Askari Polisi wa Uganda Wamuua Mtu Kimakosa kwa Kumpiga Risasi Wakidhani ni Kiongozi wa Kisiasa

Picha Waziri wa Nchi Teknolojia, Habari na Mawasiliano Idah Nantaba iliyopigwa kwenye video ya Youtube ambaye alinusurika kuuwawa katika jaribio la mauaji.

Tarehe 24, mwezi Machi, 2019, ilitangazwa habari kuwa Waziri wa nchi Teknolojia, Habari na Mawasilano Mheshimiwa Idah Nantaba amenusurika na jaribio la mauaji na kwamba askari wa Uganda wamebahatika kumpiga na kumuua mmoja wa washambuliaji katika mji mdogo wa Nagojje ulipo kilometa 53 Mashariki mwa mji mkuu Kampala.

Kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita, matukio mbalimbali ya mauaji ya viongozi vigogo wa kisiasa, kidini au kijeshi yamesababisha kuwepo kwa hukumu chache halisi au taarifa sahihi kuhusu matukio hayo. Wananchi wa Uganda walirahisishiwa kwa mara kwanza kwa kusikia kwamba askari wamechukua hatua za haraka.

Hata hivyo, habari ya kuchanganya imeibuka kuhusu mtu hasa aliyeuawa.

Nantaba aliwataarifu askari polisi akiwathibitishia kwamba wanaume wawili waliokuwa wanaendesha pikipiki walikuwa wanamfuatilia kwa zaidi ya kilometa 40. Askari polisi walichukua hatua na kuwazuia wanaume wawili waliokuwa kwenye pikipiki karibu na mji wa biashara wa Nagojje.

Ronald Ssebulime, mwenye miaka 40, na ambaye ni baba pekee wa watoto wanne alikuwa akiendesha pikipiki na akiwa amebeba abiria. Polisi walikosea wakidhani kuwa watu wawili ndio waliokuwa wakitaka kumshambulia Nantaba na walijaribu kuwakamata waliokuwa wakiendesha pikipiki. Kulitokea purukushani ya kukimbizana na Ssebulime aligonga nundu. Wale watu wawili walitelekeza pikipiki na kujaribu kutoroka kwa mguu, lakini askari polisi walipiga risasi hewani na mwisho Ssebulime alisalimu amri. Abiria wake alikimbia.

Ssebulime aliwasihi kuwa yeye hana hatia lakini askari polisi walipiga pingu na kumtupia ndani ya gari la polisi. Waliendesha kwa umbali mfupi na kisha walisema “amri imebadilika” kabla hawajampiga risasi na kumuua, haya yalitolewa na mashuhuda wa tukio hilo waliongea na NTV ya Uganda.

Shahidi mmoja alisema:

[Ssebulime] alichukuliwa kutoka kwenye gari dogo la doria [akiwa amefungwa] pingu na kupigwa risasi.

Mwingine alisema:

Askari polisi alirudi hatua mbili nyuma na kumpiga risasi mara mbili..

Uchunguzi mbovu

Mshangao uliofuata, askari walituma ujumbe kupitia tweeter kwamba kumpiga risasi ilikuwa ni halali kwa sababu watu waliokuwa wanaendesha pikipiki walikataa kusalimu amri:

Risasi kadhaa zilipigwa kuelekea upande wao ili waweze kusalimu amri lakini ilikuwa bure. Katika harakati hizo Sebbulime Ronald mkazi wa Kijiji cha Nakabugo, katika kata ya Nakabugo, kaunti dogo ya Pakiso iliyopo kaunti ya Busiro katika wilaya ya Wakiso alipigwa risasi na kuuawa katika purukushani

Waliongeza kusema kuwa mshukiwa wa pili alitoweka na wanahofia kuwa ni hatari kwa kuwa ana silaha, angawa askari polisi hawakuthibitisha hilo.

tarehe 24 Machi 2019, Jeshi la polisi Uganda lilisema; Askari polisi wanaendelea kutafuta kwa kutumia mbwa eneo alipo mshukiwa wa pili ambaye anaogopwa kuwa na silaha na ni hatari. Tunataka kuutaarifu umma kuwa waziri, ingawa anahofu yupo salama na hakushambuliwa kama ilivyolipotiwa na vyombo vya habari.

Mzungumzaji wa jeshi la polisi Fred Enanga alisema kwamba waziri, mashahidi na maafisa polisi waliohusika katika kupurkushani wangetoa kauli wakati wanaendea kuchunguza kumbukumbu zilizomo kwenye simu ya Ssebulime pamoja na karatasi za usajiri wa pikipiki yake..

