Wanablogu wa Mauritania Wakabiliwa Mashtaka ya Kukashifu kwa Kutoa Taarifa ya Rushwa

Picha kupitia Nasser Weddady akiwa anawasiliana kupitia Twitter

Mamlaka za Mauritania ziliwakamata mabloga wawili, Abderrahmane Weddady na Cheikh Ould Jiddou kwa kutoa taarifa juu ya Rushwa.

Weddady na Jiddou walikamatwa tarehe 22 Machi baada ya kuitika wito wa kuitwa na kitengo cha makosa ya kiuchumi cha Mauritania. Wote walichunguza na kutoa taarifa kuhusu tuhuma kuwa Rais wa nchi Mohamed Ould Abdel Aziz anajihusisha na rushwa.
Kabla ya kukamatwa kwao, wote waliandika kupitia Facebook kuhusu tuhuma za Dolla za Kimarekani bilioni 2 zinzomhusu Ould Abdel Aziz katika akaunti yake iliyopo Dubai. Kutokana na taarifa ya chombo cha habari, mamlaka ya Falme za Kiarabu zilisimamisha akaunti yake kutokana na maombi ya idara ya Fedha ya Marekani katika mapambano dhidi ya kutakatisha fedha.

Weddady aliandikakwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa askari polisi walimhoji kuhusu chanzo chake na kwa nini hakusubiri serikali kuchunguza suala hilo. Alijibu kwamba kufungiwa kwa akaunti kuliripotiwa mtandaoni na chombo cha habari cha nje na kwamba “hana imani juu ya uchunguzi makini juu maovu yanayomhusisha Rais na wale wanaomzunguka”.

Mwanzoni mwa mwezi Machi, mabloga wote waliitwa na kuhojiwa na kitengo cha makosa ya kiuchumi juu ya taarifa yao dhidi ya rasilimali zinazotuhumiwa. Mamlaka ziliwanyang’anya pasi za kusafiria na vitambulisho vyao vya taifa na baadaye waliachiwa siku hiyo hiyo.

Pia, tarehe 22 Machi askari polisi waliwakamata watu hao wawili baada ya ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kuhitimisha kwamba taarifa zilizotolewa ni za uongo na walitarajia kuchunguza na kukamata wote waliozisambaza kwa sababu walitaka “kuidhuru nchi, taasisi zake, wananchi na mifumo wa mahakama na fedha.”

Mabloga hao wawili wapo kizimbani wakishitakiwa kwa kusambaza “shutuma za uongo” dhidi ya Ould Abdel Aziz chini ya kifungu cha 348 cha sheria katika kanuni za adhabu za Mauritania. Wanakabiliwa na kifungo kuanzia miezi sita hadi miaka mitano jela kila mmoja. Wanaendelea kuwa jela wakisubiri kutajwa kwa kesi yao.

Katika mahojiano na Global Voices kupitia WhatsApp, Nasser Wedaddy, kaka yake na Abderrahmane Weddady na mjumbe mmoja wa jumuia ya Global Voices alisema waendesha mashtaka wameshindwa kuonesha Ushahidi halisi dhidi ya Abderrahmane na Ould Jiddou. Pia alieleza kuwa mwanasheria wao amegundua hakuna kesi yoyote dhidi yao: Alisema.

Muendesha mashtaka alidai kuwa ushahidi ‘ulipotea’. Ni tafisida yake badala ya “hatuna ushahidi wowote wa kuwatia hatiani.”

Tangu mwaka 2016, Abderrahmane Weddady amekuwa akiandika na kuripoti Kuhusu kashfa ya mali isiyohamishika, ambayo mtu mmoja ambaye anadaiwa kuwa na uhusiano na familia ya Rais kumiliki kwa udanganyifu maelfu ya nyumba za Mautania na kudaiwa kuziuza, kaka yake Nasser Weddady said. Jiddou pia aliandika kuhusu kashfa hiyo kupitia ukurasa wake wa Facebook, mke wake aliliambia shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch.

Pia, Nasser Wedaddy alitoa maoni juu ya kazi hii:

Uchunguzi wa miezi 39 wa kaka yangu juu ya mpango mkubwa wa nchi wa ponzi tangu uhuru wake umesifiwa na watu wengi kama huduma kwa jamii. Aliweza kuweka wazi utapeli uliogharimu nyumba na akiba zao za zaidi ya familia 700. Aliweka wazi pia namna Rais wa sas anavyolinda na kufaidi kutokana na kashfa hiyo.

Uhuru wa kutoa maoni umeminywa kweli katika Mauritania na mara nyingi mamlaka hutumia sheria ya kukufuru kuwanyamanzisha wanaharakati wa haki za binadamu, Mabloga na waandishi wa habari ambao huongea dhidi ya utawala au kuweka wazi mabaya yanayofanywa na serikali

Katika taarifa kwa Global Voices, familia ya Abderrahmane Weddady ilidai kwamba watu hao wawili waachiwe na mashtaka dhidi yao yafutwe :

Tunahitaji wote wawili Abderrahmane Weddady na Cheikh Ould Jiddou kuachiwa huru kwa haraka na bila masharti. Na kusikilizwa kwa shauri dhidi yao kufutwe na serikali ya Mauritania iombe radhi rasmi juu ya uchochezi huu mkubwa na holela wa serikali kuwakamata wapinzani wa kisiasa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.