MUBASHARA mnamo Februari 10: Mazungumzo na Jillian C. York kuhusu kitabu chake kijacho “Silicon Values”

Nani ana nguvu ya kuamua kitu gani kionekani na kipi kisionekane kwenye mtandao?” Hili ndilo swali muhimu linaloulizwa na mwanaharakati na mwandishi Jillian C. York kwenye kitabu chake kijacho “Silicon Values,”* kinachotarajiwa kuzinduliwa mnamo Machi 23, 2021.

Mnamo Jumatano, Februari 10 saa 2:00mchana GMT, Jillian ataungana na mkurugenzi mtendaji wa Global Voices Ivan Sigal kwa mazungumzo mubashara ya video kuhusu kitabu chake, ambacho, kama anavyoeleza kwenye dibaji, “tunatafuta kuchimbua historia ya namna majukwaa makubwa ya mawasiliano ya Silicon Valley yalivyotengeneza mfumo wake wa kipekee—hususani, mfumo ambao unatawala namna tunavyoweza kujieleza mtandaoni.”

Jillian, ambaye ni Mkurugenzi wa Uhuru wa Kujieleza wa Kimataifa katika shirika la Electronic Frontier Foundation, na ni mwanachama maarufu wa siku nyingi wa Global Voices, ambako anapambana kuandika kuhusu uhuru wa kidijitali na uhuru wa kujieleza katika mukhtadha wa Mashariki ya Kati.

Kipindi hiki ni bure na wazi kwa umma na kitaruka moja kwa moja kwenye mtandao wa  Facebook Live, YouTube, na Twitch.

Tunasuburi kwa hamu kukuona ukiungana nasi Jumatani, Februari 10 saa 2:00mchana GMT (bofya hapa kuangalia muda unaoendana na eneo ulipo)!

*Kununua kitabu hiki kupitia kiungo hiki kutasaidia kuichangia Global Voices.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.