Benin Yashuhudia Kuzimwa kwa Mtandao Siku ya Uchaguzi

Swichi ya kuwasha na kuzima. Picha na Andrew Huff. [Creative Commons (CC BY-NC 2.0)/ Flickr, Tarehe 20 Januari, 2007]

Walipoamka tarehe 28 Aprili, wakiwa tayari kupiga kura katika uchaguzi wa wabunge nchini Benin’ wapigakura hawategemea kukuta WhatsApp au Facebook ambazo zinatumika kuwasiliana au kupata habari wapi pa kupigia kura.

Baadhi ya mitandao mikubwa ikiwemo Twitter, Instagram, Telegram na Viber ilikuwa imezimwa mapema siku ile. Mpaka saa 5 Asubuhi, asilimia 99.5 ya upatikanaji wa mtandao ulikuwa haupatikani na kuipeleka nchi ya Afrika magharibi kutokuwa na mtandao nchi nzima ambapo mtandao ulifunguliwa usiku.
Vikundi vya haki za binadamu na waangalizi wa uchanguzi walikatishwa tamaa lakini bila taharuki kwa ajili ya kukosekana kwa mtandao ambako inaonekana kupangwa na serikali iliyopo madarakani.

Sheria mpya za uchaguzi zilizowekwa na uongozi uliopo wa Rais Patrice Talon umefanya mageuzi ya siasa katika Benin ambapo hadi mwaka huu ina vyama vingi vya siasa vinavyoshindana. Lakini chini ya sera mpya ambazo zinaweka kizingiti kwa chama kushiriki katika chaguzi isipokuwa vyama viwili ambavyo vimeweza kuweka wagombea katika uchaguzi huu wa wabunge. Vyama hivyo vyote vipo karibu na Rais.

Katika kuelekea uchaguzi, kulikuwa na mfululizo wa maandamano ya wananchi – ambayo yalitokea ingawa kulikuwa na kuzuiliwa kwa waandamaji mtaani waliosambatishwa na vyombo vya jeshi la polisi ambavyo vilitumia mabomu ya kutoa mchozi na marungu kuvunja maandamano. Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International liliripoti kuwa viongozi wa vyama vya upinzani wengi walikamatwa kipindi cha maandamano.

Wanaharakati mtandao wa wazi wa shirika la vyombo vya habari kwa Afrika Magharibi , Mtandao bila mipaka , CIPESA, Access Now, Sauti za Dunia (Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika) na makundi mengine yalishtumu kuzimwa kwa mtandao katika taarifa ya pamoja:

Kamati ya Haki za binadamu ya Umoja wa mataifa ambayo ndiyo mtafsiri rasmi wa mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia na kisiasa inasistiza katika kutoa maoni ya jumla namba 34 kwamba makatazo ya kuongea mtandaoni ni lazima yatiliwe umuhimu ili kupata malengo halisi. [7] Kuzima kuna matokeo yasiyo mazuri kwa watumiaji na pia nikuwanyima fursa ya kupata habari na mawasiliano ya dharura wakati huu muhimu. Kuzima sio muhimu pia huadhiri upatikanaji wa malengo halisi kwa kuwa mara nyingi hueneza kutokuelewa na kuhamasisha watu wengi kujiunga kwenye maandamano.

Kwa heshima tunawaomba:

  • kuhakikisha kwamba mitandao ya kijamii inarudishwa katika hali yake ya mwanzo
  • Tangazeni kwa umma ahadi yenu ya kuhakikisha mtandao utakuwa wazi na mtaarifu umma kwa usumbufu wowote utakaotokea
  • Wahimizeni watumiaji wa mawasiliano na mtandao kuheshimu haki za binadamu kupitia uwazi wa sera na vitendo vyenye matokeo mabaya kwa watumiaji.

Akiongea na mtandao bila mipaka mwandishi na mwanaharakati raia wa Benini Mylène Flicka wa gazeti la Irawo alisema:

Kuzima mtandao siku ya uchaguzi inaongeza tu mashaka kwa mchakato wa uchaguzi ambao tayari una dosari. Kwa sasa Benin inafanya vibaya katika masuala ya Demokrasia.

Mitandao yote iliunganishwa na kuwashwa asubuhi tarehe 29 Aprili muda ambao kupiga kura kulikuwa kumefungwa tayari.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.