Baada ya mapinduzi ya Sudani, mamlaka za mpito za Sudani zimesaini makubaliano ya amani na The Sudan Revolutionary Front — kikundi kikuu cha waasi ambacho kimeendelea na utendaji wake hata baada ya kuondolewa kwa kiongozi wake wa zamani Omar al-Bashir, mwaka jana.
Makubaliano haya ya amani ya Kihistoria yalisainiwa hapo Agosti 31, katika mji wa Juba, Sudani Kusini ambapo yanaungwa mkono na jumuiya za Kikanda na zile za Kimataifa kama vile nchi za Kitroika, Umoja wa Ulaya, Misri na baadhi ya nchi za Ghuba.
Pia jambo hili la kusisimua limegubikwa na kipindi cha mafuriko ya Kihistoria ambayo yameathiri baadhi ya maeneo ya Sudani, yakisababisha kuendelea kuporomoka kwa uchumi ambao tayari ulikuwa umeshadorora.
Hata hivyo bado raia wa Sudani mitandaoni walisherehekea habari hizo mitandaoni.
Bloga wa Kisudani Waleed Ahmed aliandika:
اليوم نرد الجميل ❤ .. نرد الوطن
- الفيديو لحظة إعلان حركة جيش/تحرير السودان بقيادة مناوي وقف إطلاق النار دعما لحراك ثورة ديسمبر 16/2/2019 #سلام_السودان pic.twitter.com/YItG1V0B6l
— Waleed Ahmed (@alkangr) August 31, 2020
Leo tunajitolea, tunarudi nyumbani. Video ambayo inaonesha jeshi (Sudan Liberation Movement (SLMAA) likiongozwa na Minawi likitangaza kuweka silaha chini hapo Disemba 16, 2019, ili kuunga mkono harakati za mapinduzi.
Mini Arko Minawi, kiongozi wa SLMA, aliandika:
التوقيع الذي تم في الامس سوف يضع السودان في زخم جديد ، علي الاطراف والشعب السوداني والاحزاب والمجتمع المدني بتعاون مع الاصدقاء والجوار الاقليمي علينا صنع منصة متينة لتاريخ جديد لبلادنا .
— Mini Arko Minawi. | مني اركو مناوي (@ArkoMinawi) September 1, 2020
Utiaji saini wa jana utaiweka Sudani katika mwendo mpya, katika vyama na kwa watu wa Sudani, mashirika na vyama vya kijamii katika ushirikiano na marafiki na kanda jirani. Lazima tutengeneze jukwaa madhubuti kwa ajili ya historia mpya ya nchi yetu.
Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok aliyakaribisha makubaliano ya amani kwa kusema:
أهدي السلام الذي وقعناه اليوم بدولة جنوب السودان الشقيق إلى أطفالنا الذين ولدوا في معسكرات النزوح واللجوء لأُمّهات وآباء يشتاقون لقراهم ومدنهم، ينتظرون من ثورة ديسمبر المجيدة وعد العودة، وعد العدالة، وعد التنمية، ووعد الأمان.#سلام_السودان pic.twitter.com/sQRpunAlMo
— Abdalla Hamdok (@SudanPMHamdok) August 31, 2020
Ninaituma amani ambayo tumeitilia saini leo katika Taifa letu la Sudani kwa watoto wetu ambao wamezaliwa ukimbizini na katika makambi, kwa baba na mama ambao wanatamani vijiji na miji yao wakiyasubiri kwa hamu mapinduzi tukufu ya Disemba, ahadi ya kurejea, ahadi ya haki na ahadi ya maendeleo na usalama.
Makubaliano haya yanavihakikishia uhuru wa kujitawala wenyewe vikundi vya waasi katika maeneo wanayoyashikilia chini ya uangalizi wa serikali kuu. Makubaliano yatahakikisha kuwa theluthi moja ya viti vya ubunge ni vya watu kutoka katika maeneo ya waasi ili kuwasilisha mahitaji na masuala yao. Makubaliano pia yanahakikisha haki na usawa kwa wote ambao walishtakiwa na uongozi uliopita wengi wao wakiwa ni watu ambao sio Waislam au watu wasio na asili ya Kiarabu.
Haya sio Makubaliano ya kwanza ya amani katika historia ya Sudani. Baadhi ya wananchi mitandaoni walisema kuwa makubaliano ya amani ni mzunguko wa kawaida nchini Sudani na yanaweza yasilete amani wala utulivu.
Inbal Ben Yehuda aliandika:
An event that occurs once in every 5-9 years is not a "historic moment". It's routine.
