#MatrikiUtambulisho: Mazungumzo ya Twita yanayoangazia utambulisho na haki za kidijitali barani Africa

Chumba cha Intaneti cha TEDGlobal. Picha ya Creative Commons ya mtumiaji wa Flickr, Erik (HASH) Hersman, Juni 3, 2007. (CC BY 2.0)

Global Voices, kupitia waandishi wake wa Ukanda wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahari kwa ushirikiano na Mradi wa Rising Voices itaendesha kampeni ya mtandao wa twita kama sehemu ya mradi unaofahamika kama, “Utambulisho: Jukwaa la kudhibiti vitisho vya mtandaoni dhidi ya uhuru wa kujieleza barani Afrika,” kuanzia Aprili 20 mpaka Mei 22, 2020.

Kama mwendelezo wa “Uandishi wa Kuelekea kwenye Uhuru: Siasa na haki za kidijitali barani Afrika ,” kampeni hii ya wiki tano ya mtandao wa kijamii kuhamasisha jamii itashirikisha mjadala ulioandaliwa na @GVSSAfrica ukiwashirikisha wanaharakati wa lugha tano za Kiafrika, ambao wataangazia uwiano wa lugha na haki za kidijitali.

Mradi huu umefadhiliwa na Mfuko wa Haki za Kidijitali Afrika  unaoendeshwa na Ushirikiano wa Sera za kimataifa za TEHAMA kwa ajili ya Afrika ya Mashariki na Kusini (CIPESA). Global Voices ni mmoja wapo wa wanufaika wa ufadhili huo. 

Wanaharakati hao watatwiti kwa lugha za ki-Afrika kama vile ki-Bambara, ki-Igbo, ki-Khoekhoe, ki-N|uu, ki-Swahili, ki-Yorùbá, sambamba na ki-Faransa na ki-Ingereza.

Pia wataweza kutushirikisha uzoefu na uelewa wao binafsi kwa mtazamo wa lugha kuhusu changamoto zinazotishia haki za kidijitali.

Mazungumzo hayo yatahoji namna gani tishio la kutoegemea upande wowote mtandaoni linavyoathiri maudhui ya mtandaoni kwenye lugha za Kiafrika; uenezaji wa taarifa potovu katika lugha za Kiafrika kwenye lugha tofauti mtandaoni na kile kinachofanywa na makampuni au mashirika ya kijamii kuhusiana na hili; athari za ukosekanaji wa mtandao wa bei nafuu katika maeneo yaliyo na jamii kubwa za wazungumzaji wa lugha ya Kiafrika; umuhimu wa na changamoto za haki ya kupata taarifa katika lugha za kidijitali a Kiafrika. Vile vile, wataangazia suala la sera za mashirika, na pia changamoto zinazoendelea kuwepo zenye uwezo wa kuathiri jinsi raia wanavyoweza kujielezea huru katika lugha yao.

Kutana na waendeshaji wa mjadala huo kwenye mtandao wa Twita

Mjadala huu wa Twitter utawasilishwa na Denver Toroxa Breda (ki-Khoekhoe/ki-N|uu/Kiingereza) kutoka Afrika Kusiki, Adéṣínà Ghani Ayẹni (ki-Yorùbá/ki-Ingereza) kutoka Nijeria, Kpénahi Traoré (ki-Bambara/ki-Faransa) kutoka Burkina Faso, Roseblossom Ozurumba (ki-Igbo/ki-Ingereza) kutoka Nijeria na Bonface Witaba (ki-Swahili/ki-Ingereza) kutoka Kenya.

Baadhi ya washiriki hao walishiriki kampeni ya mtandaoni ya @DigiAfricanLang  kuadhimisha Mwaka wa Kimataifa wa Lugha za Asili 2019.

Aprili 20-24: Denver Toroxa Breda (@ToroxaD

Denver Toroxa Breda. Picha imetumiwa kwa ruhusa.

Breda mzungumzaji wa Kikhoe, mwenye utamaduni wa Kuwiri au mwanaharakati, ni mwandishi anayepigania urasimishaji wa lugha za Kikhoekhoe na kin|uu, lugha mbili za kwanza nchini Afrika Kusini. Kikhoekhoe kinazungumzwa nchini Namibia, kinasomwa mashuleni, lakini Afrika kusini ambako ndio chimbuko lake, ni watu 2,000 tu wanakizungumza, sio lugha inayotambuliwa rasmi, haipo shuleni. Lugha ya Kin|uu ina mzungumzaji gwiji mmoja tu, sio lugha inayotambuliwa rasmi, na mashuleni, na ni lugha iliyoko katika hatari ya kutoweka.

Kpénahi Traoré. Picha imetumika kwa idhini.

