Wanachama Vigogo wa Vyama vya Upinzani Tanzania Wanahamia Chama Tawala

Edward Lowassa alikuwa mwanachama wa muda mrefu wa chama tawala CCm hadi alipoondolewa katika kinyanganyiro cha kugombea Urais na alijiunga chama cha Upinzani CHADEMA. Hivi Karibuni, amerudi CCM. Picha ilipigwa kwenye YouTube kupitia chombo cha habari cha KTN cha Kenya. Tarehe 18 Octoba, 2015.

Katika Tanzania, wanachama vigogo wa vyama vya upinzani wamehama na kurudi chama tawala, Chama cha Mapinduzi, hali hiyo imeadhiri siasa za vyama vingi katika taifa hili la Afrika Mashariki.

Wanachama wengi ni wale waliokuwa katika chama kikuu cha upinzani, chama cha Demokrasia na Maendeleo au CHADEMA, ambapo miaka michache iliyopita wabunge wake wanne, madiwani 75 na baadhi ya wenyeviti wa vijiji wamehamia CCM.

Jukwaa la katiba Tanzania limedai kuwepo na marekebisho ya katiba kwa kuwa yanaweza kuzuia kuhama huko “lengo ni kuepuka gharama zisizo za lazima ambazo serikali inaingia katika kuendesha na kuratibu mara kwa mara chaguzi za marudio,” alieleza Hebron Mwakagenda mwenyekiti wa TCF.

Tume ya Uchaguzi ya Taifa imeratibu mara kadhaa chaguzi za marudio kwa gharama kubwa ambayo matokeo yake kumekuwepo na idadi ndogo ya wapiga kura. Lakini pia mchakato wa kupiga kampani umejenga hali ya woga na kutokuaminiana miongoni mwa wananchi.

Suala la Edward Lowassa

Tarehe 1 mwezi Machi, 2019, Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa na mjumbe wa Halmashauri kuu ya CHADEMA alikihama chama hicho na kurudi chama chake cha zamani cha CCM baada ya kukihama miaka minne iliyopita.

Katika sherehe fupi ya kumkaribisha, mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alimkaribisha Lowassa kwa mikono miwili :

Ndugu Lowassa amejionyesha kuwa yeye ni mtu muungwana. Tumefundishwa kusamehe…..na nia yetu ni kujenga nchi mpya, Tanzania yenye Umoja bila siasa za kuleta migogoro.

Lowassa alithibitisha kuwa amerudi nyumbani na hakuna sababu kwa sasa hivi kuwa katika chama cha upinzani.

Lowassa ni mmoja wa makada wachache waliolelewa na kuandaliwa na chama cha umoja wa kitaifa au TANU ambacho ni miongoni mwa vyama cha kwanza vilivyoundwa kabla Tanzania kupata uhuru kutoka kwa Mwingereza mwaka 1961, na baadaye aliandaliwa na umoja wa Vijana wa CCM kipindi cha mfumo wa chama kimoja.

Soma zaidi :

“Hata mneng’uaji mzuri huondoka jukwaani: Viongozi maarufu Afrika: Katika kipindi cha mpito cha Siasa”

Chini ya uangalizi wa CCM, Lowassa aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Monduli kwa miaka 25 na kushika nyadhifa za uwaziri kwa miongo minne. Mwaka 2008 kipindi cha Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete wakati Lowassa ni waziri mkuu Lowassa alilazimika kujihuzuru baada ya kuhusishwa na udanaganyifu katika sakata la kampuni ya kufua umeme ya RICHMONDI.

Lowassa alijiunga na CHADEMA tarehe 4 Agosti , 2015, kuelekea uchaguzi mkuu baada ya CCM kumuondoa kwenye orodha ya wagombea urais katika chama hicho. Baada ya kuondolewa aliishtumu CCM na viongozi wake kuwaita “madikteta, wasio na demokrasia na wenye uchu wa madaraka.”

Baada ya kuhamia CHADEMA, chama hicho na washirika wake walimteua Lowassa kuwa mgombea Urais chini ya UKAWA ambao ulikuwa ni umoja wa vyama vya upinzani. Katika uchaguzi mkuu huo wa mwaka 2015, Lowassa alipata kura milioni sita sawa na asilimia 40, dhidi ya kura milioni 8.8 za Magufuli wa CCM ambazo zilikuwa sawa na asilimia 60.

Kutokana na ushawishi wa kisiasa aliokuwa nao Lowassa, vyama vya upinzani kama, CHADEMA kilivuna viti 70 vya ubunge ukilinganisha na viti 48 vya mwaka 2010, wakati Chama cha wananchi (CUF), pia kikiwa mwanachama wa UKAWA kilipata viti 45 ukilinganisha na 36.

