Vyombo Vya Habari Vya Serikali Vinamshambulia Mwanafunzi wa Shule ya Upili Ambaye Aliikosoa Serikali

Blanka Nagy akizungumza katika maandamano ya Januari 2019. Picha na Márk Tremmel, CC BY-NC-SA 2.5.

Habari hii iliandikwa na Tamás B. Kovács na kutafsiriwa na Anita Kőműves kwa ajili ya Jarida la Hungary lisilo la kibiashara, Atlatszo. Nakala hii iliyohaririwa inapatikana hapa kama sehemh ya ushirikiano wake na Global Voices.

Vyombo vya habari vinavyoiunga serikali ya Hungary mkono vimeanza mashambulizi mapya dhidi ya Blanka Nagy, mwanafunzi wa shule ya upili ambaye alizungumza vibaya dhidi ya serikali katika maandamano kadhaa tangu mwisho mwa mwaka 2018.

Nagy anavumilia ukosoaji mwingi dhidi yake na pia amedhalilishwa kijinsia na chanzo kimoja cha habari kimemuita “kahaba”.

Tayari ameshafungua kesi ya kudhalilishwa na kushinda kesi dhidi ya vyombo vitatu Lokàl, Ripost na Origo ambayo vinavyoiunga mkono serikali, vilisema kuwa alikuwa akifeli shuleni. Hata hivyo, baada ya Nady kushinda kesi dhidi ya Origo, chanzo hicho kilimshambulia tena kwa kuchapisha ripoti yake ya shule. Nady aliwaambia Atlatszo kuwa alikuwa anafikiria kuwashtaki Origo tena kwa sababu ya habari zao za hivi karibu.

Blanka Nagy amekuwa maarufu nchini Hungary katika majira ya baridi yaliyopita baada ya kutoa hotuba katika maandamano ya kuipinga serikali, ambapo alikosoa wanasiasa maarufu, huku akitumia lugha kali. Maneno yake makali yalisambazwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii kupitia video ya hotuba yake.

Miezi miwili baada ya video yake kuvuta hisia katika mitandao ya kijamii, vyombo vinavyoiunga serikali mkono na Wanazuoni kama vile Zsolt Bayer walianzisha mfululizo wa mashambulizi dhidi yake. Vyombo hivyo vilisema kuwa alikuwa akifeli masomo yake mengi na pia alikuwa amekosa siku nyingi za masomo. Pia walimuita “asiye na kipaji anayetaka kuwa maarufu” na “kahaba”.

Wakili wake alifikisha nakala ya matokeo yake mahakamani na kuonesha kuwa hakuwa anafeli katika masomo yake na pia nakala hizo za matokeo walipewa mawakili wa Origo. Chanzo hicho cha habari kiliamua kuchapisha taarifa kutoka katika ripoti ya matokeo ya Nagy na kusema kuwa alikaribia kufeli somo la Historia muhula uliopita na pia yupo katika hati hati ya kufeli masomo mengine pia.

“Mimi na Wakili wangu tunafikiria kuwashitaki chanzo cha habari kilichochapisha nakala ya matokeo yangu kutoka shuleni”, Nagy aliwaambia Atlatszo katika mahojiano. Alisema kuwa Origo hawakuwa na haki ya kuchapisha matokeo yake. Yeye na wakili wake wanadhani kuwa Origo hawakuwa na haki hata ya kuyaona matokeo yake walipoyawakilisha mahakamani.

“Na shutuma zao za hivi karibuni sio za kweli pia”, Nady alisema “Sifeli somo langu la Historia, tofauti na walichokisema. Nina matokeo mazuri  alama zangu ni zaidi ya 2 (ambayo ni sawasawa na daraja C). Wanachosema ni uongo. Ningeaibika kama ingekuwa ni kweli kwa sababu katika familia yangu kulikuwepo na mwalimu wa Historia miongoni mwa babu zangu”, alimalizia kusema.

“Nadhani matukano yote haya dhidi yangu ni kitu cha ajabu sana ila sibabaiki tena. Inaonyesha jinsi kwa namna fulani ninavyowatisha baadhi ya mamlaka za juu za chama tawala cha Fidesz. Ukweli ni kwamba kitendo cha Zsolt Bayer mwenyewe kunishambulia na vyombo vya habari vinavyounga serikali mkono kusambaza taarifa za uongo dhidi yangu, vinathibitisha hilo”, aliongeza.

Kukashfu na kutoa taarifa za uongo ndizo silaha pekee za vyombo vinavyounga mkono serikali ya Hungary. Baadhi ya mamlaka za upinzani zimejibu kwa kuvishtaki vyombo hivyo vya habari kwa kukashfu. Kulingana na takwimu za hivi karibuni zilizokusanywa na Atlatszo, vyanzo vikuu vya propaganda vimeshindwa kesi nyingi, na viliamriwa na mahakama kusahihisha taarifa mara 109 kwa mwaka 2018.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.