- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mwaka Mmoja Baada ya Maandamano wa-Nicaragua Hawaishii Kutaka Ortega Aondoke -Wanataka Mwanzo Mpya

Mada za Habari: Amerika Kusini, Nicaragua, Haki za Binadamu, Maandamano, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Vita na Migogoro
[1]

“Hawawezi kutuwekea mawazo yao vichwani mwetu hivyo wanatupiga risasi #SOSNicaragua” Ndivyo linavyosomeka bango la mwandamanaji mmoja wakati wa maandamano kwa ajili ya wafungwa wa kisiasa huko Managua. Agosti, 2018. Picha na: Jorge Mejía Peralta (CC BY 2.0)

Tangu maandamano makubwa dhidi ya Rais Daniel Ortega yalipuke [2] nchini Nicaragua Aprili 2018, serikali imepiga marufuku maandamano, imewakamata maelfu bila kuwafungulia mashtaka na kufungia kwa pamoja vyanzo vikuu na vile mbadala vya habari. Majaribio ya kufanya mazungumzo yameshindikana,  kwa sasa hatma ya Nicaragua imebaki kuwa swali gumu.

Maandamano [3] yalianza kwa kupinga mabadiliko ya sera za mifuko ya hifadhi za jamii ambapo yangepandisha makato ya kodi ya mapato wakati ikipunguza maslahi ya kiinua mgongo [4]. Mwanzoni mchakato [5] huo ulifanywa na mamlaka ulifungua mlango wa maandamano ya nchi nzima yakimtaka Rais Daniel Ortega, mkewe na Makamu wa Rais Rosario Murillo wajiuzulu.

Takwimu za vifo vilivyotokana na maandamano hayo yanapishana na hayajahuishwa tangu mwaka jana kwa sababu vikwazo dhidi ya uwekaji wa taarifa na kumbukumbu umeongezeka. Disemba 2018 serikali iilizifungia baadhi ya NGO [6] ambazo zilikuwa zikifuatilia kwa karibu vurugu za polisi na uvunjaji wa Haki za Binadamu ikiwepo kituo cha Haki za Binadamu cha Nicaragua (Cenidh [7]) na Taasisi ya Maendeleo ya Demokrasia (Ipade [8]).  

Pia Disemba hiyo, vikundi viwili vya Kamisheni ya Haki za Binadamu Ndani ya Amerika (IACHR)—Mpango Maalumu wa Kuratibu Ufuatiliaji Nicaragua (MESENI) na Kikundi cha Wanazuoni Huru wa Fani Mbalimbali—walifukuzwa kutoka nchini [9], na kuiacha Nicaragua bila chombo huru cha kusimamia Haki za Binadamu na kufungua “hatua mpya ya unyanyasaji [10]”, hii ni kulingana na Mwanaharakati wa haki za Wanawake na Muelimishaji María Teresa Blandón.

Soma zaidi: ‘Sisi ni Wahanga tunaowasaidia wahanga': Wakinakili uvunjaji wa Haki za Binadamu Nicaragua [11]

Makadirio ya chini ya majeruhi, waliotambuliwa na serikali [12] Agosti 2018 imeongezeka na kufika 197. Hata hivyo, Shirika la Haki za Binadamu, limekaridia kuwepo kwa vifo 322 [13] mpaka ilipofika Septemba 18 2018, ambapo vifo vingi vilikuwa kwa kupigwa risasi kichwani, shingoni na kifuani.

Mwanablogu Ana Siú [14] aliandika kwenye Medium hivi karibuni kuhusu uzoefu wake katika maandamano ya Aprili 2018. [15]:

A través de una transmisión en vivo en Instagram, vi a una amiga de la universidad ser atacada por turbas. Escuché cómo ella gritaba y luchaba por no salir lastimada […] Finalmente, el “motorizado” la soltó, pero se llevó consigo el celular sin saber que seguía transmitiendo. Entonces dijo: “vamooos, vamooos. Hay que llevar estos celulares a revisarlos”. Esto siguió como por 20 minutos. 

