Katika kuzindua bunge la jimbo lake hapo Januari 31, makamu mpya wa Brazili aliyechaguliwa karibuni Ana Paula da Silva alivaa nguo angavu nyekundu na mapambo. Aliweka picha ya tukio hili katika ukurasa wake wa Facebook na, siku iliyofuata aliamka na kukutana na mafuriko ya maoni yenye chuki. Sababu: Kifua chake.
Ana Paula da Silva ni mmoja wa wanawake watano kati ya wabunge 40 waliochaguliwa katika bunge la Santa Catarina, jimbo la kusini mwa Brazili.
Picha yake ilipata maoni 6,400 na ilishirikishwa mara 6,447 ikiambatana na vitisho na matusi mengi.
Lakini kwa Brazili hii sio mara ya kwanza uchaguzi wa nguo kwa mwanamke kuingilia uwezo wake katika sehemu ya kazi kuleta shida.
Muongozo wa wanaume juu ya mavazi ya kike
Mwaka 2009, kansela wa mji wa Porto Alegre, Fernanda Melchionna aliingia katika kikao cha ndani akiwa amevaa tai yenye mistari miyeusi na nyeupe akipinga muswada uliokuwa unataka kupitisha aina ya mavazi kwa ajili ya wabunge wanawake.
Melchionna, ambaye sasa ni makamu wa jimbo, mara nyingi huenda kazini akiwa amevaa jinzi au nguo za michezo na watumishi wenzake wa kiume huona kuwa sio sawa.
Alisema kuwa mijadala juu ya nguo za wanawake inawafaa “wavivu, wale wasiotumia mamlaka zao kushughulikia changamoto za kijamii.”
Sio katika siasa pekee wanawake wanakumbana na masuala kama hayo. Mwaka 2017, mwanasheria Pamela Helena de Oliveira Amaral aliapa kumshitaki jaji baada ya kuahirisha kesi na kuanza kukosoa mavazi yake. Pamela alikuwa amevaa gauni refu la bluu ambalo lilikuwa likionesha mabega yake. Jaji Eugênio Cesário aliondoka ukumbini na alirudi baada ya Pamela kuazima nguo ya kujifunika kutoka kwa mfanyakazi mwingine wa kike.
Pamela alisema katika mahojiano katika kipindi kile kuwa:
Eu fiquei estarrecida, sem entender. Não assimilei até agora. Foi humilhante, vergonhoso e constrangedor o que ele me fez passar na frente dos meus colegas. A sala estava cheia de estudantes e advogados.
Nilishangazwa na kuchanganyikiwa. Bado sijaelewa kwa ujumla. Alichofanya nipitie kilinidhalilisha na kutia aibu mbele ya wenzangu. Ukumbi ulikuwa umejaa wanafunzi na wanasheria wengine.
Katika chapisho lenye kichwa “Nguvu ya Msichana na Nguvu ya Mavazi: uanamke katika siasa”, mwanablogu Nawsheen Rumjaun alichambua jinsi watu wanavyopenda kuchukulia uchaguzi wa nguo kwa wanawake katika mazingira ya kisiasa:
[…] Idadi ya wanawake wenye nguvu inaongezeka, lakini bado ni ngumu sana kuwa mwanamke katika siasa. Nguo wanazochagua zinageuka kuwa silaha ya kuweka misingi ya mamlaka yao katika ulimwengu huu wa wanaume. Katika siasa hakuna muongozo wa mavazi lakini kuna sheria bubu kwamba wanaume watavaa suti na wanawake watavaa nguo za heshima. Wale wanaovuka mstari ule ulio kati ya kile kinachodhaniwa kuwa ni ya heshima na isiyo ya heshima wapo katika hatari ya kulaumiwa kwa sababu ya mavazi yao.
Urefu wa Mstari wa Shingo
Ana Paula alipata kura 51,739 na kumfanya mbunge wa tano ambaye alishawahi kupigiwa kura nyingi jimboni kwake.
Katika mahojiano na Universa, tovuti ya nyumbani inayojihusisha na masuala ya wanawake, alisema hivi kuhusu mashambulizi aliyopokea: ” Ushiriki wa wanawake katika jamii ni mdogo sana kiasi kwamba mstari wa shingo tu unaweza kuwa jambo kubwa sana,” alisema.
