- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Papa Francis Ataitembelea Makedonia Kaskazini Mwezi Mei, Muda Mfupi Baada ya Uchaguzi wa Rais

Mada za Habari: Ulaya Magharibi, Ulaya Mashariki na Kati, Macedonia, Vatican, Dini, Mahusiano ya Kimataifa, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia
Picha ya Papa Francis katika tovuti papa.mk [1]

Picha za skirini kutoka katika tovuti ya papa.mk, imewekwa na Serikali ya Jamuhuri ya Makedonia Kaskazini wakati Papa alipowatembelea Mei 7, 2019.

Papa Francis ataitembelea Makedonia Kaskazini Mei 2019, kwa siku mbili baada ya raundi ya pili ya uchaguzi wa Rais.

Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Papa kutembelea Makedonia Kaskazini. Kutembelewa huko itakuwa ni sehemu ya ziara ya siku tatu katika ukanda huo ambapo pia atatua Bulgaria.

Serikali ya Makedonia Kaskazini imetengeneza [2] tovuti, ya papa.mk [1] kuwezesha ziara hiyo. Kutokana na uwepo wa tamaduni mbalimbali katika nchi, maudhui katika tovuti hizo yanapatikana kwa lugha tatu tofauti ambazo ni Kimakedonia, Kialbania na Kiingereza.

Baadhi ya wananchi wameuliza kuhusu serikali kumiliki tovuti hiyo, wakisema kuwa inaleta utata kwa sababu serikali hiyo haina dini.

Wananchi wa Makedonia wanaweza kuomba tiketi za kuhudhuria Ibada Takatifu [3] itakayoendeshwa na Papa ambapo tiketi hizo zinapatikana bure katika makanisa nchini wakati wageni toka nje ya nchi wanaweza kupata nafasi kwa kupitia tovuti. Ibada hiyo itafanyika katika viwanja vya Mji Mkuu wa Skopje, Mei 7.

Wakatoliki wanwanaf angalau asilimia moja ya watu wote wa Makedonia Kaskazini ambapo asilimia 65 ni Wakristo wa ki-Orthodox na angalau asilimia 33 ni Waislamu. Pamoja na idadi yao ndogo, jamii ya Kikatoliki ina watu mbalimbali kama vile Wamakedonia, Waalbania, Wakroeshia, Waslovenia na Wapoland.

Kwa upande mwingine, nchi hii ina maana kubwa katika ukatoliki kwa sababu mji wake mkuu Skopje ndipo alipozaliwa Mama Theresa [4](1910-1997), ambaye alitunukiwa kuwa Mtakatifu Teresa wa Calcutta. Mmoja kati ya wamisionari wa karne ya 20 na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, alizaliwa katika familia yenye asili ya ki-Albania ambapo nyumba yao ilikuwa pale ambapo kwa sasa ni uwanja mkuu wa mji.

Kipengele cha kisiasa katika ziara hiyo kinafunika umuhimu wake kidini. Kama mkuu wa nchi, Papa amepangiwa kuonana na waziri mkuu na rais anayemaliza muda wake [5], ambaye madaraka yake yatakoma siku tano baadaye.

Wamakedonia wanaona ziara hii kama ishara ya kutambuliwa na nchi za Magharibi na kuinua jitihada za serikali kuiweka nchi karibu na uanachama wa NATO na Umoja wa Ulaya. Hisia hizi zinapatikana huko twita katika chapisho la jenerali mstaafu wa polisi Stojanche Angelov, ambapo alitoa maoni katika ziara ya maandalizi ya Mkuu wa Taasisi ya Usalama wa Raia ya Makedonia kwa Vatican.

Asante kwa siasa za hekima na za kijasiri zilizoamuliwa na serikali hii, nchi yetu ndogo inasonga mbele kwa kasi kubwa. Mkurugenzi wa Taasisi ya Usalama wa Raia, Sasho Tasevski aliandaa usalama wa hali ya juu kwa ajili ya Papa Fransis atakapokuwa hapa Skopje.
Stevo [Pendarovski] kwa urais!

Mwezi mmoja kabla ya safari ya Papa, habari za Vatican mfumo wa habari wa Holy See, waliongeza lugha ya Kimakedonia [8] katika kazi zake. Ni lugha ya 34 inayopatikana katika chombo hicho. Askofu wa Skopje, Askofu Kiro Stojanov alisema “hili ni tunda la awali la ziara ya kitume ya Papa Francis.”

Septemba, Papa atatembelea Msumbiji, Madagascar na Mauritius. Global Voices imeandika mrejesho kutoka Msumbiji [14] kuhusu ziara hiyo.