Nchini Burundi Kuchorachora Picha ya Rais —ni Kosa la Kukupeleka Jela

Rais Jacob Zuma akitembelea Burundi tarehe 25, February, 2016. Picha: Serikali. Flickr, CC licence.

Wanafunzi sita waliwekwa kizuini siku ya Jumanne tarehe 12 katikaMkoa wa Kirundo kaskazini-mashariki mwa Burundi kwa kuchorachora kwenye picha ya Rais Pierre Nkurunziza katika vitabu vitano vya kiada. Wanafunzi hao walishtakiwa kwa “kumfedhehesha mkuu wa nchi.

Shirikisho la Taifa la Mashirika (FENADEB) yanayojihusisha na masuala ya Watoto katika Burundi limetaarifu kuwa mwanafunzi mwingine mwenye miaka 13 aliachiwa mara moja kwa sababu ya kuwa na umri mdogo chini ya miaka 15.

Wanafunzi watatu ilisemekana waliachiwa kwa muda siku ya Ijumaa tarehe 15 Machi lakini watatu waliobaki waliwekwa rumande. Wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 17, kama watapatikana na hatia wanaweza kufungwa miaka mitano jela kwa kumdhihaki Rais. Gazeti la Iwacu lilitaarifu kuwa familia za Watoto waliokamatwa walikuwa na huzuni sana.

“Kuchorachora [kwenye picha ya Rais] ni kosa linalostahili adhabu kwa sheria ya Burundi,” kutokana na ripoti ya Reuters. Hata hivyo, umri wa mtenda kosa unaweza kutumika kama “jambo la kuzuia”katika kesi hii ya wanafunzi.

Mwalimu ambaye hakutaka jina lake kutajwa
Alibainisha kuwa vitabu hivyo vya kiada vilikuwa havijakaguliwa kwa miaka kadhaa na mara kwa mara vimekuwa vikitumiwa na wanafunzi wengine, kwa hiyo ni vigumu kujua nani kaviwekea alama.
Tukio kama hilo lilitokea mwaka 2016, kutokana na mabishano juu ya Rais kugombea mhula wa tatu, ambapo wanafunzi wa elimu ya sekondari ya juu walichorachora kwenye picha ya Nkurunziza katika vitabu vya kiada. Mamlaka zilichukulia jambo hili kama kumdhihaki sana Rais na kuamua kuwafukuza mamia ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali nchi nzima, wanafunzi. kumi na moja walishtakiwa kwa “kumfedhehesha mkuu wa nchi” na “kuhatariisha amani ya nchi,” ingawa baadaye ilitaarifiwa kuachiwa.

Vitendo hivi alivikosowa sana Zeid Ra'ad Al Hussein wa shirika la haki za binadamu la umoja wa mataifa ilitoa taarifa tarehe 29 Juni, 2016:

Nimefadhaishwa na kuendelea kuripotiwa kusimamishwa shule na kukamatwa kwa Watoto wa shule na wanafunzi kwa kuchorachora kwenye picha ya Rais katika vitabu vya kiada.

Nkurunziza ni ‘Kiongozi Mkuu wa Milele’

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi. Picha na Eric Miller / Kilele cha Jukwaa la uchumi la kimataifa, Afrika, katika mji wa Cape Town, Juni 3-6 mwaka 2008. Picha kupitia Flicker (CC BY-NC-SA 2.0).

Pierre Nkurunziza amekuwa Rais wa Burundi tangu mwaka 2005. Mwaka 2015, aliteuliwa kuiongoza Burundi muhula wa tatu na chama chake katika mazingira ya kutatanisha.

Mwezi Machi mwaka jana, Nkurunziza alitajwa na chama chake cha CNDD-FDD kuwa “kiongozi mkuu wa milele”,. Katibu mkuu wa CNDD-FDD, Evariste Ndayishimiye alielezea kwa nini Nkurunziza alitunukiwa cheo hicho:

Ni kiongozi wetu. Kwa hiyo katika chama chetu… hakuna hata mmoja anayelinganishwa naye. Ni mzazi wetu; Ndiye anayetushauri. Ndiyo maana, nawaomba wanachama wetu kumheshimu kwa sababu nyumba isiyokuwa na mwanaume (Kichwa) inaweza kudharauliwa na yeyote. Kwetu, tuna kiongozi mzuri sana.