Pia aliweka video katika ukurasa wake wa Facebook akijibu mashambulizi hayo. Hata hivyo, maoni katika video hiyo yalikuwa yamejaa matusi. Mtumiaji mwenye jina Vitor alisema:
Com todo respeito, mas você se esqueceu em qual ambiente trabalhará nos próximos dias? Formalidade por favor. Tenha respeito! Decoro parlamentar.
Kwa heshima kubwa, je umesahau ni katika mazingira gani utakuwa unafanya kazi siku chache zijazo? Ustaarabu tafadhali. Kuwa na heshima! Jamala wa Bunge.
Mtumiaji mwingine mwanamke anayeitwa Yelena Sier, alipokea maoni 252 ndani ya maoni yake ambapo alimkosoa mwanasiasa huyo:
Geral não entende!! Ninguém vai no hospital com biquíni, as crianças não vão a escola de pijama, os homens não vão comprar pão só de cueca, ninguém vai fazer uma cirurgia com qualquer roupa, ninguém vai para uma festa de 15 anos ou um casamento de pijama, etc… cada ocasião uma traje adequado, nas empresas existem uniformes e assim por diante, e todo mundo sabe disso. A questão não é a roupa que a mulher usa ou deixa de usar, mas para cada local um traje adequado.
Watu hawaelewi!! Hakuna mtu huenda hospitali akiwa amevaa bikini, watoto hawaendi shuleni wakiwa wamevaa nguo za kulalia, wanaume hawaendi kununua mkate wakiwa wamevaa nguo za ndani na hakuna mtu anaweza fanya upasuaji akiwa amevaa nguo holela, hakuna mtu anaweza kwenda harusini akiwa amevaa nguo za kulala n.k… Kila tukio lina mavazi yake rasmi, katika makampuni kuna sare na kadhalika na kila mmoja anajua hilo. Jambo la msingi hapa sio ni kitu gani mwanamke amevaa au hakuvaa lakini kila sehemu ina mavazi yake rasmi.
Katika chapisho lingine tofauti Rosimere Furtado alitetea haki ya Ana Paula kuvaa kama atakavyo:
Parabéns pela discussão levantada! Enquanto uma Deputada com vestes comportadissima levanta discussões perseguindo Educadores e afirmando que a Educação não necessita de investimento financeiro, a senhora levanta discussão sobre a importância da mulher na política, sobre feminicidio, sobre causas que independe da cor ou traje. Em um “mundo” onde a mente é deturpada e a sexualidade é esarcebada, qualquer decote é uma guerra!!!
Hongereni kwa kuibua suala hili! Wakati mwakilishi wa jimbo akiwa katika mavazi ya heshima ya hali ya juu akiwakisoa waalimu na akisema kuwa elimu haihitaji uwekezaji wa fedha, mmeanzisha mjadala wa umuhimu wa wanawake katika siasa na sababu ambazo ni uhuru wa rangi au mavazi. Katika “ulimwengu” ambapo fikra haziwakilishwi ipasavyo jinsia hukosolewa na nguo ya kuonesha kidogo huwa sababu ya vita!!
Ana Paula aliwajibu wanaomshambulia kwa kuwakumbusha historia yake: kabla hajachaguliwa kuwa mbunge, alishachaguliwa mara mbili kuwa meya wa mji wa Bombinhas na aliiacha ofisi ikiwa na ufanisi wa kukubalika kwa asilimia 90.
Ana Paula pia aliposti katika ukurasa wa Facebook mahojiano ambapo alisema: “Wanawake wapo katika siasa na jamii inatakiwa ianze kuwazoea kama walivyo. Kuna mambo mengi ya msingi kwa bunge la wawakilishi kujadili.”
Pia aliyahifadhi mashambulizi hayo na kusema kuwa atawashitaki watu waliomdhalilisha. Alimwambia mhojaji mwingine :
Vou continuar vestindo o que eu quero. Não pretendo me violentar para agradar ninguém
Nitaendelea kuvaa ninavyotaka! Sikusudii kujiumiza mwenyewe kwa kuwafurahisha wengine.