—
Abuja peace agreement – 2006
Doha peace agreement – 2011
Juba peace agreement – 2020
—
Better to wait before we celebrate. #Sudan #Darfur#سلام_السودان— Inbal Ben Yehuda (@Inbaluna) August 31, 2020
Tukio linalotokea mara moja kila baada ya miaka 5-9 sio “jambo la Kihistoria” ni mzunguko tu.
—
Makubaliano ya Amani ya Abuja – 2006
Makubaliano ya Amani ya Doha – 2011
Makubaliano ya Amani ya Juba – 2020
—
Bora tusubiri kabla ya kusherehekea #Sudan #Darfur#سلام_السودان
Makubaliano Hayajakamilika
Pamoja na uwepo wa tukio hili la kusisimua, makundi mawili ya waasi hayajatia saini makubaliano haya. Kikundi cha SLMA kiliongozwa na Abdul Wahid al-Nur, na Chama cha harakati za Uhuru wa Wasudani kaskazini (SPLM-N), kinachoongozwa na Abdelaziz al-Hilu, wote walijitoa kwa sababu ya kutokujibiwa kwa baadhi ya maswali kuhusu mfumo wa uendeshaji wa jeshi la muungano na utambulisho wa nchi.
Siku tatu baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya amani Waziri Mkuu wa Sudani alisafiri kwenda Addis Ababa, Ethiopia, kuonana na al-Hilu kujadili kuhusu ya mgongano huo kulingana na Usuluhishi wa Sudani
Prime Minister Abdallah Hamdok on Wednesday held a secret meeting with Abdel Aziz al-Hilu in an effort to break the deadlock in the peace talks mediated by the South Sudanese government.https://t.co/IrNxxW9a0M pic.twitter.com/VgtyDZxfv3
— Sudan Tribune (@SudanTribune_EN) September 3, 2020
Hapo Jumatano, Waziri Mkuu Abdallah Hamdok alifanya mkutano wa siri na Abdel Aziz al-Hilu zikiwa ni jitihada za kuondoa vikwazo katika mazungumzo ya amani yaliyofanywa na serikali ya Sudani Kusini. .https://t.co/IrNxxW9a0M pic.twitter.com/VgtyDZxfv3
Mkutano huu ulisababisha kusainiwa kwa mkataba utakaosimamia kuheshimiwa kwa makubaliano ya amani yaliyofanyika huko Juba.
Mitandao ya kijamii ya Sudan ilizizima kwa kusambazwa kwa nakala ya makubaliano hayo yaliyoandikwa kwa lugjs ya Kiingereza, mkazo ukiwa katika kipengele cha 3 kinachozungumzia masuala ya dini na utaifa:
A democratic state must be established in Sudan. For Sudan to become a democratic country where the rights of all citizens are enshrined, the constitution should be based on the principle of ‘separation of religion and state’ in the absence of which the right to self-determination must be respected. Freedom of belief and worship and religious practice shall be guaranteed in full to all Sudanese citizens. The state shall not establish an official religion. No citizen shall be discriminated against based on their religion.
Taifa la kidemokrasia lazima lisimikwe Sudani. Kwa Sudani kuwa Taifa la kidemokrasia ambapo haki za watu wote zinaheshimiwa, katiba lazima iwe na misingi ya ‘kutenga udini na utaifa’ ambapo haki za mtu binafsi lazima ziheshimiwe. Uhuru wa kuamini na kuabudu na shughuli za kidini utolewe kwa wananchi wote wa Sudani. Serikali isiweke dini ya Taifa, asiwepo mwananchi atakayebaguliwa kwa sababu ya dini yake.
Wananchi wa Sudani wamegawanyika katika makundi mawili katika suala hili: kundi la kwanza linaona kuwa kutenga uraia na dini ni jambo la msingi katika misingi haki za Binadamu; kundi la pili linaona kuwa serikali ya mpito haina mamlaka ya kufanya maamuzi juu ya jambo hilo bila ruhusa ya wananchi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia.
Baada ya mkutano huo, ukurasa wa Twitter wa Waziri Mkuu ulichapisha nakala ya mkataba huo kwa lugha ya Kiarabu ambapo maudhui yake yalitofautiana na yale yaliyopo katika nakala iliyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Wakati katika nakala ya Kiingereza msisitizo umewekwa kwa kuonesha kuwa haiwezekani kutenganisha dini na utaifa, katika nakala ya lugha ya Kiarabu inapendekeza “majadiliano” katika suala hili lenye utata.
Tofauti katika nakala hizi mbili umeibua maswali mengi kuhusu hatma ya makubaliano haya.