Wakati chama CNDD-FDD kikishusha hadhi ya cheo chake, Hadhi ya Nkurunziza inayoshinikizwa ni kuwa “Kiongozi mkuu wa milele” imefanya kuwa vigumu kwa mtu yeyote kukataa maamuzi yake , ukijumuisha na hoja yake ya kubadilisha mihula ya miaka miwili inayoruhusiwa na katiba ya nchi. Hii inaakisi mamlaka ya utawala wa chama tawala kuwa yapo kwa mtu mmoja Nkurunziza na wanaomuunga mkono na hasa taasisi zinazoongoza nchi.

Wachoraji wakiwa na mshikamano

Raia mtandaoni wameamua kuchorachora picha za Rais Nkurunziza kama kupinga kupitia alama za tweeter: #Nkurunziza na #Burundi:

Wanafunzi wa sekondari ya juu wapo jela kwa kuchorachora picha ya Rais #Nkurunziza.

Kuchukuliwa hatua kali ukosoaji

Serikali ya Burundi imekuwa makini juu ya ukosoaji tangu mwaka 2015, baada ya kushindwa kwa Mapinduzi yaliyopelekea mapigano wa vikundi vya waasi, ukosoaji wa ukiukwaji wa haki za binadamu, vikwazo , vya uchumi ugumu na migogoro ya wakimbizi . Jaribio la Nkurunziza la kutaka kuongoza muhula wa tatu lilipingwa na Umoja wa ulaya na Umoja wa mataifa ambao walitaka kurejeshwa kwa amani kabla ya uchaguzi. Kukiwa na changamoto hizi, “ kuzingirwa na mawazo” kulifanya mamlaka kuwa wakali na kuminya kwa nguvu wale walioonekana tishio.
Taasisi ya kimataifa inayojihusisha na haki za Binadamu (The Human Rights Watch) mwezi Mei 2018 katika taarifa yake maalumu iliweka wazi kuwa majeshi ya nchi ya Burundi, usalama wa taifa na wanachama wa umoja wa vijana wa chama kinachotawala ambao wanajulikana kama Imbonerakure walifanya ukatili wakilenga wapinzani, wanaharakati wa haki za binadamu na waandishi wa habari, “wakiuwa watu wapatao 1,700, ubakaji, mateso, kupigwa, vitisho na kukamata watu ovyo.”

Hii imesababisha mgogoro wa wakimbizi ambao umepelekea warundi kukimbilia hasa Tanzania, Rwanda, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Uganda. Wakati maelfu wamerudi, shirika la wakimbizi la Umoja wa mataifa (UNHCR) lilitoa taarifa ya zaidi wakimbizi wa Burundi 347,000 mwezi Februari 2019. UNHCR inadai:

…vurugu za kisiasa Burundi zilikuwa mbaya sana mwaka 2015 baada ya Rais kutangaza mpango wa kugombea kuongoza kwa muhula wa tatu. Maandamano mtaani yalipelekea mapigano makali na mamia elfu walikimbilia nch jirani kutafuta usalama.”

Mapema mwezi huu Burundi imefunga ofisi za shirika la umoja wa mataifa linalojihusisha na haki za binadamu baada ya kukaa humo miaka 23, ikisema kuwa halihitajiki tena. Serikali ilikasirishwa na kamishina wa zamani wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na haki za binadamu ndugu, Zeid Ra'ad Al Hussein, ambaye mwezi Februari mwaka 2018 alieleza Burundi ya Nkurunziza kama moja ya “nyumba iliyochinja watu wengi sana hivi karibuni”.

Vyombo vya habari na magazeti kufungwa, unyanyasaji kwa wapinzani, kuyaminya mashirika binafsi na kuminywa kwa nafasi za kisiasa za kuzungumza na kutoa maoni.

Kwa mfano, mwanaharakati wa kijerumani Rukiki ambaye aliandika juu ya vitendo vya mateso yaliyofanywa na utawala wa Nkurunziza alihukumiwa kwenda jela miaka 32 mwaka 2018 kwa madai kwamba “alishiriki katika mpango wa kuipinga serikali,” “alidhohofisha usalama wa taifa” na “uasi.” Kesi ya Rukiki ilighubikwa na ukiukwaji wa taratibu za uendeshaji kesi na ililetwa kabla ya kura ya maoni ya katiba yenye utata.

“Suala la kuchorachora” pia ni moja ya viashiria vya serikali isiyobadilika, inayokatisha tamaa ukijumuisha ndoa za kulamisha mwaka 2017 kwa kuwafanya wachumba ambao hawajaoana kukaa kinyumba, kuminya makahaba na omba omba.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.