Televisheni ya taifa nchini China yapotosha matamshi ya mwanasayansi wa Shirika la Afrika Duniani (WHO) kwenye video inayosambaa sana
Hotuba halisi ya Dkt.Swaminathan umehaririwa
Oiwan Lam Hanningtone OmolloAfya
Habari hii imetumia utafiti wa Factcheck Lab, wakala wa uhakiki wa ukweli ulioko Hong Kong,ambaye pia ni mshirika wa habari wa Global Voices ambapo mwandishi ni mwanachama.
Tokea Septemba 22, taarifa za habari na machapisho ya mtandao ya kijamii inayoenea katika mitandao ya Kichina ilinukuu sivyo kuwa mwanasayansi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (SAD), Dkt. Soumya Swaminathan, alisema chanjo za Uchina dhidi ya COVID-19 “zimethibitishwa kuwa na athari.”
Hizi ripoti na machapisho zinanukuu chanzo video ya dakika inayotayarishwa na televisheni ya China kwa programu-tumizi ya kushiriki video China Miaopai. Huo video inaonyesha hotuba ya mkurugenzi mkuu wa SAD Tedros Adhanom Ghebreyesus akiongelea umuhimu wa kukuza chanjo ya UVIKO-19,ikifuatiliwa na matamshi ya Dkt. Swaminathan.
Katika video ya CCTV, ambayo maelezo yake mafupi yanasema “Mwanasayansi mkuu wa WHO: Chanjo za China za UVIKO-19 zimehakiki kuwa na athari” (世卫组织首席科学家:中国的新冠疫苗已被证明有效), huu ni taarifa ya Swaminathan:
Kama mnavyofahamu,pia wanayo programu amilifu ya kukuza chanjo na baadhi ya chanjo yako hatua mbele katika majaribio ya kliniki, huu pia ni maslahi kwetu, tunaifuatilia kwa karibu. Wengineo wa washirika wamethibitisha kufaidika kutokana na majaribio la kliniki yanayoendelea..
Lakini, hotuba asili ya Dkt. Swaminathan umehaririwa.Sentensi yake ya mwisho, kwa uhakika, ulianza na neno “ikiwa,” na mziki wa mandharinyuma ulifanya utoke kana kwamba anasema “ulithibitisha” badala ya “thibitisha.”
Matamshi ya Dkt. Swaminathan kamili ni haya yafuatayo :
Tumehusika na mjadala na Uchina kwa miezi mingi iliyopita kwa sababu,mnavyojua, hao pia wanao programu amilifu ya kukuza chanjo na na chanjo zao mingi ziko hatua mbele ya majaribio ya kliniki, huu ni maslahi kwetu,kwa hivyo tunafuatilia kwa karibu. Tumekuwa na mjadala wa kujenga na wazi nao na kila mara wamesisitiza kujitolea kwao kwa ufikavu kote duniani ikiwa baadhi ya chanjo zao zimepita majaribio ya kliniki yanayoendelea [msisitizo umeongezwa]. Kwa hivyo nafikiria mazungumuzo yanayoendelea, bado ni wazi na tunatumania nchi mingi watajuinga.
Haya matamshi yalitolewa katika mkutano wa wandishi si bayana ya SAD iliyofanyika mnamo Septemba 21. Nakala kamili ya tukio hiyo ya saa moja na nusu yanaweza patikana hapahere.
Hiyo kongamano ilinuia kuwasilisha sasisho kuhusu mpango uliogharimu dola bilioni 18 ya merikani ya WHO na mashirika mengine kupeleka chanjo cha UVIKO-19 hapo mbeleni kote duniani. Kufikia sasa, mataifa 156 wamejisajili katika mpango huu; si Uchina wala Amerika ni miongoni mwao.
Kama ilivyokadiriwa, video ya CCTVT,pamoja na ripoti ya habari na machapisho zinazozalishwa, zimevutia ridhaa za kizalendo. Chapisho katika Weibo na Daily Economic News imependwa na watu zaidi ya 337,000. Chini hapa ni baadhi ya maoni maarufu:
Najivunia sana nchi yangu. Hii ndio zawadi ya Siku ya Kitaifa na Tamasha la Katikati ya Vuli.
Huwezi dhania ukasi wa Uchina. Navunia nchi yangu.
China imeokoa dunia.
Baada ya wakaguzi hakika huashiria maneno ya Dkt. zimepotoshwa, baadh ya vyombo vya habari,ikiwa pamoja na CGTN na CCTV, walifutilia machapisho yao ya mtandao wa kijamii. Miongoni mwao ni Ligi ya Kikomunisti ya Vijana ya China, ambao chapisho lao ilinikuliwa na mtumiaji wa mtandao wa twita @Emi2020JP kabla kupotea toka Weibo:
Tedros anafaa kuchanjwa kwanza.
Kama @Emi2020JP, wengi wa watumiza wa mtandao wa twita waliamini WHO was assisting China with distorting the video, na kuchapisha maoni ya hasikwa kwake Tedros:
Tedros ni kisugulio ya choo!
Nitalipa kumpatia Tedros sindano ya ziada!
Jana mama yangu aliniambia, habari ya humu nchini ilisema Amerika itanunua chanjo mingi toka Uchina. Sina haja kuelezea.Wacha waishi katika fantasia yao .
Kazi mzuri sana, kuanzia kusitiri ueneaji wa virusi mpaka matangazo ya mauzo ya chanjo!
Ingawa machapisho kwa uchina yamefutiliwa,nakala za kuiga bado yanasambaa katika mitandao ya kijamii, kama this public post WeChat.
Vyombo vya habari yanayoegemea Beijing huko Hong Kong, kama Speak Out HK (港人講地)and Today Review (今日正言), pia yamechapisha habari kutokana na hio video.
Kuna chanjo takriban 200 za UVIKO-19 yalioko katika hatua mbali mbali ya majaribio ya kliniki ulimwenguni, na mengi miongini mwao yameandaliwa na maktaba za Uchina. Hakuna ambayo imepita awamu ya 3 ya majaribio kwa sasa.