- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Binyavanga Wainaina Mwandishi wa Kenya, Aliyeifundisha Dunia ‘Namna ya Kuandika Kuhusu Afrika’, Afariki Akiwa na Miaka 48

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Kenya, Uganda, Habari za Hivi Punde, Haki za Binadamu, Haki za Mashoga, Mawazo, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia

Mwandishi Mkenya Binyavanga Wainaina akiwa kwenye sherehe ya Kitabu Brooklyn, mwaka 2009. Wainaina aliyekuwa na miaka 48, alifariki Jumanne tarehe 22 Mei katika Mji wa Nairobi, Kenya.  Picha na Nightscream, CC  3.0 na Wikimedia Commons.

Ni masaa 24 tu tangu  Binyavanga Wainaina Mwandish Mkenya kutoweka katika ulimwengu huu, lakini uwepo na athari yake vinaendelea kurindima duniani kote.

Msema kweli, mwandishi shoga mu-wazi  alilaumu mapatano na kutia changamoto serikali akichokoza kwa uandishi wa kimapinduzi ambao ungefungua mlango kwa maelfu ya waandishi wanaotamani kubadilika katika kuandika na kuelezea namna Afrika ilivyo.

Mwandishi, mwalimu na mwanaharakati wa LGBTQ, Binyavanga Wainaina mwenye umri wa miaka 48, alifariki [1] siku ya Jumanne tarehe 22, Mei, Nairobi, Kenya, baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Leo nimefikiria: Maisha yako yatakuwa na maana gani yanapoondoka? Kifo cha Binyavanga kimenifanya nifikirie kuhusu nilivyokuwa miaka mitano au mingi iliyopita na pia alikuwaje kwetu kama kijana mwenye tashwishi shauku na njaa ya mabadiliko mbalimbali juu ya bara letu na kwetu pia.

Fungai Machirori (@fungaijustbeing) May 22, 2019

Kwa dakika chache, rafiki, wafuasi  na mashabiki wake Wainanina walifurika kwenye mitandao ya kijamii wakibadilishana kumbukumbu na shukrani na kujadili maandiko yake mengi yenye mvuto sana

Wainaina anajulikana sana kwa makala zake za kuchokoza , “Namna ya kuandika kuhusu Afrika,” [3] iliyochapishwa katika gazeti la  mwaka 2006. Pia, anajulikana kwa kitabu chake cha kumbukumbu ya maisha yake cha mwaka 2012, “Siku moja Nitaandika kuhusu sehemu hii,” [4] na makala ya “ Mama, Mimi ni basha,” [5] iliyochapishwa Chimurenga, sambamba na Afrika ni Nchi kilichochapishwa mwaka 2014. Makala hiyo ilichangamsha sana kwenye mtandao wa Twitter kwa sababu watu walijaribu kuonesha ukweli na magazeti walimuita Wainaina kuwa ni  mmoja wa watu 100 mashuhuri wa kushawishi [6] ulimwenguni

Katika makala ya “Namna ya kuielezea Afrika,” Wainaina aliviita vyombo vya habari vya magharibi na misaada ya viwanda  — vyote vilivyopo Nairobi — kuwa vinaendeleza ubaguzi usiofaa juu ya bara la Afrika kwa kutumia dhihaka na kejeli kubwa.

Usije ukajaribu kuweka picha ya mwafrika mzuri juu ya jalada la kitabu au ndani yake isipokuwa huyo mwafrika awe ameshinda tuzo ya Nobel. Bunduki aina AK-47, midomo mizuri, matiti wazi:tumia hivi. Kama utalazimika kujumuisha mwafrika, uhakikishe unampata kutoka Masai au Zulu au nguo ya Dogon.

“Kijembe chake kilikuwa— Kisu kidogo kikali,” anaandika mwandishi Mnaijeria Nwachukwu Egbunike.

