Osama Al-Najjar Mwanaharakati wa Falme za Kiarabu ‘Anasota’ Jela Miaka Miwili Zaidi Baada ya Kumaliza Kifungo Chake

Osama al-Najjar bado yupo kizuizini, ingawa alimaliza kutumikia kifungo chake miaka miwili iliyopita. Picha : Akaunti ya Twiita ya mwanaharakati

Mwanaharati wa Falme za Kiarabu Osama al-Najjar anaendelea kuwa kizuizini kimakosa, ingawa alishamaliza kutumikia kifungo chake cha miaka mitatu jera zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Al-Najjar alikamatwa mwezi Machi 2014 kwa kutuma jumbe kupitia tweeter akishtumu kwamba baba yake aliteswa gerazani na kutoa wito aachiliwe huru na wafungwa wengine waliofungwa kwa kutoa maoni yao katika Falme za Kiarabu.

Hussain Al-Najjar ambaye ni baba yake Osama, ni miongoni mwa wanaharakati 94 katika Falme za Kiarabu ambao walishtakiwa kama kikundi mwaka 2013 kwa mashtaka ya “ kuhatarisha usalama wa Taifa” baada ya kutoa wito wa mageuzi ya kisiasa katika Falme za Kiarabu. Kwa sasa anatumia miaka 11 jera.

Mwezi Novemba 2014, Baraza la usalama wa Taifa la Mahakama kuu ya shirikisho, ambalo maamuzi yake hayawezi kukatiwa rufaa, lilimuhukumu Osama miaka mitatu jera kwa kutumia sheria ya nchi ya makossa ya mtandaoni kwa mashtaka ambayo yalijumuisha “kuchochea chuki”dhidi ya taifa kwa “kuandaa na kuendesha tovuti yenye fikra na habari za dhihaka na kukashifu.”.

Alitakiwa kuachiwa tarehe 17 mwezi Machi, 2017, lakini kwa takwa la kushtakiwa na umma, Mahakama ilimuona kuwa ni ”tiishio” kwa usalama wa Taifa na iliongeza kizuizi chake bila kuthibitisha kitachukua muda gani. Miaka miwili baadaye, Osama ameendelea kuzuiliwa, bila kuwepo mwisho wa kizuizi chake.

Taasisi ya kimataifa ya kutetea uhuru na mageuzi ya kisiasa katika Falme za Kiarabu, hivi karibuni katika taarifa yake ya kuadhimisha kumbukumbu ya mwisho wa kifungo cha Osama rasmi ilisema :

Kwa kuwa hakuna shauri linaloendelea juu ya kizuizi hiki, wale wote wenye tatizo hili ni bora wakamatwe na serikali badala mahakama kutoa adhabu. Aina hii ya uendeshaji wa kutoa kizuizi unakiuka viwango vya kimataifa vya mchakato wa utoaji vizuizi.

Ingawa hakutiwa hatiani kwa makosa ya ugaidi, Osama anaendelea kushikiliwa kituo cha kutoa ushauri nasaha katika gereza la al-Razeen kwa sheria ya nchi ya kupambana na ugaidi. Mamalaka za Falme za Kiarabu zinadai kwamba madhumuni ya maamuzi hayo ni kutoa uangalizi kwa wale ambao wanaonekana ni “tiishio dhidi ya Taifa”. Hata hivyo, vikundi vya haki za binadamu, vinasema kwamba mamlaka zinatumia sheria ya kupambana na ugaidi na hizi zinazoitwa vituo vya kutoa ushauri nasaha kama kisingizio cha kuendeleza vizuizi visivyokuwa na muda usiojulikana kwa wafungwa waliofungwa kwa kutoa maoni.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.