Mnigeria Abubakar Idris Dadiyata Bado Hajapatikana, Ni Mwaka Mmoja Sasa Baada Ya Kutekwa

Picha ya Abubakar Idris Dadiyata, imetumika kwa ruhusa kutoka kwa The SignalNg.

Abubakar Idris Dadiyata, mhadhiri na mkosoaji mashuhuri wa serikali ya Nigeria alitekwa nyumbani kwake mnamo mwezi Agosti 1, 2019, huko Barnawa jirani na Kaduna, Kaskazini Magharibi mwa  Nigeria.

Mwaka mmoja baada ya kutekwa kwake bado Dadiyata hajapatikana.

Dadiyata alikuwa mkufunzi katika chuo Kikuu cha Umma cha Dutsinma, katika Jimbo la Katsina. Kama mwanachama wa chama cha upinzani cha Watu na Demokrasia (People's Democratic Party) mara zote Dadiyata alikwaruzana na wanachama wa Chama tawala cha Maendeleo Kwa Watu Wote (All Progressive Congress party) katika mitandao ya jamii.

‘Taasisi zote za serikali ya jimbo na serikali kuu hazijishugulishi na chochote’

Dadiyata alichukuliwa kwa nguvu na watekaji mnamo saa 7 usiku alipowasili nyumbani kwake, mwaka mmoja uliopita siku ya tarehe 1, Agosti 2019, iliripoti Premium Times.

Mke wa Dadiyata, Kadija katika mahojiano na shirikika la habari la BBC alikumbuka kwamba mumewe alikuwa “anaongea na simu huku injini ya gari yake ikiwa inaunguruma bado,” alipokamatwa na watekaji hao. Ingawa Kadija hakuweza kusikia “kilichokuwa kinazungumzwa au ni nani alikuwa anaongea naye kwenye simu,” anakumbuka watekaji wa mume wake “walikuwa wanamfuatilia na walikuja hadi nyumbani.” Mke wa Dadiyata alibaki kuchungulia dirishani chumbani kwao wakati mumewe akichukuliwa na kuondoka watekaji hao.

Mbaya zaidi, ni kwamba hamna taarifa kuhusu alipo Dadiyata. “Inaumiza,” sana jinsi watoto wao wanavyoendelea kumuulizia baba yao aliyepotea, Kadija aliiambia BBC.

Kuliko kumtafuta Dadiyata, taasisi za ulinzi za Nigeria zimeendelea kujitoa kwenye lawama za aina yoyote zinazohusiana na kupotea kwake.

Idara ya Ulinzi wa Taifa la Naijeria, mpaka Januari iliendelea kukataa kumweka Dadiyata kizuizini. Idara ya Ulinzi wa Taifa inasema kwamba kwa kuwa Dadiyata “alichukuliwa nyumbani kwake na watu wenye silaha haimaanishi kwamba watu hao ni wafanyakazi wa Idara ya Usalama wa Taifa.”

Vilevile mwanasheria mkuu wa Jimbo la Kaduna, Aisha Dikko, alikataa kufahamu “alipo” au kuhusika na “lolote” katika utekaji wa Dadiyata. “Kwa vyovyote ni kinyume na ni mtazamo finyu kutaka kuamini kwamba kwa kuwa alitekwa akiwa katika jimbo la Kaduna basi serikali ya jimbo inahusika,” alisema Dikko.

Hata hivyo, kukana kuhusika kwa Usalama wa Taifa na serikali ya jimbo la Kaduna hakuondoi sononeko la mke wa  Dadiyata na watoto wao wawili wala hairejeshi uhuru wake.

Maombi ya kutaka kuachiliwa kwa Dadiyata bado yanaendelea kurushwa katika kurasa za Twitter yakiwa na hashtagi ya #MwakaMmojaBilaDadiyata, ikiwa ni dai la Uhuru wake kutoka kwa Wanaijeria.

Bulama Bukarti alilalamikia “maumivu” ambayo “uharamia huu” umeisababishia familia ya Dadiyata:

Mtumiaji huyu wa Twitter “alighafilika” alipoyasikia mahojiano ya mke wa Dadiyata:

Akin Akíntáyọ̀ haelewi jinsi  Dadiyata anaweza  “kupotea bila kujulikana alipo kwa mwaka mzima:”

Bahati mbaya ni kama vile hakuna mtu anayejali kumtafuta mkosoaji huyo:

Kinyume chake “taasisi za serikali zote za jimbo na serikali kuu zinapambana” kuepuka  lawama “kutokufanya chochote” alisema mwanaharakati wa Haki za Binadamu Professor Chidi Odinkalu katika mahojiano yake  na Vyral Africa:

Besides saying that they don’t know where he is. Nobody has really made the effort to tell us what they have done to find him and how it is that they can’t account for him. It tells you how so little we matter as citizens. The least we can do is ask where Dadiyata is and why can’t our government find him.

Zaidi ya kusema kuwa hawajui alipo, hakuna mtu ameonesha  jitihada za kutuambia wamefanya nini hasa ili kumpata  na ni jinsi gani hawatakiwi kuhusishwa naye. Hii inakuonesha ni jinsi gani hatuna maana kama raia wadogo. Kidogo tunachoweza kufanya ni kuuliza yuko wapi Dadiyata na ni kwa nini serikali yetu haimtafuti?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.