Makala au kitabu chake kilichonukuliwa sana na wanataaluma, mashirika yasiyo ya kiserikali na wafanyakazi wa kutoa misaada kimekuwa na matokeo makubwa ya uelewa juu ya Afrika na matokeo hayo yanaendelea kuzungunguka, kushangaza na kukasirisha.

Kuhusu matokeo yake, mwanadishi Pernille Bærendtsen anaandika:

Kwangu mimi, makala imenifuata tangu nilipoletewa kama zawadi mwaka 2008 na rafiki yangu Mkenya. Hakika mimi ni mmoja wa watu waliohutubiwa na Binyavanga: Mfanyakazi wa ustawi wa maendeleo aliyeajiriwa nchini Tanzania na shirika la Denmark lilisilo la serikali aliandika kuhusu matokeo ya makala hiyo. Huo ulikuwa wakati maendeleo na misaada ya viwanda vikiongezeka ufanisi wake ili kupata harambee kwa ajili ya badiliko ya gharama yaliyokuwa yanajitokeza. Nilikuwa na sababu nyingi za kujisikia aibu, lakini pia nilikuwa na muda wa kupanga namna ya kubadilika.

Baadaye Binyavanga alielezea [7] katika jarida la Bidoun namna makala hii ilivyotokea tu katika maisha na athari mbili: Kwa kuweka wazi na kuelezea hatari juu ya “waandishi wa liwaya, wafanyakazi wa mashirika yasiyo ya kiserikali, wanamusiki, wahifadhi, wanafunzi na waandishi wanaosafiri” ambao wanasoma haya maelekezo ya namna – au hata namna ya kutoandika kuhusu Afrika, huanza kuomba idhini yake.

Wainaina alikuwa mtoto wa kiume wa baba mkenya na mama mganda, aliendelea kuhoji udanganyifu unaoelezwa juu ya Afrika hasa kupitia jarida la kumbukumbu la maisha yake liliovuma mwaka 2012 lililojulikana kama “Siku moja nitaandika kuhusu  mahali hapa [8].” Ikiwa na taarifa kemkem, iliwavutia wasomaji kuanzia utoto wake katika miaka ya 1970 akiwa Kenya na kipindi akiwa mwanafunzi huko Afrika ya Kusini ambapo alikaa miaka mingi akiwa uhamishoni.

Ukosoaji ulisifia kitabu hicho kama halisi na kweli [9], lakini baadaye Wainaina alikiri kuwa alikuwa amesahau sura muhimu — upendo wa maisha yake.

“Mama, mimi ni shoga,” Wainaina alikuwa mkenya wa kwanza mwenye hadhi ya juu na kuwa mu-wazi kwa kutamka kwenye mitandao ya kijamii, na kuamsha maoni lundo kutoka kwa jamii. Ikaonekana ni “sura iliyopotea” katika kumbukumbu ya maisha yake. Wainaina aliona aseme kuwa yeye ni shoga kwa mama yake alikuwa anakaribia kufa. Makala yake ilifika kwa muda muafaka kama kampeni dhidi ya mkutano mkubwa wa kupambana na ushoga na sheria dhidi ya ushoga ilikuwa imependekezwa nchini Uganda na baadae Tanzania ambapo vitendo vya ushoga ni jinai.

Hata hivyo, tofauti na waandishi wengine waliokuwa uhamishoni,  Wainaina alirudi nyumbani kama Nanjala Nyabola anavyoelezea BBC kupitia Twitter, anasema “hiyo ilikuwa muhimu”:

Kwa wale miongoni mwetu ambao walikua pamoja na ” waandishi maarufu wa kikenya” wanaoishi uhamishoni, waliotiwa gerezani, maskini au wasiopongezwa au kukataliwa vibaya mno, yeye alirudi nyumbani na hilo lilikuwa jambo muhimu sana . Alikuwa mtu asiyeleweka lakini kwa hili anastahili shukrani daima.

