- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Angola Yakabiliana na Tuhuma za Ubadhilifu kwa Kufuta Zabuni, Serikali Yadaiwa Kugawanyika

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Angola, Haki za Binadamu, Sheria, Siasa, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia
[1]

Ukurasa wa mbele wa gazeti la de Angola kuhusu zabuni iliyoshinda ya kampuni ya Telstar. iiliyopigwa na Dércio Tsandzana, tarehe 19 Aprili 2019 na kwa idhini

Rais wa Angola João Lourenço tarehe 18 Aprili alifuata  [2]zabuni ya serikali kwa ajili ya mwendesha simu za mkononi katika nchi hiyo, akisema kwamba mshindi wa zabuni Telstar hakukidhi vigezo muhimu vinavyohitajika kutoa huduma hiyo. Maamuzi ya Rais yanaweza kuonesha mgawanyiko katika serikali ya Angola.

Kampuni ya Telstar ilianzishwa Januari 2018 ikiwa na mtaji wa kwanza 200,000 (kama dola za kimarekani 600), na wadau wake wakubwa ni Manuel João Carneiro (asilimia 90) na mfanyabiashara António Cardoso Mateus (asilimia 10), taarifa hii ni kutokana [3] na gazeti la  Portuguese Observador. Kutokana [4] na taarifa mtandao wa Angola, ushindi wa Manuel João Carneiro ulitolewa na Rais aliyemaliza muda wake Eduardo dos Santos.

Gazeti la Observador lilitaarifu kwamba makampuni 27 yalishiriki katika mchakato wa kuomba zabuni ulifunguliwa na Wizara ya mawasiliano na Teknolojia ya habari chini ya José Carvalho da Rocha.

Kutokana na gazeti la Angola [5] tarehe 25 Aprili, João Lourenço alisaini taratibu ambazo ziliweka sheria mpya kwa ajili ya kufungua mwaliko wa zabuni.

Baada ya matokeo ya zabuni ya kwanza kuwekwa wazi kwa umma, wananchi wengi wa Angola walihoji uadilifu katika mchakato huo. Wengine walikwenda mbali kwa kusema kwamba mshindi Telstar hajawahi kuwa na tovuti haya yalisemwa na Skit Van Darken, mhariri na muongozaji wa vipindi kupitia Facebook [6]:

A Telstar – Telecomunicações, Lda, constituída a 26 de Janeiro de 2018, com capital de 200.000 Kwanzas…de acordo com o Diário da República, cujos accionistas são o general Manuel João Carneiro (90% do capital), na reforma, e António Cardoso Mateus (10%).

O accionista maioritário tem ligações à empresa Mundo Startel, uma sociedade de capitais anónimos, registada na INACOM, o regulador das telecomunicações, com licença de telefonia fixa, entretanto expirada. Uma empresa que nem se quer website tem!

EU NÃO ACREDITO SE QUER QUE EXISTIRAM OUTROS CONCORRENTES

ESSE PAÍS É UMA DESGRAÇA

Tafsiri: Telstar – Telecommunications, Ltd, ilianzishwa tarehe 26 Januari 2018, na mtaji wa Kwanza 200,000… kutokana na gazeti la Diário da República, ambalo wadau wake ni  the general Manuel João Carneiro (asilimia 90) na  António Cardoso Mateus (asilimia 10).

Mshikadau mkubwa ana uhusiano na kampuni ya Mundo Startel, kampuni yenye dhima inayojitosheleza, iliyosajiliwa INACOM, mdhibiti wa mawasiliano akiwa na leseni ingawa imeshapita muda wake. kampuni ambayo haina hata tovuti!

SIAMINI HATA KIDOGO KWAMBA KULIKUWA NA WASHINDANI WENGINE

NCHI HII NI AiBU

kwa sasa, Joaquim Lunda [7], mwandishi wa habari na mtangazaji wa mara kwa mara katika mitandao ya kijamii, alisifia kitendo cha Rais na hata nilifikilia kuwa waziri mhusika alikimbia hatari ya kufukuzwa kwa kushindwa huku:

Agradeço e é de louvar a decisão tomada pelo Presidente da República, João Lourenço em anular o concurso público que atribuiu à empresa angolana Telstar a licença para a quarta operadora de telecomunicações em Angola. Havia muitas reticências e muitos pontos por esclarecer no assunto. Não se reconhece idoneidade numa empresa que foi criada em 2018 c/ capital social de 200 mil kwanzas em ser lhe atribuído a tal empreitada.
Tenho a plena certeza que os dias do Ministro das Telecomunicações e das Tecnologias de Informação, José Carvalho de Rocha, estão contados. Após o desaire que foi o ANGOSAT 1, agora mais este que testemunhamos hoje, duvido se o “Dread” vai resistir.
Apreciemos os Cenários…Nas Calmas!!”

Tafsiri Ninshukuru na ni kitendo cha kupongezwa, maamuzi yaliyochukuliwa na Rais wa Jamhuri, João Lourenço, kufuta zabuni ya serikali ambayo kampuni ya Angola ya Telstar ilishinda leseni ya kuwa mwendeshaji wa mawasiliano katika Angola the licence for the fourth telecommunications operator in Angola. kulikuwa na watu wengi kutoridhishwa na mambo mengi ya muhimu ya kuweka wazi mazuiyoThere were many reservations and a lot of points to clarify around the issue. Mtu haoni tija katika kampuni ambayo iliundwa mwaka 2018 na mtaji wa Kwanza elfu 200, kupewa tuzo ya zabuni.
Nina uhakika kabisa kuwa siku za waziri wa mawasiliano na teknolojia ya habari zinahesabika. Baada ya kushindwa na  ANGOSAT 1, sasa na hiki tunachoshuhudia leo, nina wasiwasi kama “Hofu” kama itafanya lolote. .
Tufurahie mchezo huo… kimya kimya!!”

Uamuzi wa Rais ulikuja baada waziri yule yule aliyeongoza mwaka 2017, mradi wa setilaiti Angosat 1,   anaingia kwenye matatizo [8]  tena.

Adriano Sapiñala [9], makamu wa chama kikuu cha upinzani yeye anaona tatizo linaonesha mfarakano katika serikali:

JLo tem de andar a combinar bem com os seus auxiliares porque ontem o Ministro de tutela dizia que o tempo das reclamações tinha terminado e por isso a Telstar teria avançado com os passos subsequentes sendo ela vencedora do concurso fraudulento e hoje JLo vem e anula o concurso!! Vocês comunicam assim tão mal?

Agora ou o Ministro coloca o seu cargo à disposição (demitindo-de) ou então JLo tem de o exonerar porque se anulou o concurso é porque não correu bem e para não beliscar ninguém inocente, que se apurem responsabilidades!!

Tafsiri: JLo [João Lourenço] anapaswa kupanga vizuri timu yake kwa sababu jana waziri mwenye dhaman alikuwa anasema kwamba muda wa malalamiko umeisha na kwa hiyo Telstar ingeendelea na hatua inayofuata kutokana na kwamba ilikuwa mshindi wa zabuni ya ulaghai na leo JLo anajitokeza na kufuta zabuni! Mawasiliano si mazuri?

Sasa labda waziri aweke msimamo wa (kujihuzuru) au JLo anapaswa kumfukuza kwa sababu kama amefuta zabuni ni kwa sababu mchakato wake haukuwa mzuri na ili isiathiri mtu yeyote safi lazima watu wawajibike!!