- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mwanaharakati Ahmed Mansoor Aliyefungwa UAE Aendelea na Mgomo wa Kutokula

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Umoja wa Falme za Kiarabu, Haki za Binadamu, Harakati za Mtandaoni, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, GV Utetezi

Mwanaharakati wa Haki za binadamu Ahmed Mansoor sasahivi anatumikia kifungo cha miaka kumi jela katika Falme za Kiarabu. Picha na: Taasisi ya Martin Ennals, kupitia Citizen Lab.

Mtetea haki za binadamu katika Falme za Kiarabu Ahmed Mansoor ameendelea na mgomo wake wa kutokula ulioanza tangu katikati ya mwezi Machi 2019. Wafuasi wake wanasema afya yake imedhoofika sana.

Maafisa usalama walimkamata Mansoor nyumbani kwake tarehe 20, mwezi Machi 2017 kutokana na maoni aliyoyatoa mtandaoni. Mwezi Mei 2018, alihukumiwa [1] chini ya sheria ya makosa mtandaoni ya mwaka 2012 ya “kutukana ustawi na heshima ya Falme za Kiarabu” na “kuchapisha taarifa za uongo na habari katika mitandao ya kijamii zinazoharibu uhusiano wa Falme za Kiarabu na nchi majirani zake.” Mahakama ilimuhukumu [2] miaka kumi jela na faini ya 1,000,000 fedha ya Falme za Kiarabu (sawa na dola za Kimarekani 270,000).

Mansoor amekuwa akitetea mageuzi ya kisiasa na kulinda haki za binadamu nchini mwake na barani kwa zaidi ya muongo mmoja. Ni mshindi wa Nobel wa taasisi ya Martin Ennals 2015, [3] ambayo hutetea na kulinda haki za binadamu ambao wapo katika hatari. Ni mwanachama wa shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch Mashariki ya kati na Kamati ya ushauri Kaskazini mwa Afrika.

Hii si mara ya kwanza kwa Mansoor kuwekwa kizuizini. Mwaka 2011, yeye na wanaharakati wa kisiasa wanne walifungwa jela [4] kutokana na kuhusishwa na kuendesha mjadala mtandaoni kupita UAEHewar.net. Pia alitumia jukwaa hilo kuchapisha ombi akiomba mageuzi ya kisiasa katika Falme za Kiarabu. Maafisa usalama waliutumia wito huo kama msingi wa kumshtaki Mansoor kwa kutukana viongozi wa Falme za Kiarabu. Alitiwa hatiani na kuhukumiwa miaka mitatu jela lakini aliachiwa huru [5] kwa msamaha wa Rais baada ya kutumikia miezi saba tu.

Kabla ya kukamatwa kwake mwaka 2017 alipiga kampeni mtandaoni kwa niaba ya wanahakati waliokuwa wamefungwa jela katika Falme za Kiarabu na mahali pengine. Siku moja kabla ya kukamatwa kwake alituma ujumbe kupitia tweeter [6] juu ya kuendelea kukamatwa kiholela kwa mwanaharati katika Falme za Kiarabu Osama al-Najjar [7], ambaye ameendelea kuwepo jela ingawa amemaliza [8] kifungo chake cha miaka mitatu jela. Kutokana na shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch, pia alisaini [9] barua ya pamoja na wanahakati wengine wakiomba viongozi wa The Arab League katika mkutano mkuu wao mwezi Machi 2017 huko Jordan kuawaachia wafungwa wa kisiasa katika nchi zao.

Mwezi Desemba 2018, Baraza la usalama wa taifa la Mahakama kuu ya Shirikisho ambalo ndilo lenye maamuzi ya mwisho, lilithibitisha hukumu yake ya miaka kumi.

Kutokana na kituo cha Ghuba cha haki za binadamu (GCHR), Mansoor alianza [1] mgomo ”kupinga hali mbaya ya gerezani na uendeshwaji mbaya wa kesi yake”:

sasa hivi Mansoor amefungwa katika gereza la Al-Sadr lililopo Abu Dhabi, ambapo amewekwa peke yake. Chanzo kiliiambia GCHR kwamba amefungwa katika “hali mbaya” katika chumba kidogo bila kitanda, maji na hakuna bafu. Afya yake imedhoofika sana na yupo katika hali mbaya.

Makundi ya watetezi wa haki za binadamu wameeleza kuguswa na afya ya mwanahakati huyo, na kuomba mamlaka za UAE kumuachia huru.

“Ahmed Mansoor anahatarisha afya yake akiomba uangalizi wa kifungo chake cha dhuruma kwa sababu alitetea jamii ya uvumilivu na Maendeleo ambayo Falme za Kiarabu hudai kujenga,” alisema [9] Sarah Leah Whitson, Mkurugenzi wa taasisi ya haki za binadamu ya Human Rights Watch katika Mashariki ya kati. “Mamlaka za UAE zinapaswa haraka na bila ya maasharti kumuachia Monsoor ili aendelee kutumika kama sauti kwa ajili ya haki katika bara hili kwa kuwa inahitajika sana,” aliongeza.

Kampeni ya kimataifa ya uhuru katika UAE iliomba [10] mamlaka kumhudumia Mansoor kwa kufuata viwango vya haki za binadamu kimataifa na kuruhusu makundi ya kimataifa ya haki za binadamu kumtembelea.

Tunasistiza wito wetu wa kuachiwa huru Ahmed Mansoor haraka na bila ya masharti. Kutokana na hili, tunashauri mamalaka za Falme za Kiarabu kumhudumia kwa kufuata viwango vya chini vya Umoja wa mataifa vya kuhudumia wafungwa ambavyo vinaruhusu utolewaji wa matibabu na usafi magerezani. Ili kuhakikisha hili, ni muhimu mashirika binafsi yaruhusiwe kuingia na kumtembelea Mansoor.

 

Jifunze juu ya athari za kimwili zinazotokana na mgomo wa kutokula kwa kutumia mkusanyiko wa maandishi na majdwali hapa chini, iliandaliwa na washirika wa Visualizing Impact.