‘Tunatakiwa kusema fikra zetu’

Wakati Binyavanga kiukweli alipata kupendwa na makundi mbalimbali wa kimataifa, nyumbani alikosoa na alikumbana na shinikizo  la kutostahili katika misingi iliyowekwa [12]. Binyavanga alidai nafasi ya uhuru wa kuongea na kutoa fikra. Kwa ujasiri — katika jumuia inayokuwa inayowezeshwa na LGBTQ — alisistiza juu ya kupindisha misingi ile

Katika kujibu kelele na majibu mengine, mwaka huo huo Wainaina aliandika “Tunatakiwa kusema fikra zetu,” [13] kwenye Yuotube ukiwa ujumbe wenye sehemu sita zilizofuatana zikibeba fikra zake juu ya uhuru na fikra. “Ninahitaji kuishi maisha ya uhuru wa fikra,” alieleza katika sehemu ya kwanza.

Ninaomba kizazi hiki cha wazazi vijana kuwa na vijana wanaona waafrika wakiandika habari zao wenyewe — tendo hilo rahisi ni tendo la kisiasa muhimu ambalo kila mmoja anapaswa kuwa nalo. Nina wiwa kuliona bara ambapo kila aina ya fikra za mtu hazitakiwi mpaka ziruhusiwe. Mimi ni mwafrika wa waafrika wote, ninahitaji kuona bara hili likibadilika.

Mara kwa mara Wainaina alipitsha shauku lake la madiliko kupitia uandishi wake, elimu na uongozi. Mwaka 2002, baada ya kushinda tuzo bora ya Caine kwa makala yake ya “kugundua nyumbani,”  alitumia fedha ya tuzo [14] hiyo kushirikiana  kuanzisha Kwani? [15] Gazeti lenye lengo la kuendeleza sauti  na fikra mpya zinazoibuka barani kote.

Kwani? iliendelea kwa muda likichapishwa na kuwa na mtandao ukiwaunganisha waandishi kutoka Lagos to Nairobi, Mogadishu hadi Accra.

Wakati alitikisa bila huruma mikataba ya kijamii Kenya  — alivyojitokeza hadharani kuwa ni shoga na baadaye kuweka wazi kuwa ana virusi vya ukimwi kupitia Twitter siku ya UKIMWI duniani mwaka 2016 — mara nyingi ilileta maumivu, kushindana na it often came with backlash, struggle and pain.

Wainaina alikuwa mtu  mtata ambaye alipambana akiwa na msongo na mara nyingi alipigana sana kutokana na  kuwa mtu mashuhuri shoga lilionekana ni jukumu lake tata katika jamii kama mtu wa watu. Alikuwa na mashabiki lakini alikumbana na ukosoaji kutoka kwa mwandishi mashuhuri Shailja Patel, ambaye alimshtumu [17]Wainaina kuwa mtu mwenye “sumu ya kuwachukia watu wa jinsia moja wenye mahusiano ya kimapenzi.”

Mtumiaji wa Twitter, Néo Músangi anasimulia mapungufu ys tabia ya Wainaina katika ujumbe wake kupitia Twitter:

“Sina nguvu za kutosha lakini ninamlilia Binya kama rafiki yangu kipenzi katika ugeni na utetezi wangu. Ninasikitika sana kwamba aliumiza wengine. Ninasikitika kwamba alikosea kama binadamu, angetuchukia tukimsafisha.”

Mwandishi Bwesigye Mwsigire, mkurugenzi wa Writivism Festival nchini Uganda, pia  alielezea mkanganyiko huu   [20] kupitia Facebook:

mtindo wake wa maisha ilikuwa ni tatizo. His style was a transgression. Nzuri na kuachia makosa Beautiful and freeing transgression. … Watu tunaoshikilia kwa sababu ya kazi na mawazo yao ni watu tu.[T]he people we obsess over because of their work and ideas are people after all. Ni binadamu They are human. Tupo tayari kuwapenda katika changamoto zao Are we ever ready to love them in their complexity?

