- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Wanahabari Hawa wa Colombia Wanahitaji Kuelewesha kuwa Pablo Escobar Hakuwa Shujaa

Mada za Habari: Amerika Kusini, Colombia, Historia, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vyombo na Uandishi wa Habari
[1]

Picha ya skrini kutoka katika tamthilia ya La Pulla “Pablo Escobar ni shujaa,” inapatikana YouTube.

Jambo hili halikuanza na tamthilia kutoka  Netflix, lakini Narcos kwa hakika ilisaidia  kufufua [2] hadhi ya muuzaji mkubwa wa dawa za kulevya  kwa miaka ya 1980 wa Colombia ndugu Pablo Escobar katika utamaduni maarufu Amerika Kaskazini. Tangu imezinduliwa mwaka 2015, tamthilia zenye utata zimechochea mijadala [3] kuhusu Colombia kuendelea kuonekana kimataifa kama [4] Paradiso ya dawa za kulevya inayoshikiliwa na wauza dawa za kulevya wachakaramu.

Kama kujibu hilo, mwandishi wa habari wa Colombia aliye nyuma ya chaneli ya YouTube ya La Pulla [5] (kwa Kihispania, “Kauli”), ambapo ni mradi wa gazeti la ki-Colombia la El Espectador, alitengeneza video akijibu watu ambao bado wanamtukuza Escobar kama “shujaa”. Kati ya mambo mengine, video hiyo inaonesha vipengele vya majanga na takwimu za vipindi vibaya zaidi katika historia ya Colombia kama vile kuuawa kwa mkurugenzi wa zamani wa  El Espectador, Guillermo Cano [6] Disemba 17, 1986, na shambulizi la bomu [7] karibu na ofisi zao Disemba 1989.

Ni kawaida katika nchi nyingine kuona watu na fulana zake, wakihamasishwa na tamthilia kutoka Netflix kama vile ‘Narcos’. Na watu wanapokuja Colombia hulipa fedha nyingi sana ili kwenda kutalii na kuona [8] na kufurahia mafanikio yake makubwa. […] “Shujaa” huyu aliyehamasisha watu wengi kukimbilia fedha za biashara ya dawa za kulevya [kama] njiwa wanavyokimbilia punje za mahindi na kusababisha uchumi wa nchi kuwa chungu kidogo cha kutakatisha fedha kutoka katika uuzaji wa dawa za kulevya. “Shujaa” huyu alikuwa sio rafiki wa watu: alifanya mashambulizi 623, aliwaachia raia 1710 maumivu na aliuwa watu 402.

“Shujaa” huyu alitulazimisha kulikimbia kila sanduku lililotelekezwa mtaani au katika gari lililoegeshwa bila kuwemo mtu ndani yake [tukifikiri] kuwa [litakuwa] ni bomu lingine moja. “Shujaa” huyu alitulazimisha kujifungia ndani, kumshuku kila mtu na kujihami kwa moto na vurugu. Shujaa huyu alitulazimisha kuishi maisha ya hofu isiyokoma .

Waongoza watalii waliojumuishwa katika video hii wanafahamika kama Waongozaji wa Narco [8], na huwaongoza watalii kuzunguka mji wa Medellin kupitia maeneo maarufu yanayohusiana na maisha ya Pablo Escobar. Mwaka 2018, mshirika wa Global Voices, Radio Ambulante [9] aliwaelezea waongozaji hao katika moja ya sehemu ya vipindi vyao vya podcast vilivyopata tuzo.