita.

Kulingana na chombo cha habari Observador [7], filamu hiyo iliandaliwa na Giant Sables Media ya Angola na Zen HQ Films ya Afrika Kusini.

Mtayarishaji wa filamu wa Angola, Jeremias Didalewa, alituma ujumbe [8] wa shukrani kwenye wasifu wake wa Instagram kwa kufanikiwa kufunga mpango huo na jukwaa:

Malta, amigos e compatriotas. Conseguimos fechar o deal com a Netflix. Teremos o filme “DIAS SANTANA” primeiro filme Angolano na Netflix.

Um filme, com uma produção Angolana 80%/Sul Africana 20%. História de uma família Angolana, que começa em Angola e termina na África do Sul. Com vários actores nacionais e internacionais.

Jamaa, Marafiki na wenzetu. Tuliweza kufunga mpango na Netflix. Tutakua a filamu “DIAS SANTANA” filamu ya Angola kwenye Netflix.

Filamu, imetayarishwa kwa ushirikiano wa asilimia 80 kutoka Angola na asilimia 20 ya Afrika Kusini. Ni simulizi la familia linaloanzia Angola na kuishia Afrika Kusini. Imejumuisha waigizaji kadhaa wa kitaifa na kimataifa.

Onyesho la filamu ya Angola linakuja mwezi mmoja baada ya filamu ya kwanza [9] ya Msumbiji pia kuonekana kwenye orodha ya Netflix.