Nilimuona rafiki yangu wa chuoni akiwa anashambuliwa na genge kupitia Instagram Mubashara. Nilimsikia akipiga kelele na akipambana kuepuka kuumizwa […] Mwishowe, mwanaume aliyemshambulia akiwa kwenye pikipiki alimwacha lakini alichukua simu yake. Hakujua kuwa bado anaonekana mubashara. Kisha akasema, “tuondoke! Tunatakiwa kuzichukua hizi simu zikakaguliwe”. Tukio hilo liliendelea kwa dakika 20.

Pia aliangazia kuhusu maandamano ya Mei 30, ambapo yalikuwa maandamano ya kihistoria yaliyoitishwa katika tarehe ambayo Nicaragua husherehekea siku ya Mama ambapo watu 15 waliuawa. [16]:

Este día cambió la forma en que vivíamos las protestas. Los que estábamos en esa marcha multitudinaria vimos cómo asesinaron a jóvenes. Fue la primera vez que atacaron con balas de plomo a una marcha masiva. Nunca me había sentido tan cerca de la muerte como esa tarde.

Siku ile tulibadili mitazamo yetu kuhusu maandamano. Baadhi yetu tuliokuwa katika maandamano yale tuliona jinsi walivyokuwa wanawaua vijana. Ni mara ya kwanza polisi  kushambulia maandamano makubwa kama yale kwa risasi za moto. Sijawahi kuwa karibu na kifo namna hiyo.

Wakati wanafunzi walipozuiana [17] wenyewe kwa wenyewe katika vyuo vikuu katika mji mkuu wa Managua, wafanyakazi wa mashambani walifunga barabara [18] katika maeneo ya mashambani. Hapo Juni waandamanaji wa Masaya waliutangaza mji wa Mashariki kuwa “mamlaka huru kutoka kwenye udikteta [19]”. Serikali iliwashambulia waandamanaji waliotengeneza vizuizi vya kujilinda na kujibu mashambulizi ya polisi. Waandamanaji walizidi kujihusisha na vurugu na mapigano na kufikia Agosti 2018 vilikuwa vimetokea vifo 22 vya maafisa wa polisi, na hii ni kulingana na takwimu za serikali. [12].

Katikati ya 2018 [20], polisi walianzisha walichokiita “operación limpieza” (Operesheni ya kusafisha) kuharibu vizuizi na kuwashtaki watuhumiwa walioshukiwa kujihusisha navyo. Taarifa zinasema kuwa vyombo vya usalama vilifanya hivyo vikishirikiana na Vikundi vya wanamgambo [21].

Wanafunzi wengi [22]viongozi [23] wa harakati za wakulima, wapigania haki  [24]na wanahabari [25] walilengwa katika kampeni hiyo hatari na wengi wao wameshtakiwa, [26] na baadhi ya watumishi wa afya waliohudumia majeruhi wakati wa maandamano wamepata misukosuko kwa kile walichokifanya [27]. Chama cha Madaktari wa Nicaragua wamesema kuwa angalau madaktari 240 [28] walifukuzwa kazi katika hospitali za umma kama njia ya kuwakomoa.

Soma zaidi: Waandamanaji wa Nicaragua na waandishi wa habari wakumbana na mashambulizi makali mitaani na kwenye mitandao. [29]

Hapo Septemba maandamano yalifanywa kuwa sio halali tena [30], na shughuli zozote kwa sasa katika mitaa zinahitaji [31] kibali maalum kutoka kwa mamlaka, ambapo mara nyingi vibali hivyo hukataliwa. [32].

Hapo Februari 27, 2019, meza ya  mazungumzo [33] ilirejelewa kati ya serikali na chama cha upinzani, Alianza Cívica por la Justicia y la Democracia (Muungano wa Haki na Demokrasia kwa Raia), ikifuatiwa na kuachiliwa huru kwa mamia ya watu kutoka gerezani. [34]. Ukilinganisha na mazungumzo ya kipindi kilichopita, kikao hiki hakikujumuisha viongozi wa harakati za wakulima na wanafunzi [35], kwa sababu baadhi yao wako kifungoni, na wengine wapo uhamishoni. [36]

Sio Rais mpya pekee—ni mwanzo mpya

Kwa kuwa mgogoro huu wa nchi unaingia mwaka wa pili sasa, wahka na wasiwasi wa kesho ya Nicaragua umebebwa na hashtagi #SOSNicaragua [37], ambayo hutolewa kila siku pamoja na madai, picha za waathirika na vilio juu ya wanafunzi walio magerezani na familia zao. 