Ni kukaribishwa au Kushawishiwa ?

Kurudi kwa Lowassa katika chama tawala kumeibua pongezi na kejeli kutoka kwa wanasiasa na wachambuzi maarufu wa mambo ya siasa. Mwenezi na msemaji wa CCM, Humphrey Polepole alimpongeza Lowassa kwa maamuzi yake shupavu ya kurudi kwenye chama chake cha zamani na cha muda mrefu:

kurudi na kuomba msamaha ni uungwana na unyenyevu mkubwa.

Watu wengine wamesema kuwa kiwango kikubwa cha wanachama kuhama vyama sio jambo zuri kwa siasa kitaifa. Naibu Katibu mkuu wa chama cha CUF Tanzania bara, Magdalena Sakaya, alisema kuhama huko “ni hatari kwa ustawi wa Demokrasia” na inaashiria mkakati wa siri wa kuua upinzani, aliongeza.

Mkuu wa kitivo cha Falsafa na mafunzo ya Dini, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Adolf Mihanjo, aliwaita wanaohama vyama kuwa ni watu ambao hawana itikadi na wanatafuta nafasi za uongozi tu:

Watu wameanza kuona kuwa wanaohama vyama wanashawishiwa kwa kupewa rushwa hii ni hatari.

Pia, naibu Katibu mkuu wa chama cha CUF visiwa vya Zanzibar, Nassoro Mazrui, alieleza wasiwasi juu ya msitakabali wa siasa za Tanzania kwa muda ujao alisema rushwa imeghubika siasa za vyama vingi. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe anaamini wanaohama vyama wanakuwa wameshawishiwa na CCM kama njia ya kunyamazisha upinzani.

Hata hivyo, Maulid Mtulia na Godwin Mollel ambao walijiunga na CCM mwaka jana, walisema kuwa wamehama kutokana na kuridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Magufuli. Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo na mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe aliyakataa madai hayo, na kuyaita “ni madai au sababu zilizotupu ambazo hazina vigezo wala ushahidi.”

Dkt. Richard Mbunda ambaye ni Profesa wa sayansi ya siasa chuo kikuu cha Dar es Salaam, alionya kuwa ni vigumu kurudisha uhalali pindi unapotoweka. Wanaohama vyama wanajenga hali “ya kupigia kura mtu yeyote” ambayo ni janga kwa taifa: Serikali yoyote inaweza kuingizwa kidemokrasia na baadaye inaweza kusababisha uasi wa raia au utawala haramu, alisema.

Kuminywa kwa nafasi ya kisiasa kwa vyama vya Upinzani

Tanzania ilihalalisha kuwa na siasa za vyama vingi mwaka 1992 chini ya ibara ya 3 (1) ya katiba. Katika siasa za vyama vingi, vyama vya siasa vina jukumu muhimu katika kuimarisha amani inayohitajika katika mahusiano ya kisiasa kitaifa. Hata hivyo, serikali iliyopo madarakani imeweka vikwazo vinavyozuia uwezo wa vyama vya upinzani kama vile vyama kutokuwa na mikutano ya siasa na kutooneshwa kwa mijadala ya bungeni kipindi bunge linaendelea.

Mwezi Februari, marekebisho mapya ya sheria ya vyama vingi yalipitishwa ambayo yanazuia zaidi vyama vya siasa kufanya siasa kwa uhuru. Tangu Magufuli aingie madarakani mwaka 2015, kumekuwa na kuendelea kuminywa nafasi ya kufanya siasa kupitia miswada na sheria mbalimbali kuzuia uhuru wa kutoa maoni au kujieleza mtandaoni.

Wanasiasa — pamoja na viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa wameruhusiwa kufanya mikutano ya kisiasa katika majimbo yao. Wanaokwenda kinyume hukamatwa na kushtakiwa. Kabwe ambaye ni kiongozi wa ACT-Wazalendo aliamuliwa kuripoti kwa kamanda mkuu wa polisi wa mkoa wa kusini mwa Tanzania, mkoa wa Lindi kwa kuendesha mkutano wa kisiasa nje ya jimbo lake. Halima mdee, mbunge wa Kawe alikamatwa baada ya kuongea na wapiga kura wake kwa sababu ya “kufanya mkutano bila kibali.”

Kutokana na hali ya siasa ya vyama vingi iliyoghubikwa na wanachama wake vigogo kuhama kama Lowassa, vyama vya siasa vinapambana kuwepo. Ingawa tangu kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa tumaini lilikuwa kukua kwa Demokrasia.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.