- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Wanawake wa Afghanistan Watuma Ujumbe kwa Serikali na Taliban: Tunataka Tujumuishwe

Mada za Habari: Asia ya Kati, Afghanistan, Maendeleo, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Wanawake na Jinsia

Mabaraza ya Wanawake ya Jirga yanaendelea katika majimbo yote ya Afhanistani. Picha imetumika kwa ruhusa kutoka kwa Wanawake wa Afghanistan kwa ajili ya Amani.

Katika miezi inayokuja Afghanistan itaandaa mkutano wa kwanza kabisa wa wanawake kwa ngazi ya kitaifa, ambapo wanawake maelfu wataungana kuikumhusha serikali na na Taliban kuwa amani wanayoisubiri kwa kipindi kirefu haitawezekana bila sauti zao.

Kwa miongo kadhaa iliyopita ya vita, wanawake wa Afghanistan wamekumbana na unyanyasaji wa kutisha ambao umeongeza kutengwa kijamii na kuwafanya wawe na tahadhari kisiasa

Kanuni za kuwatenga wanawake katika ngazi ya taifa ziliibuka chini ya utawala wa Taliban ambao uliichukua nchi katikati ya 1990 kabla haujaondolewa na uvamizi ulioongozwa na Marekani.

Mabaraza ya Wanawake ya Jirga yanaendelea katika majimbo yote ya Afhanistani. Picha imetumika kwa ruhusa kutoka kwa Wanawake wa Afghanistan kwa ajili ya Amani.

Uvamizi huo ulisababisha kupatikana kwa elimu ya msingi lakini wanawake walibaki na jinamizi la kutokuwa salama na tishio la vurugu.

Upendeleo dhidi ya wawakilishi wanawake katika bunge haujabadili asili ya utamaduni wa siasa za Afghanistan ambao umetawaliwa na wanaume zaidi.

Kuanza kuonekana tena kwa Taliban katika meza za mazungumzo huko Moscow [1] na Doha [2] imekuwa tishio kubwa kwa mafanikio haya yaliyofikiwa kwa sasa.

Kikundi hicho kimeendelea kushikilia msimamo wake wa kutokutambua nafasi ya mwanamke katika Umma na katika serikali ya Afghanistan ambayo bado hawajafanya nayo mazungumzo ya ana kwa ana.

Hivi karibuni Taliban wamependelea kuzungumza na Washington, Moscow na kuchagua vikundi vya wanasiasa wa Afghanistan. Kikundi hicho kimesema [3] kuwa nafasi yake katika haki za wanawake iko mstari mmoja na ile ya dini kuu Afghanistan, Uislam na imebaki na uhasama na uharakati wa kutafuta usawa wa kijinsia.

Mabaraza ya Wanawake ya Jirga yanaendelea katika majimbo yote ya Afhanistani. Picha imetumika kwa ruhusa kutoka kwa Wanawake wa Afghanistan kwa ajili ya Amani.

Kuwa Umesikika

Na wanawake wa Afghanistan na wanaharakati wa haki za wanawake kutoka maeneo yote wamekutana na kuunda kampeni ya Wanawake wa Afghan kwa ajili ya Amani [4], a  ikiwa na washiriki 15,000 na zaidi kutoka katika majimbo yote 34.  

Kampeni hiyo ilianza miezi sita iliyopita kama mpango shirikishi wa Mtandao wa Wanawake wa Afghan [5], Wizara ya Masuala ya Wanawake [6], Baraza Kuu la Amani [7], na Ofisi ya Mke wa Rais wa Afghanistan [8].  

Katika kila jimbo, Wanawake wa Afghan kwa ajili ya Amani waliwaleta pamoja wanafunzi wa kike kutoka vyuo vikuu, wanawake wafanyakazi serikalini pamoja na wanawake waliosoma na wasiosoma wakitoa maoni yao.

Kwa pamoja wameshirikishana matakwa na mitazamo yao kuhusu amani.

Mabaraza ya Wanawake ya Jirga yanaendelea katika majimbo yote ya Afhanistani. Picha imetumika kwa ruhusa kutoka kwa Wanawake wa Afghanistan kwa ajili ya Amani.

Waandaaji walizungumza kuhusu nafasi za wanawake katika serikali na jamii na walishirikisha njia za kuwa na matokeo chanya katika jamii na kufanya sauti zao kusikika na mamlaka zote za ngazi ya shina na Taifa.

Kusudi la awali ni kutengeneza makubaliano ya kitaifa kuwa wanawake wa Afghanistan wasisahaulike. Wanawake wanahitaji kupata nafasi katika mazungumzo ya amani na kushirikisha matakwa yao na matarajio yao ya baadaye kwa ajili ya Taifa.

Mabaraza ya Wanawake ya Jirga yanaendelea katika majimbo yote ya Afghanistan. Picha imetumika kwa ruhusa kutoka kwa Wanawake wa Afghanistan kwa ajili ya Amani.

Makongamano tayari yalishafanyika katika majimbo kadhaa ikiwemo Panjshir [10], Khost [11], Parwan [12], Baghlan [13], Ghazni [14], na Logar [15]. Makongamano yataendelea katika majimbo mengine 28 yaliyosalia kwa majuma kadhaa yajayo.

Kifuatacho ni kibwagizo cha kongamano la jimbo la Khost:

Katika hitimisho la kila kongamano washiriki waliafiki kuhusu azimio kuhusu vipaumbele na changamoto wanazokutana nazo wanawake nchini.

Wakati hakuna tarehe yoyote iliyowekwa kwa ajili ya kongamano la kitaifa (baraza la kikabila), tukio hili liliahidi kuweka pamoja kazi zote za makundi kwa ngazi za majimbo.    

Kufanyia kazi katika ngazi ya jimbo ni muhimu sana. Wakati kuna wanawake wawakilishi katika bunge huko Kabul wanawake magavana [16] ni wachache sana kama ambavyo uwakilishi wa wanawake ni muhimu katika mengine. Kwa wanawake wengi wa majimbo ya pembezoni makongamano haya yamekuwa fursa pekee ya kwanza kabisa kwao kushiriki katika mchakato wa kisiasa na sauti zao kusikika.

Wanawake wa Ghazni [14] walisema:

Amani haimaanishi kuisha kwa vita pekee, na hakuna Taifa litakalofanikiwa katika mipango yake ya Kitaifa bila ushirikishwaji wa wanawake; kwa hiyo wanawake lazima wapewe nafasi katika mchakato wa amani ya kisiasa na kijamii.