Kukamatwa kwa Mwandishi Mchunguzi Ivan Golunov Kwaleta Mageuzi katika Jamii ya Urusi

Mimi na sisi (Wote) ni Ivan Golunov. Bendera iliyotolwa na Meduza, na kutumiwa kwa ruhusa

Точка кипения: Haya maelezo ya lugha ya Kirusi maana yake ni kiwango cha kuchemka —kiwango ambacho kikifika inatosha inakuwa inatosha —labda njia nzuri ni kuwasilisha namna idadi ya warusi walioguswa na kukamatwa kwa Ivan Golunov mwandishi mchunguzi maarufu inavyoongezeka.  Alikamatwa tarehe 6 Juni Moscow kwa kile kinachoonekana  mashitaka ya kusingiziwa  ya kujihusisha na kumilki madawa ya kulevya.

Golunov alikamatwa na kukataliwa kuonana na mwanasheria jambo ambalo ni kinyumecha sheria za Urusi. Mwanasheria wake alithibitisha ana maumivu makali akiwa mahabusu . Baada ya kupelekwa hospitalini aliruhusiwa na kuwekwa kwanye nyumbe maalumu tarehe 8 Juni.

Mwanzoni Askari wa Urusi walionesha picha za maabara ya madawa ya kulevya zinazosadikiwa zilipigwa kwenye nyumba ya gorofa ya Golunov lakini baadaye picha hizo ziliondolewa. Pia chombo cha habari cha pro-Kremlin nchini Urusi leo  kimethibitisha kwamba picha zile hazikupigwa kwenye Gorofa za Golunov. Mashtaka aliyozushiwa Golunov yanaweza kumpelekea kupewa kifungo cha miaka 10 hadi 20 gerezani.

Golunov mwenye maika 36 anafanya kazi  Meduza, moja ya mitandao ya jamii michache ya kuijitegemea inayotumia lugha ya Kirusi iliyobaki Urusi.  Meduza ilisajiliwa katika nchi jirani ya Latvia, lakini ina ofisi na waandishi wa habari wachache nchini Urusi . Golunov ameongoza kuchapisha uchunguzi wa matukio kadhaa ya rushwa yanayowahusisha viongozi wa ngazi za juu.

Tangu Golunov akamatwe, Meduza imekuwa ikitoa makala za Golunov chini ya leseni ya creative commons na imehamasisha vyombo vya habari na watu binafsi  kuzichapisha tena habari hizo, jambo ambalo limeungwa mkono kwa nguvu na Global Voices. Miongoni mwa habari muhimu alizochapisha ni kuhusu makamu Meya Pyotr Biryukov alivyopitisha miradi kwa ajili ya familia yake  na namna mradi wa kuifanya moscow kuwa mji wa kuvutia ulivyokuwa na bajeti iliyozidi makadirio. Habari aliyokuwa anashughulika nayo kabla hajakamatwa ilikuwa inahusu ukiritimba wa huduma za mazishi katika Moscow.

Kukamatwa kwa Golunov kumechochea kauli za mshikamano ambazo zilikuwa nadra miongoni mwa waandishi wa habari, wanaharakati na wanasheria na hata waimbaji maarufu na watu maarufu nje ya Mscow na Petersburg Mtakatifu. Tarehe 10 Juni, magazeti matatu makuu yalikubaliana kuchapisha matoleo yanayomuunga mkono Golunov katika  kurasa za mbele. Magazeti yaliuzwa na kuweka rekodi mpya. Katika hali isiyo ya kawaida vyombo vya habari vya pro-Kremlin pamoja na Channel One,   ambavyo vina watanzamaji wengi vinaomba kuwepo na uchunguzi ulio wa haki.

Tarehe 12 Juni  itakuwa ni  siku ya Urusi, ambapo matembezi na maandamano  ya umma yaliyoruhusiwa na serikali za mitaa yatafanyika. Kwa sheria za urusi, maandamano ya umma yanahitaji ruhusa. Watu wanaomuunga mkono Golunov wametangaza kuwa watakuwa na matembezi yao wenyewe bila ya kupata ruhusa rasmi.

Waangalizi wa Kremlin wanasema serikali ya Urusi inaangalia kuondoa mashtaka dhidi ya mwandishi wa habari huyo  kabla ya tarehe 20 Juni. Siku ambayo Rais  Vladimir Putin ambaye viwango vyake vimeshuka katika historia  nchini, atakuwa anaongea na  simu moja kwa moja  katika kipindi cha kuongea na umma kwa mwaka ambapo anapokea maswali kutoka kwa wananchi kwa simu na mitandao ya kijamii.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.