Soma zaidi: Wanaharakati wa Diaspora wa Nicaragua wabeba mzigo “mara mbili”’ [38]

Chanzo cha habari cha Nicaragua, Niú [39] waliwahoji waandamanaji walioongoza maandano ya Februari katika maeneo ya jirani na Costa Rica na walielezea ugumu wa maisha waliyo nayo huko uhamishoni.

Alejandro Donaire, mwanafunzi alisema kuwa alikimbia nchini baada ya kushiriki maandamano ya amani, aliiambia Niú jinsi ilivyo vigumu “kujisikia kuwa sehemu ya jamii na maisha ya kawaida,” baada ya kutumia muda mrefu kwa ” kuishi kwa kujificha, kukimbia na kuandamana”.

Madelaine Caracas, msemaji wa kikundi cha wanafunzi kinachofahamika kama Ushirikiano wa Wanafunzi kwa Demokrasia [40], pia alishirikisha Niú kiu yake ya kutaka kuona mabadiliko ya Nicaragua ambayo yatakuwa ni zaidi ya Ortega kuondoka:

[Tenemos que] erradicar autoritarismos, machismos, caudillismo y demás males que han penetrado en la cultura política del país […] Ahora, más que nunca, estamos seguros de que Ortega se va este año […] este año estaré en Nicaragua y tengo [esa seguridad] porque (Ortega) está ahogado internacionalmente, está ahogado económicamente y también porque la parte insurreccionada que se levantó en abril está hoy, más que nunca, más organizada.

[Tunataka] kuuondoa udikteta, ukandamizaji wa kijinsia, ubinafsi na madhaifu mengine ambayo yamejipenyeza katika utamaduni wa siasa za nchi. Tunaamini zaidi kuwa Ortega ataondoka mwaka huu na kwamba nitarudi Nicaragua mwaka huu. Na nina hakika kwa sababu Ortega kwa sasa hasikiki katika anga za kimataifa na za kiuchumi na pia kwa sababu wale wote walioshiriki maandamano ya Aprili wamejiandaa kikamilifu kwa sasa.

Raundi hii ya mwisho ya mazungumzo kati ya Serikali na upinzani ilifikia mwisho [41] Aprili 3, kukiwa na makubaliano katika mada mbili kati ya nne zilizojadiliwa. Kwanza serikali imeahidi kuwa, itawaachia huru [42] wafungwa wote wa kisiasa na pili itaheshimu uhuru wa raiaHapakuwepo na  makubaliano [43] yoyote yaliyofanywa kuhusu haki kwa wahanga wa vurugu za uchaguzi au kujinadi kwa ajili ya uchaguzi wa 2021.

Kikundi cha upinzani cha Muungano wa Kiraia ulisema kuwa, hata hivyo serikali imeshindwa kabisa kuheshimu makubaliano hayo [44]. Imeendelea kuripotiwa kuwa, Polisi wameendelea kuvuruga maandamano ya amani  [45]. Kama ilivyokuwa April 6, ni wafungwa 50 pekee kati ya wafungwa wa kisiasa 600 walioachiliwa huru [46], na waliowekwa katika vizuizi majumbani mwao.

Baadaye hapo April 17, kufuatia kitisho kipya cha [47] kuwekewa vikwazo na Marekani, zaidi ya wafungwa 600 waliachiliwa huru na kwenda kumalizia vifungo vyao katika vizuizi vya nyumbani, hata hivyo kulingana na Muungano wa Kiraia, ni wanachama 18 pekee [48] wa kikundi hicho waliokuwa katika orodha ya wafungwa wa kisiasa waliokuwa na tumaini la kuachiliwa huru. Katika fikra za watu kama vile Mwanaharakati na mtafiti Felix Madariaga [49], kiongozi mpya wa Kesho ya Nicaragua amebaki gerezani leo [50].

Wakati huo huo, vikundi vya upinzani vimeitisha maandamano ya kuadhimisha kumbukumbu ya [48] matukio ya Aprili 2018. Kukiwa na katazo toka kwa mamlaka [51] na zuio la kibali dhidi ya maandamano hayo, pia inatarajiwa kuwa kutakuwepo na ukandamizaji mpya kutoka kwa polisi.