- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

MUBASHARA mnamo Mei 20: Tunachojifunza kuhusu Ulaya kupitia Shindano ya Eurovision

Mada za Habari: Ulaya Magharibi, Ulaya Mashariki na Kati, Mahusiano ya Kimataifa, Muziki, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Matangazo, GV Insights

Kwa wengi barani Ulaya na kwingineko, Shindano la Uimbaji la Eurovision [1] linafuatiliwa sana kila mwaka, na mashabiki wake hukusanyika kwa makundi kulitazama shindano hilo. Kwa wengine, ni shindano linaloboa, lisiloisha, kwa zaidi ya miaka 65, zimekaa muda mrefu na kuchosha.

Lakini ulipende au usilipende, hakuna mashaka kwamba shindano la Eurovision—na mwitikio linalousababisha—linatoa mtazamo mzuri kuhusu Ulaya ya sasa, siasa [2] zake,  taswira  [3]yake na tunu zake.

Ungana nasi Mei 20 saa 11mchana GMT [4] kwa kipindi chetu cha Global Voices Insights [5], mfululizo wa mazungumzo, ambako Mhariri Mtendaji wa Global Voices Filip Noubel [6] atakaa na Mhariri wa habari za Ulaya Mashariki Tanya Lokot [7] na mhariri wa Ulaya ya Kati Filip Stojanovski [8] kwa mazungumzo kuhusu shindano hilo la Eurovision kama suala la kiutamaduni na kisiasa.

Kipindi hiki pia kitaonesha mahojiano na washirikisha wawili wa shindano hilo ambao walitikisa pia kwenye maonesho ya  Rotterdam mnamo Mei 22. Washiriki hao ni Benny Cristo [9], anayeiwakilisha Jamhuri ya Czech [10], na Vasil [11], anayeiwakilisha Macedonia Kaskazini [12].

Kipindi hiki ni bure na kiko wazi kwa mtu yeyote, na kitarushwa mubashara kwenye mitandao ya Facebook [13], YouTube [14] na Twitch [15]

Tunatarajia utaungana nasi siku hiyo (bofya kiungo hiki [4] kufahamu muda halisi kwa saa za nchini kwako)!