Kwa sasa, mengi yamezungumzwa juu yake. hakuna haja ya kurudia yaliyosemwa. Watu wamekumbusha maumivu aliyo. … Hii aiondoi maumivu mtu anayoyasikia kwa kifo chake.

Kuna Binyavanga Wainaina mmoja tu. Ni mhenga kwa sasa. Tusherehekee maisha yake. .

‘Kipaji cha udadisi’

A queer icon, Binya — kama alivyokuwa akijulikana sana —  often received torrents of vitriolic anti-gay rhetoric that only spiked online as the news of his death spread across various channels.

Mwanaharakati Mkenya Boniface Mwangi atuma ujumbe kupitia Twitter baada ya kutuma ujumbe wa kusifia Wainaina kupitia Facebook; chuki na maoni ya ushoga zilifuata ujumbe wake. that after writing a Facebook tribute to Wainaina, hateful, homophobic comments derailed his message:  Wainaina alikuwa mtu mwenye kipaji cha udadisi ambaye inapaswa akumbukwe:

“Nilituma ujumbe mfupi kupitia Facebook juu ya kifo cha Binyavanga, #RIPBinyavanga [21] kulikuwa na maoni mabaya na aibu sana sijawahi kusoma. Hata wezi ambao hutuibia kodi na kuua watu hawapati chuki kubwa kama ile. Ukweli ni, Binya alikuwa na akili na kipaji cha udadisi na ataendelea kusomwa na kukumbukwa

Mganda ambaye ni mtetezi wa haki za akina mama na mwandishi Rosebell Kagumire alitonesha kile alichojifunza kutoka kwa ushupavu wa Wainaina wa kusema wazi:

Msiruhusu woga. Msijizuie ninyi wenyewe. Ongeeni kile kinachohitajika kusemwa. Kizurikiandikeni. Ishi ukweli wako na kwa moyo wako. Pale ambapo utapumua pumzi yako ya mwisho kutakuwa na maneno milioni yenye maana sana uliyoyatoa kwa Binyavanga

Kupitia maisha  na maandishi yake alijitoa na kuwafanya wengine idhini ya kuona maisha kivingine, na kifo chake cha ghafla kinaashiria misuri ya mashairi Through his life and letters, he gave himself and countless others the permission to imagine life as it could be otherwise, and his sudden passing inspired poetic musings:

Siku moja nitaandika juu ya nywele zako za kupendeza

Siku moja nitaandika juu ya kicheko chako

Siku moja nitaandika juu ya kutotawalika kwako

Siku moja nitaandika juu ya uwezo wako wa kufikiri

Siku moja nitaandika juu ya kukataa kwako

Leo naandika asante

Mkenya Yvonne Adhiambo Owuor ambaye ni mwandishi wa habari na mwandishi wa “Dust [26],” na kwa kweli rafiki wa Wainaina, anahitimisha kwa maombolezo ya mwisho:

“Nani alikuambia uondoke? kutoka kwenye mwili wako usiku bila kuacha anuani mpya?”

Uso umeinama, macho yanachoma, alisema. “Una sekunde 3 tu za kurekebisha manung'uniko” wewe kule. Wewe nani alikuambia uondoke? Kutoka mwilini mwako bila kuacha anuani mpya? Ni kwa nani mtu anaweza kwenda kwa hofu na kutetemeka akiwa maandishi ya kujaribia?

Sasa yeye ni miongoni mwa watu mashuhuri, unaweza kuungana na “sayari ya Binya” [29] ukiwa na kumbukumb kubwa ya kazi yake.

Sina nguvu za kutosha lakini ninamlilia Binya kama rafiki yangu mpendwa katika ugeni na utetezi wangu. Ninasikitika sana kwamba aliumiza wengine. Ninasikitika kwamba alikosea kama binadamu, angetuchukia tukimsafisha.”