Rais wa Guinea Alpha Condé Awambia Wafuasi Wake Kuwa Tayari Kupambana

Ingawa katiba ya Guenea inaruhusu tu mihula miwili mfululizo kuwa madarakani, Rais wa sasa wa nchi hiyo Alpha Condé, hivi karibuni alitangaza kwamba ana nia ya kugombea urais kwa muhula wa tatu mfululizo. Ili kusaidia kufanikisha hilo, hakusita kushawishi wafuasi wake kufanya vurugu. Katika uchambuzi uliochapishwa na gazeti la Horizon Guinée, mwandishi wa bahari Sonny Camara anayeishi Conakry (mji mkuu wa nchi hiyo), alilipoti sehemu za hotuba ambayo Rais alihutubia tarehe 24 Machi, 2019:

Nitakuwa ninavua kofia yangu ya Urais. Nitavaa kofia ya uanaharakati kwa sababu sasa niko tayari kupambana dhidi ya watu hawa [katika upinzani] […] mwe tayari kukabiliana […] Hakuna mtu yeyote katika Guinea atakayenizuia kuwauliza watu wangu wanachokitaka [kwa ajili ya nchi] […] Kama [Upinzani] wanataka kushinda kirahisi, muwe tayari kuwashinda ili wajue hamuogopi kitu chochote.

Condé alichaguliwa kuwa Rais wa Guinea mwaka 2010. Ni Rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia katika historia ya nchi hiyo. Hata hivyo, uchaguzi wa mwaka 2010 ulikuwa na malalamiko kutoka kwa waangalizi wa uchaguzi ikiwepo kituo cha Carter ambapo ililipotiwa kuwa karibu kura milioni moja zilipotea katika uhesabuji wa mwisho. Condé alichaguliwa tena mwaka 2015 kwa asilimia karibu 58 ya kura zote. mwaka 2016. Idhaa mpya ya redio ya FRANCE 24 ilitangaza kuwa kampuni ya madini ya Rio Tinto ilimlipa afisa wa serikali ya Guinea dola milioni 10.5 kwa ajili ya kupata haki ya kuchimba madini katika mkoa wa Simandou.

Miezi michache baada ya kuchaguliwa mwezi Mei 2015, Condé alianza kupendekeza nia yake ya kugombea muhula wa tatu. Ibrahima Diallo ambaye ni mkurugenzi wa Liberté FM, kituo cha redio kilichopo Conakry, ilisistiza juu ya ripoti ya hali ya Guinea:

Mais, à entendre Alpha Condé dire à l’opinion publique nationale et internationale que le «souverain peuple» de Guinée décidera ou non d’un troisième mandat pour lui sous – entend que celui qui voulait être la «synthèse» de feu Mandela et d’Obama pour son pays est «pire» que ses prédécesseurs qu’il a toujours combattus durant sa vie d’éternel opposant. Aujourd’hui, quand Koro dit «c’est le peuple qui décidera», il veut juste faire porter par le vaillant peuple de Guinée le mérite pour lui de briguer «un éventuel mandat» après les deux consécutifs.

Lakini, kusikia Alpha Condé akiwatangazia wananchi na watu wakimataifa kuwa watu wa Gunea walio huru wataamua kama atagombea au hatagombea muhula wa tatu inamaanisha kwamba yeye ambaye alitaka kuwa kiunganishi kati ya marehemu Mandela na Obama kwa nchi yake ni mbaya zaidi ya mtangulizi wake ambaye alipambana maisha yake yote kama mpinzani wa maisha. Leo, wakati Koro (Jina la utani la Alpha Condé) anataka kuwafanya watu mashujaa wa Guinea kuhalalisha lengo lake la kugombea muhula wa tatu baada ya ile mihula miwili mfululizo.

Condé amenuia kutekeleza mpango wake kwa kuchukua hatua kuhakikisha hakosi kwa kumuondoa rais wa mahakama ya katiba, Kéléfa Sall, hatua ambayo haikufuata utaratibu halali. Amadou Tham Camara, mwandishi wa habari wa gazeti la Guinée News, aliandika :

Baada ya kudhoofisha CENI [Tume huru ya Taifa ya uchaguzi], hii ni taasisi ya katiba ambayo imepewa majukumu ya kusimamia uchaguzi wa kitaifa ambayo imedhoofishwa. Kuanzia sasa na kuendelea, chama kilichopo madarakani kinatakiwa kuwa na theluthi mbili ya watu wengi wenye sifa wakati wa uchaguzi wa wabunge uliopangwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2019. Watu hawa iwe ndiyo kigezo cha kuanzisha marekebisho ya katiba. Kwa hiyo itakuwa hatua kubwa ambayo imechukuliwa ya kutoondoa kizuizi cha katiba ambacho kinazuia idadi ya mihula ya rais wa Jamhuri kuwa miwili.

Inaonekana kosa la Sall lilikuwa kumuonya Condé – wakati alipokuwa kwenye sherehe ya kuapa kuongoza nchi kwa muhula wa pili– dhidi ya kubadilisha katiba. Sall alisema :

Uongozi wa taifa lazima utukusanye kwa pamoja kwa jambo la muhimu. Hatutakusanyika na watu wenye msimamo mkali ambao ni hatari kwa umoja wa taifa. Epuka njia zinazokatazwa na Demokrasia na utawala bora. Acha kukumbwa na wimbo wa vigora vya mbadilisha itikadi ya siasa, ingawa wananchi wa Guinea wamekuchagua na kuweka matumaini yao kwako, hawaendelei kuwa watazamaji tu.

Upinzani wa wananchi wa Guinea umekuwa wazi. Kwenye mkutano na waandishi wa habari tarehe 29, Machi ambao uliandaliwa na wanachama wa zamani wa halmashauri ya mpito ya taifa (aina ya bunge la mpito) na mwenyeji alikuwa ni umoja wa usiguse katiba yangu. Boubacar Siddighy Diallo, mmoja wa wazungumzaji alikumbushia kuwa katiba ya Guinea ina sehemu mbili ambazo zinafanya katiba kamili.. Alisema kuwa kwa pamoja sehemu hizi zinalinda katiba” kutobadilishwa badilishwa ili isisababishe kuathiri amani na umoja wa taifa.”

Wapinzani walijibu kwa hasira. Kwenye mkutano wa wapinzani, Cellou Dalein Diallo ambaye ni rais wa umoja wa nguvu ya kidemokrasia ya Guinea, chama huru cha siasa alisema:

Wapinzani wa jamhuri wamethibitisha utayari wao wa kuunda umoja na vyama vingine vyote katika taifa kupinga kurudishwa nyuma kwa demokrasia na urais wa Maisha ambao Alpha Condé anataka kujigawiya…

Sekou Koundouno ambaye ni kiongozi wa nguvu ya umma ya Guinea (FSG) alitangaza kupitia Facebook kuwa Kundi la wanajamii walimwandikia mwanasheria mkuu wa mahakama ya makosa ya jinai ya kimataifa wakimuomba kutupia jicho la karibu kwa taifa letu na kuchukua msimamo wa umma kuepuka vurugu katika Guinea. Pia wananchi wa Guinea walijibu kupitia Tweeter :

Maneno ya Rais wa Jamhuri yanahatarisha amani na utulivu wa jamii katika Guinea. Bado pia, ninalaani sana tabia hii ya mheshimiwa wa nchi yetu. Hakika, nilazima kuwaita Jumuia ya kiuchumi ya nchi za Afrika magharibi [CEDEAO], Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa n.k.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.