Global Voices imetimiza miaka 15!

Desemba 2004. Ilikuwa lazima uwe mwanafunzi wa chuo kikuu kutumia mtandao wa Facebook, Twitter ilikuwa bado haijaanza kutumika, wachokozi bado walikuwa wanaishi kwenye madaraja ya masimulizi ya kusadikika. Simu zetu bado hazikuwa na akili, kuvuja wakati huo ilimaanisha maji na ungemwita fundibomba kurekebisha, na bado Amazon.com hawakuwa na uwezo wa kuuza baadhi ya bidhaa. Kulikuwa na tovuti nyingi za habari, blogu zilikuwepo na zilifanya vizuri, na tulishaanza kuzungumza mtandaoni. Hapo ndipo Global Voices ikazaliwa.

Tumekuwepo kwa miaka 15! Kwa umri wa mbwa, hiyo ni miaka 110. Kwa miaka ya intaneti, hiyo ni sawa miaka 1000.

Leo tunatamani kutumia fursa hii kuwashukuru waandishi wetu mahiri waliosambaa duniani kote na wasomaji wetu waaminifu na washirika wetu kwa kuipa Global Voices nguvu na uwezo wa kuendelea kusonga mbele. Tangu 2004, tumesaidia kuandika habari kubwa duniani. Tumechapisha karibu makala 100,000, na kutengeneza makala maalum zilizolenga kuziwezesha jamii za maeneo yasiyopewa kipaumbele kutumia mitandao ya kidijitali na kupigania haki za mtandaoni, ikiwa ni pamoja na kujenga jumuiya ya watafsiri wanaotafsiri zaidi ya lugha 51. Bila wewe, pasingekuwepo Global Voices.

Tusaidie kukamilisha miaka 15 mingine. Tunamaanisha kabisa—tunahitaji msaada wako. Michango kutoka kwa watu binafsi inatusaidia kulinda uhuru wetu na kutuwezesha kufanya maamuzi magumu kukua na kubadilika. Tafadhali tuunge mkono leo!

Changia sasa!

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.