Amani Ya Kihistoria, Mafuriko Ya Kihistoria
Wakati amani ikileta furaha nchini Sudani, mto Nile unaendelea kufurika ukileta majanga yasiyotarajiwa kwa binadamu.
Kulingana na taarifa ya Septemba 8 ya, baraza la Ulinzi wa Taifa, kutokana na mafuriko hayo vimetokea vifo vya watu 103, majeruhi 50, vifo vya mifugo 5,482, nyumba 27,341zimebomoka kabisa na nyumba 42,210 zimebomoka nusu, majengo ya serikali na taasisi binafsi 179 yameharibiwa, maduka na maghala 359 yameharibiwa na hekari 4,208 za mazao zimeharibiwa na mafuriko hayo.
YouStorm katika ukurasa wake wa Twitter walionesha video wakilinganisha ujazo wa maji katika mto Nile Julai 16 na Agosti 16:
Floods on the Nile in Sudan ?? 16 July comparison with 30 August #Sentinel2 ?️ north of Khartoum. Made with #EOBrowser @sentinel_hub #Sudanfloods pic.twitter.com/l8LRNBFY9m
— YouStorm (@YouStormorg) August 30, 2020
Mafuriko katika mto Nile nchini Sudani ?? Julai 16 ukilinganisha na Agosti 30 #Sentinel2 ? Kaskazini mwa Khartoum. Imetengenezwa kwa #EOBrowser @sentinel_hub #Sudanfloods pic.twitter.com/l8LRNBFY9m
Hapo Septemba 3, gavana wa jimbo la Sinnar, Ustadhi Elmahi Sulieman alitangaza hali ya hatari katika ukurasa wake wa Facebook:
The levels of the Blue Nile this night witnessed a great rise accompanied by heavy rain, which led to the breaking of the covers and shields, ‘a simple dam built by sacks of the soil,’ of the city of Singa and Umm Benin areas, and the water began to flood the city and its homes, as well as the neighbourhoods of Umm Benin. Therefore, we launch a directive to all official bodies and an appeal to all civil authorities and organizations to come to the rescue of the citizens as soon as possible, and to provide shelter, medicines and food.
Kimo cha maji ya Mto Nile usiku huu kimeongezeka kutokana ma mvua kubwa ambazo zimesababisha kuvunjika kwa vizuizi na kuta za ulinzi ‘ambavyo ni bwawa dogo lililojengwa na magunia yaliyojazwa udongo’ za mji wa Singa na maeneo ya Umm Benin, na maji yameanza kufurika katika mji na katika makazi ya watu. Hivyo basi tunatoa maelekezo kwa mamlaka zote za serikali na mashirika binafsi kujitokeza na kuja kusaidia kuwaokoa wananchi mapema iwezekanavyo na pia kuwapatia hifadhi, chakula na matibabu.
Hali ni ya kutisha:
ولاية سنار | مدينة سنجة
الوضع كارثي بعد أن كسرت الأمطار ترس البحر مما أدى لدخول مياة النيل الأزرق للمدينة pic.twitter.com/1fk94r6hnC— Wli (@wmuhaker) September 3, 2020
Katika Jimbo la Sinnar | mji wa Singa, hali ni ya kutisha baada ya mvua kuvunja ukuta wake wa kizuizi hivyo kuruhusu maji kutoka Mto Nile kuingia mjini.
Vijana wa Kisudani kutoka kisiwa cha Tuti walijenga ukuta wa kuzuia maji ya mafuriko kuingia ndani ya kisiwa chao. Kilikuwa kitendo cha kishujaa, alisimulia Hassan Shaggag:
هؤلاء من سيبنون السودان .. وليس اللذين يتصارعون على السلطة الآن #السودان_الوضع_المعيشي #تحديات_الفتره_الانتقاليه pic.twitter.com/OBApXgY6Us
— Hassan Shaggag (@HassanShaggag) August 29, 2020
Hawa ndio watakaoijenga Sudani..na ndio wanaogombea madaraka sasa.
Wananchi wa Sudani wana upungufu wa mahitaji muhimu kama vile mkate, gesi, madawa na umeme- baada ya kukatika kwa umeme kwa masaa sita kwa siku. Kudorora kwa fedha ya Sudani sasa imezidi asilimia 202, kulingana na Professor Steve Hanke. Hata hivyo, mpaka sasa serikali ya mpito haijaweza bado kulitawala soko.
Sasa tena kuna ahadi ya amani, ni nini hasa mkakati wa serikali kuyarahisisha maisha ya wananchi?