Umoja wa Afrika wageukia teknolojia ya uangalizi wa kibiolojia kukabiliana na COVID-19

Wasafiri wakivuka mpaka kati ya Ghana na Togo, Afrika Magharibi, mnamo Januari 25, 2016. Picha ya Enock4seth kupitia Wikimedia Commons, CC BY-SA 4.0.

Viongozi wa Afrika wamechukua uamuzi wa haraka kukabiliana na UVIKO-19.  Kituo cha Afrika cha Kudhibiti Magonjwa (ACDC) kiliunda kikosi kazi ya UVIKO-19 Februari 5 , kabla ya bara hili halijashuhudia hata mgonjwa mmoja. 

Leo hii, Afrika ambalo kwa sasa ndilo eneo lililoathirika kidogo sana duniani likiwa na wangonjwa wapato 1,293,048 waliothibitishwa wenye UVIKO-19 na kinachovutia zaidi ni wagonjwa 1,031,905 wakiripoti kupona, kwa mujibu wa Afrika CDCP. Bara hili lina chini ya asilimia 5 ya wagonjwa walioripotiwa duniani kote na chini ya asilimia 1 ya vifo vyote vilivyotokea duniani kote. 

Sasa, kama nchi za Kiafrika — ikiongozwa na Umoja wa Afrika —  wanalegeza vikwazo za COVID-19 na kujiandaa kufungua tena uchumi na mipaka yao, serikali nyingi wanatumia teknolojia bunifu.

Utaji wa umoja, wa teknolojia ya Kiafrika inayoweza fuatilia usambaa na kukutanisha vituo ya kupima COVID-19 kote bara umepelekea utumizi wa PanaBIOS, teknolojia wa uangalizi wa kibiolojia unaoungwa mkono na Umoja wa Afrika. 

PanaBIOS umetoa programu inayotegema rununu na wavuti na kutumia algorithimu kufuata watu walio hatarini kiafya na kuweka rekodi ya vipimo vya sampuli toka asili hadi maabara.. 

Huu teknolojia umeundwa na Koldchain, taasisi chipukizi ya Kenya, na kufadhiliwa na AfroChampions, ushirikiano wa umma na binafsi uliobuniwa kuleta pamoja rasilimali ya Afrika na taasisi kusaidia ubuzi na mafanikio ya sekta binafsi Afrika. 

Ghana ndio nchi pekee kwa saa hii inayotumia teknolojia ya PanaBIOS wakati inafungua mipaka yake. PanaBIOS kuhakikisha wasafiri wanaweza tumia matokeo ya vipimo toka nchi nyingine kuridhisha mahitaji ya idhini ya bandari kwa nchi wanayosafiria kupitia programu-tumizi ya PanaBios au kwa kuongezea nywila unaozalishwa na mfumo kwa hati za usafiri. 

Maafisa wa afya bandarini wanatumia programu-tumizi toleo la biashara kudhibitisha hati za afya kwa namna sawa kwa nchi zote.

Sheria kamili za kulinda data na ufaragha

Muungano wa Afrika na Afrika CDCP wanahimiza mataifa wanachama kushirikisha jukwaa wenye msingi wa rununu, PanaBIOS utakao wezesha matokeo kote barani kuwekwa pamoja. Lakini,tarakimu kuingilia kati afya kumezua maswali mengi kuhusu ufikavu na ufaragha wa data.

Ufuatiliaji unaoendeshwa na serikali na udhibati unaweza nuiza hofu na kutishia huru uraia, hasa katika bara ambapo nchi 27 tu kati ya 54 wanayo sheria kamilifu ya ulinzi na ufaragha wa data.

Nchi nyingine Afrika, kama Ghana yamebadili sheria kuipa rais mamlaka ya dharura kukabiliana na janga kwa kuamrisha kampuni ya mawasiliano ya simu kuipa maelezo ya kibinafsi ya wateja kama vile hifadhidata ya mteja, kumbukumbu ya simu ya mteja, data ya pesa uliohamishwa kutumia simu na haujatumika, misimbo ya wafanyabiashara wa miamala , na anwani. 