Irene Nakazibwe ambaye ni dada yake na marehemu anasistiza kuwa kaka yake alikuwa katika nafasi na muda usiyosahihi. Katika mahojiano, Nakazibwe alisema, kwa kweli Ssebulime alikuwa anaelekea shule ya sekondari ya Mt. Andrews kutembelea watoto wake wawili wanaosoma kidato cha kwanza na cha tatu. Waliongelea suala la kufanya matembezi hayo mapema siku ile. Ssebulime alifiwa na mke wake mwaka 2012 na amekuwa akitunza watoto wake wanne akiwa ndiye mzazi pekee.

Haijulikani kwa nini alijaribu kuwakimbia askari polisi wakati ana kitambulisho cha taifa na leseni ya udereva. Nakazibwe alieleza habari hiyo NTV ya Uganda:

Tarehe 27 mwezi Machi, 2019,askari polisi walikubali kwamba Ssebulime aliuwa kimakosa na maafisa wa polisi na walitoa pole kwa familia ya marehemu. Pia, walithibitisha kuwa Ssebulime alikuwa hana silaha yoyote na alikuwa amebeba mkoba uliokuwa umejaa vinywaji vya soda na chakula kwa ajili ya Watoto wake.

Boda-boda Wazimu

Kifo cha Ssebulime kimeibua hisia tofauti miongoni mwa waendesha pikipiki au pikipiki za kukodiwa ambao ni usafiri rahisi. Angalau vifo vinavyohusisha vigogo watano wakiwemo wakuu wa jeshi, Wabunge, viongozi wa dini vimetokea katika miaka mitatu iliyopita — vyote vikisababishwa na kuwagonga waendesha pikipiki .

Hii imewafanya waendesha pikipiki na maofisa wakubwa kuwa makini zaidi.

Mtumiaji wa Twitter, Ganda Gannyana anafikiri kuwa sababu ya Ssebulime kuuwa bila kuchukuwa tahadhali yakutosha inatokana na maelekezo yaliyotolewa baada ya kuuawa kwa mheshimiwa Mbunge Ibrahim Abiriga — Rais Yoweri Museveni alisema pindi kiongozi anapomhisi mtu yeyote anamfuatilia akiwa na nia mbaya, wanapaswa “kumuondoa” mtu huyo.:

Mtumiaji wa Twita Ganda Gannyana anasema; Yalikuwa maelekezo ya kipuuzi kutoka kwa Kaguta Museveni kwa kumhisi tu yeyote anakufatilia “muondoe” kwanza halafu waliobaki tutawaondoa baadaye. Sasa unaonaNow see!? Mtu asiyekuwa na hatia. Ssebulime Ronald amechinjwa.

“kupigwa risasi ukiwa umefungwa pingu;” hayo ni makusudi

Mtumiaji wa Twitter Kyeyune Moses anaona mkanganyiko kwenye kifo cha Ssebulime:

Mtumiaji wa Twitter Kyeyune Moses anaona mkanganyiko kwenye kifo cha Ssebulime.Habari ya Ronald Ssebulime ni kubwa sana is bigger than meets the eyes. Kuna habari tofauti kuhusu nani aliyemuua “anayedhaniwa kuwa mshambuliaji”na namna alivyoua.
Lakini habari inayogusa ni kuhusu watoto walioko shuleni sasa. Walipoteza mama yao, na baba yao ametoweka sasa. Je, haki itatendeka?

Mtumiaji wa Twitter Angelo Peter alighadhabika kwamba askari polisi walishindwa kutoa ushahidi kuwa Ssebulime ni hatari kabla ya kumuua:

Mtumiaji wa Twitter Angelo Peter alighadhabika kwamba askari polisi walishindwa kutoa ushahidi kuwa Ssebulime ni hatari kabla ya kumuua: Walipotaka kumfunga Bobi Wine kwa uhaini walionesha bunduki waliyoipata katika chumba chake hotelini ndani ya masaa 24. Lakini hawawezi kutuonesha bunduki aliyokuwa nayo Ssebulime kabla hawajamuua.

Alipongea na waandishi wa bahari kwa ufupi, Nantaba alisimulia habari yake na kuuliza maswali juu ya nani aliyepewa amri ya kumuua Ssebulime. Alipendekeza mazingira mazima ya tukio hilo inawezekana yamepangwa na waongozaji wa mauaji wa watu wakubwa— na bado anaamini Ssebulime ameangukia katika jaribio la kumuua:

Mipango ya mauaji haya ambayo yamekuwa yakitokea katika nchi yetu na kutokana na kile tunachokiona kitaendelea kwa sababu [Ssebulime] alikuwa ni mtu ambaye alipaswa kuwa shahidi lakini alikuwa wa kwanza kuuawa !

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.