- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Wanaharakati Nchini Iraki Wapaza Sauti Kupinga Muswada wa Makosa ya Mtandaoni

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Iraq, Haki za Binadamu, Sheria, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, GV Utetezi

Baghdad. Picha ya MohammadHuzam [CC BY-SA 4.0 (https://creativecommons.org/licenses/by-sa/4.0)].

Makundi ya Haki za Binadamu na Wanaharakati wanashauri Bunge la Irak kutupilia mbali Muswada wa makosa ya Mtandaoni ambao utazuia sana uhuru wa kutoa maoni mtandaoni kama utapitishwa.

Muswada unaweka hukumu ya kifungo kirefu cha gerezani kwa makosa yanayotokana na kauli ambazo hazikuelezwa vizuri katika mswada huo. Ibara ya 3 inatamka kifungo cha Maisha jela na faini kali kwa wale wanaokutwa na hatia kwa kutumia “kompyuta na mtandao” “kudhoofisha uhuru, uadilifu na amani ya nchi, au Uchumi wake, Siasa, jeshi au maslahi ya nchi” au “kusababisha ugomvi wa kidini, kuvuruga amani na utulivu, au kuharibu heshima ya nchi.”
Ibara ya 4 na 6 zinaweka adhabu kama hiyo kwa wale watakaokutwa na hatia ya kuchochea ” vitendo vya kigaidi na kuwa na mawazo ya namna hiyo” (Ibara 4) au ”Kuchapisha au kutangaza taarifa za uongo au za kupotosha zenye nia ya kudhoofisha uimara wa mfumo wa fedha wa kielektroniki ” (Ibara ya 6.)

Mapema mwaka huu, kituo cha Haki za Binadamu cha Gulf kilitahadharisha [1]:

“Bila kuwepo maana iliyo wazi ya ugaidi, itakuwa rahisi kutumia sheria hiyo kufilisi rasilimali za wapinzani wakisiasa na wanaharakati wengine.”

Haki za mtandaoni tayari zinakiukwa Irak. Majira ya kiangazi yaliyopita, mamalaka zilijibu maandamano [2] kukemea rushwa na Maisha ya anasa katika Basra na miji mingine kwa kuzima [3] mtandao.

Kama utapitishwa, mswada huo utafanya iwe vigumu kwa Wairaki kutumia haki zao za kuwasiliana, kuongea kwa uhuru na kupata habari mtandaoni.

Mapema mwezi huu, makundi tisa ya haki za binadamu pamoja na AccessNow, Amnesty International na waangalizi wa haki za binadamu walichapisha kauli [4] ya kuliomba bunge la Irak kutupilia mbali mswaada huo.

…Sheria hii itawafanya watumiaji wa mtandao kuwa waoga katika kutumia haki zao za msingi na uhuru wa kutumia mtandao na itaondoa haki ya kutoa maoni. Pia, sheria ina athari kubwa katika kufurahia haki na uhuru wa habari na haki ya kushiriki katika mambo ya umma katika nchi ya Irak.

Bunge lilitazamia kujadili mswada huo tarehe 4 Machi, lakini baadaye uliondolewa.

Katika akaunti ya Twita ya Afisa wa Baraza la Bunge la Irak aliwashukuru [5] wale wote waliofanya mawasiliano ili “kukosoa baadhi ya sheria,” lakini hawakuweka bayana ni sheria zipi. Makundi ya haki za binadamu na wanaharakati walipokea jibu hilo kwa furaha, lakini bado wana wasiwasi.

Ushindi mdogo: Kutokana na kampeni iliyofanywa na wanaharakati wa haki za binadamu, waandishi wa habari ndani na nje na Mashirika yasio ya kiserikali kufanikiwa kuondolewa kwa rasimu ya uhalifu mtandaoni kutoka
ratiba ya Bunge hatua inayofuata nikuondolewa kwa rasimu ya sharia kwa pamoja!
Tarehe 14 Machi, 2019

Haijaeleweka vizuri kama Bunge litaufanyia marekebisho mswada huo au kuupanga tena ili ujadiliwe