April 27-May 1: Kpénahi Traoré (@kpenahiss)

Kpénahi Traoré alizaliwa Côte d'Ivoire lakini asili yake ni Burkina Faso.

Yeye ni mhariri mkuu wa RFI mandenkan, chumba cha habari cha lugha ya Kibambara katika shirika la Radio France Internationale (RFI).

Imekuwa ni uzoefu mzuri kwa Traoré kufanya kazi katika lugha ya Kibambara. Kabla ya hapo, alidhania kuwa isingewezekana kabisa kufanya uandishi wa habari katika lugha ya Kibambara

Kisamogo ndio lugha ya mama ya Traoré, japokuwa alikuwa na lugha iitwayo Kidioula huko Côte d'Ivoire na Burkina Faso.

Wamali wanakiita Kibambara, Waguinea wanakiita Kimalinke, wengine wanakiita Kimandingo.

Mei 5-8: Blossom Ozurumba (@blossomozurumba)

Blossom Ozurumba. Picha imetumiwa kwa ruhusa.

 

Ozurumba pia anajulikana kama Asampete, jina ambalo linaweza kutafsiriwa kutoka kwa lugha ya Kiigbo kumaanisha “yule mzuri.”

Ozurumba anafurahishwa na lugha na utamaduni ya Kiigbo na amejitolea kuhakikisha kuwa watu kadhaa wanajifunza kwa kiasi fulani kuzungumza, kuandika na kusoma.
Ozurumba ni mwanzilishi wa kundi la kiigbo la watumiaji wa Wikimedia na mara kwa mara huenda akaanzisha mazungumzo kuhusu Wikimedia Foundation bila kushinikizwa.

Anaishi jijini Abuja, Naijeria, na anapenda utulivu na hisia ya mwendo wa aste aste wa jiji.

Mei 11-15: Ọmọ Yoòbá (@yobamoodua)

Adéṣínà Ayẹni. Picha imetumiwa kwa ruhusa

Adéṣínà Ayẹni, ambaye pia anajulikana kama Ọmọ Yoòbá, ni mwandishi wa habari na mwanaharati wa utamaduni ambaye anatumia kazi yake ya uanahabari kuendeleza
utunzaji, na usambazaji wa urithi wa utamaduni wa Kiyorùbá mtandaoni na nje ya mtandao.

Kama msanii wa sauti, ametayarisha matangazo mengi ya Kiyorùbá ya kampeni za redio za Naijeria na TVC. Yeye ndiye mwanzilishi wa Urithi wa Utamaduni wa Yobamoodua, jukwaa lililojitolea kueneza lugha na utamaduni wa Kiyorùbá. Ọmọ Yoòbá pia ni meneja wa lugha wa tovuti ya
Global Voices Yorùbá.

Yeye ni mwalimu wa lugha ya Kiyorùbá katika tribalingua.com ambako anafunza wanafunzi kutoka sehemu mbali mbali duniani. Pia amefanya kazi na Localization Lab, jamii ya kimataifa ya watafsiri wa kujitolea na watumiaji mtandao, watengenezaji programu za kompyuta, na wapatanishaji ambao wanafanya kazi kwa pamoja kutafsiri na kubinafsisha vifaa vya usalama vya kidijitali na ala za kukwepa ufungiwaji au uzimwaji mtandao. Ọmọ Yoòbá ameandika kitabu kiitwacho: “Ẹ̀yà Ara Ẹ̀dá Ọmọ Ènìyàn,” mkusanyiko wa michoro yenye majina ya anatomia na muundo wa mwili wa binadamu na mimea ambayo hufanya kazi ya kushangaza kwenye kila sehemu ya mwili. Yeye ni mshiriki wa utafiti katika shirika la Firebird Foundation for Anthropological Research.

May 18-22: Bonface Witaba (@bswitaba)

Bonface Witaba. Picha imetumika kwa ruhusa.

Witaba mwandishi, mtengenezaji maudhui ya asilia na mwanaharakati, mkufunzi, mtafiti, na mshauri wa masuala ya utawala wa mtandao na sera.

Yeye ni mwanzilishi wa ICANNWiki Swahili, tovuti kamusi yenye dhamira ni kukuza, kutafsiri, makala na misamiati 10,000 ya utawala wa mtandao hadi lugha ya Kiswahili kwa wazungumzaji milioni 150 wa Kiswahili ifikiapo 2020.

Vile vile, Witaba anaendesha mradi wa vijana unaolenga kujenga uwezo wa wanafunzi, wasomi, na watu binafsi kwenye sekta ya kibinafsi na; serikalini, kupitia kozi za kitaalamu kuhusu utawala wa mtandao.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.