Kuhakiki ulinzi na ufaragha wa data, mbinu zote za masomo ya mashine inayotumiwa na PanaBIOS ziko katika data ya jumla. Hio ni — data iliokusanywa inahaririwa kwa ajili ya uchambuzi wa takwimu — sio data binafsi ya kulenga watu — isipokua kwa ajili ya kufuatilia mwasiliwa, ambapo itatakikana kufikia washukiwa ama waathiriwa. 

Kuhakikisha uzuizi wa kuingilia ufaragha, Muungano wa Afrika, PanBIOS, na washirika wake lazima wapendekeze namna watakavyo zingatia sheria za ulinzi wa data za nchi tofauti tofauti kulinda ufaragha,hakikisha idhini ya data na kuepuka kushiriki data kibiashara.

Kwa sasa, huu pragramu-tumizi hauna sera ya faragha inayopatikana kwa umma, ambapo inaelezea watumiaji kanuni za kukusanya na kushiriki data. 

Changamoto ni jinsi huo sera faragha utatimiza malengo mbalimbali, kibara, kitaifa, na kikanda ya sheria za kulinda data kama vile ya Muungano wa Afrika Mkataba juu ya Usalama wa Mtandao na Ulinzi wa Takwimu za Kibinafsi,ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) sheria kielezo juu ya ulinzi wa data, Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi
(ECOWAS)
Sheria ya nyongeza A / SA.1 / 01/10 juu ya Ulinzi wa Takwimu Binafsi Ndani ya ECOWAS na Jumuiya ya Afrika Mashariki Kiunzi cha Kanuni za mtandao

Suluhu za kiteknolojia zimechangia ufanisi kukabiliana na COVID-19 Afrika 

Pamoja na PanaBIOS, baadhi ya mataifa ya Afika wameamilisha itikio inayoegemea teknolojia kupambana na uenevu wa janga la COVID-19. 

Kwa mfano, wanasayansi toka Sengali wametengeneza kifaa cha kupima COVID-19 inayogharimu $1 na Vipumuaji vya 3D ya wagonjwa. Wellvis, taasisi chipukizi ya Nijeria, walibuni chombo cha kupima COVID-19 , chombo huru ya mtandao kusaidia watumizi kujipima kiwango cha hatari ya kuambukizwa virusi vya korona kulingana na dalili na historia ya kuwemo hatarini..

Serikali ya Afrika Kusini ilitumia mtandao wa ujumbe mfupi Whatsapp kutoa mazungumuzo ya mwingiliano kujibu maswali ya kawaida kuhusu hadithi za uongo, dalili na tiba ya COVID-19. Na Uganda, wanawake wa soko walitumia programu-tumizi ya Soko Bustani kuuza bidhaa yao wakiwa nyumbani kutumia hii programu, kisha teksi ya pikipiki kumchukulia mnunuzi bidhaa.

Afrika kufanikiwa kudhibiti na kusimamia uenevu wa COVID-19 umehusishwa na umma changa, uwezo kadiri wa kupima na kufuatilia waliofariki, na uwezekano wa kuwepo na kingamwili za SARS-CoV-2 miongoni Waafrika wengine . 

Lakini, ni bayana kwamba uvumbuzi zinazoegemea teknolojia zimechangia pakubwa kufanikisha uthibati wa COVID-19, pamoja na uongozi amuzi mwanzoni mwa janga. 

Solomon Zewdu, naibu daktari na shirika la Bill na Melinda alifupisha jinsi, mnamo Januari, wakati mataifa mengi ya magharibi yakisita , Ethiopia ilianza kichujio kabambe uwanja wa ngege wa AddisAbaba. Rwanda ikawa nchi ya kwanza Afrika kusitisha katikhuli za kawaida mnamo Machi 21,na nchi kadhaa Afrika kufuatilia hivo karibuni: Afrika kusini ikatekeleza sitisho katikhuli za kawaida kabambe wakati ilikua na kesi 400 na vifo mbili. (Na idadi hicho ya umma, Italia ilikua na zaidi ya kesi 9,000 na vifo 400 ilipochukua hatua.)

Kwa kulinganisha kinyume,idadi ya walioathiriwa na kufa Amerikani ni mara sita idadi ya Afrika. Wataalam wa afya ya umma walikadiria kwamba janga lingeathiri pakubwa bara la Afrika na miili ya walokufa kutanda mitaa . 

Bayana, Afrika imethibitisha vinginevyo. 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.