Nani ana nguvu ya kuamua kitu gani kionekani na kipi kisionekane kwenye mtandao? Katika mazingira ambayo uwanja wetu huru unaendelea kuwa jukwaa binafsi la mtu, nani humchungua mchunguzi?
Kwenye mazungumzo [1] haya na mkurugenzi mtendaji wa Global Voices Ivan Sigal [2] ulioruka mubashara mnamo Februari 10, 2021, mwandishi na mwanaharakati Jillian C. York [3] anajadili swali hilo hapo juu, pamoja na mengine mengi ya muhimu alipozungumzia kitabu chake kijacho, “Silicon Values: The Future of Free Speech Under Surveillance Capitalism,” kitakachoingia sokoni mnamo Machi 23, 2021.
Agiza nakala yako ya “Silicon Values” kupitia kiungo hiki [4] na saidia kuunga mkono kazi zinazofanywa na Global Voices!